Januari Makamba: Wanaohoji kuchelewa Mradi wa JNHPP ni upuuzi tu

Kaka Makamba, kama unasoma hizi text elewa watanzania walikuwa na imani kubwa sana juu yako ila wewe mwenyewe uliiharibu na kuipunguza hiyo imani baada ya kuonekana unamkandia Dkt Magufuli. Pamoja na kuwa uliomba msamaha na Dkt Magufuli alikusamehe ila baada ya kifo chake ulionekana mwenye kufurahia kifo chake. Kosa lingine ulipoingia wizarani hapo kwenye nishati ulijinasibu kwa kusema serikali ya Dkt Magufuli chini ya uongozi wa wizara wa Dkt Kalemani TANESCO iliharibiwa, na kibaya zaidi ukasema eti kuna hujuma na ukaamua kuondoa top management yote. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana ambalo wafanyakazi wa TANESCO mpaka leo umeonesha kwa kuwaambia unawaamini japo imani yao kwako haipo. Je ufanyeje? Nadhani jitahidi kukaa kimya, usipende kuongea ongea kwa sababu kila kauli yako adui zako wanaibeba na kuifanya ajenda. Kumbuka adui ulio nao ni wengi ukiacha na watanzania wanaokuchukia kwa sababu ya kumdharau Dkt Magufuli, kuna hawa wasaka urais, wanataka utu wako uchafuke ili ukose nafasi ya kuja kuwa Rais
 
Tatizo la kutokuaminika ni huko kukunja mikono ya shati
 
Hilo bwawa lingeisha bei ya umeme ingepungua pia na hao watu huko kijijini ulikopeleka majiko ya gesi wangetumia majiko ya umeme. Weee nini bwana unatuon a sisi mazuzu malizia mradi weee shubamiti
 
Mkuu 'denooJ' ingependeza sana kama akikusoma kwa haya uliyomjibu hapa.

Kwa maneno hayo ya kutaka auliwe, ni ishara kwamba huyu waziri mambo yamemzidi kimo. Ubabaishaji umekuwa mwingi mno! Yeye na Mwigulu ni mawaziri wasioaminika kabisa!
 
Amejibu kirejareja mno!, issue nzito majibu mepesi mepesi.
 
Hilo bwawa lingeisha bei ya umeme ingepungua pia na hao watu huko kijijini ulikopeleka majiko ya gesi wangetumia majiko ya umeme. Weee nini bwana unatuon a sisi mazuzu malizia mradi weee shubamiti
Umeme utakapo kuwa nafuu kabisaa tutatumia majiko ya umeme na ya gesi hatutayahitaji tena, HAPA PANA GAME INACHEZWA KULINDA GAS NA GHARAMA ZAKE.
 
Makamba ni akili kubwa, si mtu wa kukurupuka au kueleweka kirahisi rahisi tu na vilaza..........mnataka majibu ya kistaarabu kwani nyie mnamkosoa kistaarabu?!!!

Makamba anaonewa wivu,
Makamba anaogopwa,
Makamba mwanasiasa mahiri (li?),
Makamba amewazidi wengi sana akili.

Ni mvumilivu sana huyu makamba hata hivyo......kuna kundi la watu limempania kweli kweli kumchafua na kumharibia ndo maana kila siku humu hazikauki hoja za kumkandia, kisingizo sasa kikiwa ukamilishaji wa bwawa la Nyerere utafikiri bwawa hilo ni sawasawa na ujenzi wa madarasa ya UVIKO 19 kwamba yanawahishwa kwa ajili ya f1.
 
Kwa hiyo bwawa limeisha??
Yeye alianza kwa uongo uongo wa lengo la kuhujumu bwawa ambalo ni hazina ya nchi.
Hilo halikubaliki asilani. Tutamkimbiza kama paka mwizi.
Mbona mimi nakuona unakimbia wewe kamanda?!!!
 
HII NI SEHEMU YA TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI ILIYOWASILISHWA BUNGENI FEBRUARI 15, 2022 AMBAO WAZIRI WA NISHATI ANATAMKA HADHARANI KWAMBA NI WAPUUZI
EeenHeee!

Hivi na hawa kawaingiza kwenye kundi la "wapuuzi"?

Inafaa wamwite ajieleze mbele zao alikuwa na maana gani katika matamshi yake. Wamtake atoe ripoti ya maandishi kujibu hiyo ripoti yao kuonyesha alipoona upuuzi.
 

Kitu pekee alichonacho huyu pimbi ni entitlement mentality. Hana sifa za kuongoza wizara muhimu kama hii. Yeye na mteuaji wake wote hawatoshi kwa hizo nafasi wanazozishikilia!
 
Hilo la kumtaka asitamke kitu akae tu kimya umemshauri vema, lkn kisa eti jpm siamini sana kwani mbona jk amesemwa mara kusemwa na huyo jpm na watu walikuwa wanafurahia tu?!!!
 
"Ukiona nguchiro anakufanyia mbwembwe,jua yupo karibu na shimo lake".

Makamba anasadikika kuwa smart ila tu akiwa amenyamaza,akiongea ni either pumba au upupu au vyote.

Huo utitiri wa vitabu wanavyosoma kila mwaka na mwenzie Zitto haviwasaidii zaidi ya kuwafanya arrogant.
 

Nafasi ya Kuja kuwa Rais ?
 
Hilo la kumtaka asitamke kitu akae tu kimya umemshauri vema, lkn kisa eti jpm siamini sana kwani mbona jk amesemwa mara kusemwa na huyo jpm na watu walikuwa wanafurahia tu?!!!
Mtu aliyekufa huonewa huruma hata kama alikuwa na makosa binaadamu tuna utamaduni wa kufuta. Pia Dkt Magufuli hakumsema JK bila uthibitisho, mara zote ushahidi wa mabaya ya wote watangulizi wake yaliwekwa wazi na yeye kufanya maamuzi magumu kwa kuwafafanulia wananchi. Hivyo unapomsema vibaya Dkt Magufuli inabidi uwe makini mno. Ndiyo maana ushauri huu ndugu yangu Makamba auzingatie, he won’t loose anything kwa kumsifia Dkt Magufuli kwa sababu ndiyo chanzo hata cha yeye kuwa maarufu
 
Hivi vijabio vya sa100 vina kiburi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…