#COVID19 Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu

#COVID19 Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu

Mkuu una Maanisha Verification test ya covid au Vaccination?
Sababu Wenyewe watoa chanjo wemeweka Vipaumbele

wanaotakiwa Kuanza Kuchanjwa 50yrs kuendelea sasa Mtu ana 26yrs na anasafiri je inamuhusu?

Kumbuka Tangu zamani Lazima uwe na Covid test certificate ndio usafiri tangu zamani corona ilipoingia...sasa isijekuwa umechanganya Mkuu Pascal Mayalla
 
Update:
Naomba kuomba radhi kwa ile early version, iliyosema cheti cha chanjo ni lazima, sio cheti cha chanjo bali ni cheti cha kipimo cha Corona ndio lazima kabla ya kusafiri. Hivyo Chanjo bado ni hiyari ila ni muhimu sana.

P
 
Mkuu una Maanisha Verification test ya covid au Vaccination?
Sababu Wenyewe watoa chanjo wemeweka Vioaumbele wanaotakiwa Kuanza Kuchanjwa 50yrs kuendelea sasa Mtu ana 26yrs na anasafiri je inamuhusu?
Kumbuka Tangu zamani Lazima uwe na Covid test certificate ndio usafiri tangu zamani corona ilipoingia...sasa isijekuwa umechanganya Mkuu Pascal Mayalla
Mkuu ikigijo , its true mwanzo nilijichanganya
ni Verification test ya Covid na sio Vaccination. I ofer my apology.
P
 
Mkuu una Maanisha Verification test ya covid au Vaccination?
Sababu Wenyewe watoa chanjo wemeweka Vioaumbele wanaotakiwa Kuanza Kuchanjwa 50yrs kuendelea sasa Mtu ana 26yrs na anasafiri je inamuhusu?
Kumbuka Tangu zamani Lazima uwe na Covid test certificate ndio usafiri tangu zamani corona ilipoingia...sasa isijekuwa umechanganya Mkuu Pascal Mayalla
Mkuu ikigijo , its true mwanzo nilijichanganya
ni Verification test ya Covid na sio Vaccination.
P
 
Swali kama umechanja corona na unataka kusafiri unaonesha cheti cha chanjo na kupita au lazima uwe na kile cha kupima?

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Mbona umatuchanganya wewe Paskali issue ni kupima corona ili usafiri nje ya nchi au uchanje corona?suala la cheti cha corona linahusikaje na safari za nje ya nchi?tynaomba ufafanuzi
 
Mbona umatuchanganya wewe Paskali issue ni kupima corona ili usafiri nje ya nchi au uchanje corona?suala la cheti cha corona linahusikaje na safari za nje ya nchi?tynaomba ufafanuzi

Ameshaomba radhi na kurekebisha, kinachotakiwa ni cheti cha kuonyesha umepima na hauna maambukizi.
 
Hapo sawa nimekuelewa chanjo ni hiari jamani Mama kishasema tusitishane sana
 
UFAFANUZI

Hakuna sharti la chanjo ya Corona kwa wasafiri wanaokwenda nje ya nchi. Ni vema msafiri akauliza shirika la ndege analokwenda nalo pamoja na masharti ya nchi anayotembelea. Kwa zile nchi ambazo zinahitaji kipimo cha UVIKO-19 msafiri afanye kipimo hicho ndani ya masaa 24 hadi 48 kabla ya kuanza safari. Upimaji unafanyika kwa msafiri kufanya booking kupitia pimacovid.moh.go.tz ambapo atachagua kituo cha upimaji . Baada ya upimaji majibu yatatumwa kwake kwa njia ya barua pepe aliyotumia wakati wa booking. Akifika Airport cheti hicho kitahakikiwa katika dawati la afya. Unashauriwa kujiepusha na vyeti feki.

Kuhusu uzushi unaoenea kwamba Chanjo ya UVIKO-19 inatolewa mashuleni hiyo sio kweli,Chanjo zote zinatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoainishwa na Chanjo hiyo inatolewa kwa makundi Yale matatu yalivyotangazwa.

Watoto sio walengwa wa Chanjo hii na vilevile hakuna kituo kwenye shule.

Imetolewa na ;
Catherine Sungura
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Afya
8/8/2021
 
Daaah yaani sijaelewa kbs,kwamba hao waliolia na kusaga meno hawajui kuwa wanatakiwa kwenda na cheti cha corona airport kinachoonyesha uko negative?
Asante kwa ushauri khs chanjo but khs corona test hiyo inajulikana,husafiri bila cheti cha corona cha negative results,hao wasafiri inamaana hata hiyo airline waliokata ticket hawakuwaambia?mbn mambo yako wazi na kila airline au nchi unayoenda inakua na masharti khs corona unayotakiwa kuyajua kabla ya kuanza safari.
 
Gwajima leo kaeleza vizuri sana akihubiri kanisani kasema hivi kama wao wanatuzuia kuwa hatutakiwi usafiri kwenda kwao kama hatujachanja na sisi tuwagomee wao kuja kwetu
 
Kuna tofauti kati ya kipimo cha corona (PCR)
Na Kipimo cha "Rapid Test" na chanjo Ya corona (JJ,Pfizer etc)

Na kila nchi ina masharti yake.

Kuna nchi zingine watahitaji PCR,wengine Rapid Test tu,wengine watataka Cheti cha Vaccination.
 
UPDATE 2.
Kufuatia upotoshaji uliotokana na thread hii, pale mwanzo kabla haijarekebishwa, mimi Pascal Mayalla naomba kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na taarifa ya awali ambayo haikuwa sahihi, sio sahihi. Naahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa serikali yetu kupitia Wizara ya Afya, na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu sahihi ya chanjo ya Corona.

Kunapotokea kosa lolote, katika jambo lolote, kitu muhimu sio tuu kuangalia kosa lililotendeka, (actus reus), bali nia ya mtenda kosa, kama alikuwa na nia ya kutenda kosa (mens rea)

Na mwisho naomba kusisitiza kuwa japo kwa sasa chanjo ya Corona ni hiari, kitu kinachohitajika kabla ya kusafiri nje ni cheti cha kupima Corona, na sio cheti cha chanjo. Lakini huko tuendako tutafikia mahali cheti cha chanjo ya Corona kitahitajika kabla ya kupata Visa za kuingia nchi fulani fulani, hivyo nitafika muda chanjo ya Corona itakuwa ni hiari ya lazima.

Pasco Mayalla
 
Back
Top Bottom