Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

Hii thread imebeba ujumbe muhimu na mzito kwetu lakini kwa sababu haina chadema wala sheikh ponda ndani inaonekana ya hovyo

Nilizani kuwa kwako nje ya nchi ungekuwa una mambo chanya kwa vijana wenzako ambao atujaenda Ulaya,jadili Mnakasha
Narudi katika uzi nitakuwa wa mwisho kupongeza sababu Matukio na Matokeo ni vitu tofauti
"Vox popoli vox dei"
 
Safi kabisa. Wanaobeza ziara za Mhe. Rais nje ya nchi wanune wasinune wamesikia.

komboka kichwani wewe! we unadhani ni akili sana kucheza position zote peke yako? forward ucheze wewe, winga zote mbili wewe, beki mwenyewe! we unaona akili sana hiyo? alienda kwenye kazi za waziri wa fedha WEF, alienda kwenye kazi za waziri wa nje AU, alienda kwenye kazi za mambo ya ndani SADC. Serekali siyo duka la Mkinga mmoja hilo wewe....
 
10/08/20130
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • Japan yatangaza sera mpya kwa Tanzania Sasa Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan
  • Japan itasaidia Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji katika Afrika
  • Kushiriki maboresho Reli ya Kati
  • Kusaidia kupanua na kuboresha Bandari ya Dar Es Salaam
  • Viwanda vya Japan kujengwa nchini kikiwemo cha kutengeneza pikipiki za Honda
  • Ni matokeo ya Ziara ya Rais Kikwete Japan
JAPAN imeamua kuanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania ambako nchi hiyo itaifanya Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan na kuiwezesha kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji katika Afrika kwa nia ya kuiwezesha kuwa na uchumi ulioimarika na wenye kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi.

Uamuzi huo wa Japan ni matunda ya mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Shinzo Abe yaliyofanyika Tokyo, Japan wakati Rais Kikwete alipotembelea nchi hiyo Juni, mwaka huu, 2013.

Uamuzi na msimamo mpya wa Japan umetangazwa rasmi leo, Jumamosi, Agosti 10, 2013 na Waziri wa
Uchumi, Biashara na Viwanda wa nchi hiyo, Mheshimiwa Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.

Kwa upande wa Tanzania, mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anashughulika na Uwekezaji na Uwezeshaji Mheshimiwa Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe.

Waziri Motegi amemwambia Rais Kikwete kuwa ametumwa na Waziri Mkuu Abe kufuatilia mazungumzo kati yao na kutangaza rasmi kuwa Japan imeiteua Tanzania kuwa nchi lengwa na kitovu cha uwekezaji wa Japan katika Afrika Mashariki na katika Afrika kwa jumla.

Waziri Motegi pia amemwambia Rais Kikwete kuwa pia amekuja Tanzania kutoa taarifa kuwa Japan iko tayari kushiriki katika kuboresha na kuifanya ya kisasa zaidi Reli ya Kati kwa kujenga njia ya kimataifa badala ya njia nyembamba ya sasa. Amesema kuwa Japan itatuma wataalam wake kuangalia jinsi gani ya kuanza kazi hiyo ya uboreshaji wa Reli hiyo.

Aidha, Mheshimiwa Motegi ametangaza kuwa Japan itashiriki katika upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam kwa kuifanya ya kisasa zaidi.

Waziri Motegi amesema kuwa katika azma ya Japan ya kuifanya Tanzania nchi ya mfano katika Afrika katika uwekezaji na uchumi ulioimarisha, amekuja na kundi la wafanya biashara wa Japan ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Tanzania kuona jinsi gani wanavyoweza kusaidiana katika kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.

Waziri pia amesema kuwa moja ya malengo ya uamuzi huo wa Japan ni kuhakikisha kuwa bidhaa ambazo kwa sasa zinanunuliwa moja kwa moja kutoka Japan zitazalishwa hapa nchini katika viwanda ambavyo vitajengwa na makampuni ya Japan.

Kwa kuanzia amesema kuwa makampuni mawili ya Honda na Panasonic yamekubali kujenga viwanda nchini kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za Honda hapa hapa nchini na kingine kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya umeme.

“Huu ni mwanzo tu Mheshimiwa Rais kwa sababu kama nilivyosema kuwa tunataka Tanzania kuwa nchi mfano ya uwekezaji wa Japan katika eneo hili la dunia na namna hiyo kwa pamoja tutakuwa tumeshirikiana katika kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania,” Mheshimiwa Motegi amemwambia Rais Kikwete.

Waziri huyo pia amesema kuwa baadhi ya makampuni ya Japan yana mipango ya kuwekeza katika kilimo, na hasa kilimo cha pamba, na kuanzisha viwanda vya nguo hapa hapa nchini.

Wakati wa mazungumzo yao mjini Tokyo, Rais Kikwete alimtaka Waziri Mkuu Abe kuwekeza zaidi katika Afrika akisisitiza kuwa Japan ni moja ya mataifa makubwa duniani ambayo yamefanikiwa kupata soko kubwa katika Afrika na hasa soko la magari.

Uamuzi huo wa Japan na ziara ya Mheshimiwa Motegi inakuja wiki na miezi michache baada ya Tanzania kuwa imepokea viongozi wa mataifa mengi yakiwemo mataifa makubwa ya Marekani na China na inathibitisha ni kiasi gani siasa na sera za Tanzania zinavyokubalika duniani.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

10 Agosti, 2013


ichi kinogesho kina haja kweli?

