Hizi ulizotaja ni sifa nje ya hizo za Paskali, nguvu ya Polepole inatokana na madaraka ya rais. Kwakuwa rais anaweza kufanya chochote hata kilicho nje ya katiba ya ccm na nchi, hata Polepole anaweza kufanya hivyo hivyo, ili mradi iwe ni yale yanayomfurahisha rais.
Labda tukubaliane nguvu ni nguvu bila kujali ziko ndani ya utaratibu au nje ya utaratibu. Toka Polepole awe kwenye nafasi aliyo nayo, maamuzi ya shuruti yamekuwa makubwa kuliko ushawishi au kufuata utaratibu na sheria.
Kipindi hiki ccm imetoka kuwa chama cha siasa na kuwa chama dola zaidi. Katika mazingira hayo, yoyote hata aliye mdhaifu anaweza kuonekana ni imara, kama kipimo cha uimara ni kutumia shuruti.
Kwa sasa toka Polepole awe katika nafasi hiyo ndio tumeona siasa za kishenzi kabisa na uhayawani wa wazi. Na chaguzi zote kuanzia za marudio, mpaka huu wa serikali za mitaa, ccm imetangazwa washindi bila kushindana, na kwa kufanya ushenzi na ukatili wa wazi.
Katika mazingira hayo huweza kusema mtu ana nguvu zile ulizozitaja, kwani hayuko kwenye siasa za uhalisia, bali siasa za kiburi cha madaraka.