wababayangu
JF-Expert Member
- Jul 17, 2021
- 814
- 1,107
Kigogo mnafiki sana.Mh. January Makamba, kuwaongopea na kuwadanganya wananchi haina afya kwa taifa. Kama wizara hii uliikuta na makando kando mengi, ni vyema ukakaa pembeni ili usipoteze sifa yako ya uongozi.
TANESCO wanatangaza mgao tena, yaani watu warudi kwenye manunuzi ya generator? Ni shughuli ngapi za kiuchumi zitakuwa zinakwama kwa kukata umeme? Hasara itakayopatikana nani wa kuifidia?
Wakati wa JPM haya mambo tulishayasahau, mnataka tena turudi kule, huko wapi uchumi wa kati.
Alisema mabwawa yamekauka wananchi wakapiga kelele mgao wa umeme ukasitshwa. Akaja na 2nd slogan kwamba mitambo ni mibovu eti kwa sababu mafundi waliogopa kuizima ili waifanyie matengenezo kwa kumuogopa JPM. Nalo hilo likipita kimya kimya. Sasa ndiyo kaja mazima kwamba lazima umeme uzimwe kwa sababu generators zilikuwa zikiozea madukani.
Hatua tatu mbele tano nyuma. Tunashukuru sana mama kwa uteuzi wako