Japo anaonekana mtu wa kawaida tu ndani ya CCM, Humphrey Polepole sio mtu wa kawaida!, He is extra ordinary very powerful!

Japo anaonekana mtu wa kawaida tu ndani ya CCM, Humphrey Polepole sio mtu wa kawaida!, He is extra ordinary very powerful!

Wote wanaopaza sauti za juu sana za kuabudu na kusifu wapo very powerful ndani ya CCM na serekali ya awamu hii...

1. RCs - Bashite
2. Bunge - Supika, Musukuma, Kibajaji
3. Cabinet - prof Jalalani
4. Opposition - Lyatonga & Mama Tz
5. Tanpol - Mambosasa
6. Media - unawajua!
 
Kwanini ufanye lobbying?! naamini Rais tuliye naye anaona moja kwa moja. kitakacho kubeba ni uwezo wako wa kiutendaji

Lobbying awamu hii haina nafasi na ukibainika unafanya lobbying ili upate kuteuliwa/kupitishwa kugombea nafasi yoyote ujue umejimaliza mwenyewe.

Uwezo wako wa kiutendaji, uadilifu na uzalendo wa kweli vitakubeba.
 
Hakuna la maana na Humphrey anajua kuigiza vizuri kama mtu mwenye hekima ila ukweli hana nguvu ya kweli ya Mungu.

Na anatumia zaidi vya kienyeji na hana moral authority yoyote kama anavyojinasibu. Naye atakuwa katika anguko kama Magufuli, Bashite na wengine.
 
Uko sahihi kwa asilimia 200

Polepole ni strategist yaani anafahamu kupanga mikakati kitaalam.

Pili, Polepole ni coordinator mzuri tu anafahamu namna ya kuunganisha mpango, sera na mikakati.

Tatu, Polepole ni good communicator yaani anafahamu ni vipi azungumze na hadhira kulingana na aina ya hadhira hiyo.

Hivi vitu baadhi alikuwa navyo Nape Nnauye lakini akavurugwa kidogo kutokana na kukosa experience yaani uzoefu.

Naomba niishie hapo.
 
Kinachotafutwa ni mchongo wa PR hususan kipindi hiki cha uchaguzi, ila kama tunachelewa hivi, inabidi tupaze Sauti za kupraise tusikike.
 
Hizi ulizotaja ni sifa nje ya hizo za Paskali, nguvu ya Polepole inatokana na madaraka ya rais. Kwakuwa rais anaweza kufanya chochote hata kilicho nje ya katiba ya ccm na nchi, hata Polepole anaweza kufanya hivyo hivyo, ili mradi iwe ni yale yanayomfurahisha rais.

Labda tukubaliane nguvu ni nguvu bila kujali ziko ndani ya utaratibu au nje ya utaratibu. Toka Polepole awe kwenye nafasi aliyo nayo, maamuzi ya shuruti yamekuwa makubwa kuliko ushawishi au kufuata utaratibu na sheria.

Kipindi hiki ccm imetoka kuwa chama cha siasa na kuwa chama dola zaidi. Katika mazingira hayo, yoyote hata aliye mdhaifu anaweza kuonekana ni imara, kama kipimo cha uimara ni kutumia shuruti.

Kwa sasa toka Polepole awe katika nafasi hiyo ndio tumeona siasa za kishenzi kabisa na uhayawani wa wazi. Na chaguzi zote kuanzia za marudio, mpaka huu wa serikali za mitaa, ccm imetangazwa washindi bila kushindana, na kwa kufanya ushenzi na ukatili wa wazi.

Katika mazingira hayo huweza kusema mtu ana nguvu zile ulizozitaja, kwani hayuko kwenye siasa za uhalisia, bali siasa za kiburi cha madaraka.
 
Kama ingekuwa lobbying hazina nafasi, usingeweza kuona wabunge waliohama upinzani, kujiunga na CCM kisha kupewa nafasi automatically bila kupitia vigezo vya utendaji.

Huenda umeamishwa kuwa ni vigezo vya kweli, lakini lengo hasa ni kupata wabunge watakaobeba agenda ya Magufuli kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi.

Kama huna uwezo wa kuona kwa jicho la tatu, unaweza kuamini hivyo vigezo vinavyotangazwa ili kuhadaa umma, ila agenda ya nyuma ya pazia ni nyingine kabisa.
 
Either "He is ectra ordinary and very powerful" Or "He is extraordinarilly very powerful"

I thought you were a lawyer!
 
Back
Top Bottom