Eti "Ni matokeo ya Ziara ya Rais Kikwete Japan". Sio uongo wa kisiasa huu? Nyie watu wa Ikulu msipende kudanganya-danganya watu kirahisi rahisi hivyo. Yaani Kikwete kaenda juzi tu hapa la leo-leo feasibility ya Honda ishakamilika, feasibility ya reli ya kati ishafanyika na maamuzi wajapani wanayafanya leo?

Kwani Mungesema ni Matokeo ya Economic Diplomacy imeanza tangu kipind cha Mkapa Mngeonekana wajinga? Jifunzeni kutuheshimu Watanzania tuna akili ya kuelewa mambo jamani. Punguzeni zarau. Eti
Ni matokeo ya Ziara ya Rais Kikwete Japan. My Foot!
 
inashangaza sana kuona kila jambo linalotokea watu wanalichukulia negetively, hivi swala hapa ni kikwete au maslahi kwa nchi, ni ulitaka rahisi asitafute wawekezaji, au bado mna mawazo ya nyerere kwamba tuache raslimali kwa kua haziozi, soo what? jaribuni kuwa positive angalau kidogo achani kuwaza giza kila wakati jaribuni kuiona nuru! kwa mtindo huu hamtakaa mzione fursa hata kama zitakua sebuleni kwenu! jipange acha kupiga mayowe..period!
 
Guys, personally siipendi CCM, lakini kama tutatuliza akili zetu na kuwa positive na kutumia fursa hizi vizuri bila ubinafsi na rushwa, Tanzania ya miaka mitano mpaka kumi ijayo itakuwa yenye maendeleo na uchumi imara. Kuna watu hawaelewi ni kwa nini 5 Asian tigers kama Korea Kusini, Malaysia na nyinginezo zimeweza kutoka kimaendeleo?? Waliweza kutumia fursa za technolojia na misaada ya kimifumo na uwekezaji katika elimu vilivyo. Kwa kifupi walijitambua wana nini na wanataka nini.

Kwa sasa kuna mwamko mkubwa sana wa kujitambua kwa wa Tanzania, tupo pazuri tunahitaji kubadili attitude za watanzania, wapende kufanya kazi, rushwa idhibitiwe, uzalendo pia uongezeke na hili si jukumu la serikali pekee ni sisi wote.

Mwisho nimalizie, HAKUNA JINSI NI LAZIMA TANZANIA IWE SUPER POWER AFRIKA MASHARIKI NA KATI BY 2025, dalili zote zinaonyesha hivyo. TUACHE KUJIDHARAU JAMANI CHONDE CHONDE.........
 
Hii thread imebeba ujumbe muhimu na mzito kwetu lakini kwa sababu haina chadema wala sheikh ponda ndani inaonekana ya hovyo

"MSUKULE ni mtu aliechukuliwa kwa nguvu za giza ili atumike kwenye shughuli zisizohitaji akili kama kulima shamba kwa faida ya mwenye Msukule. Chadema inawatumia vijana wasiojitambua kama misukule kwenda kufanya maandamano yasiyo halali na vurugu huku wao viongozi wamekaa majumbani kwao wakiwaangalia kwenye TV wanavyokula mkong'oto.

Kama kweli CHADEMA wanatetea haki kusingekuwa na ubaguzi wa matibabu ndani ya chama, wengine wanafanya checkup ujerumani wakati wengine wanalazwa third class muhimbili
.....JITAMBUE!"

Ukiwa msukule unawaona wenzio ndio misukule, huwezi kujitambua. Pole kaka.
 
wajapan ni wawekezaji wa kweli,huwa hawana longolongo,kwa upande wangu nina imani sana na wawekezaji wa kijapan
 
sasa nchi inauzwa kwa 10% mikataba mibovu, tunawatoa wanachi kwenye maeneo yao tunawapa wawekezaji, nchi yetu tunakuwa wakimbizi.
 
Hii thread imebeba ujumbe muhimu na mzito kwetu lakini kwa sababu haina chadema wala sheikh ponda ndani inaonekana ya hovyo

Umeona eee! Hii ni habari njema sana kwa uchumi na taifa ambayo tulitakiwa tujadili jinsi ya kushirikiana na hao wajapan bila kupunjwa! Hata vyombo vya habari vilitakiwa vifanye zaidi kwa kuchambua na kusaidia kuongeza uelewa wa jamii jinsi ambavyo tunaweza kuchangamkia fursa hizi. Wataishia copy/paste ya taarifa ya ikulu, na kutuambia tu kwamba Rais amesema tuchangamkie fursa! Swala muhimu la Tuzichangamkieje, hakuna atakaesema chochote!
 
hapo kwenye kujenga viwanda ndiyo penye magumashi , kurasini yote wamepewa wachina na waarabu badala ya ile propaganda ya upanuzi wa bandari ! Sasa bila shaka hawa watapewa kariakoo , maana hawataki kuwapeleka nje ya mji , ni kama vile nchi hii mwisho wake DSM .
 
Tatizo hizo neema haziji bila ya ufisadi ndani yake!
 
nchi yetu ni shamba la bibi

Stuka acha kulalamika! Muda wa kulalamika lalamika na kushutumu wakoloni umepitwa! Changamka kuza uchumi wako mwenyewe. Kwenye ujamaa tulitoka tangu mwaka 1985, Tz ni nchi ya kibepari.
 
Back
Top Bottom