UPDATE 2.
Kufuatia upotoshaji uliotokana na thread hii, pale mwanzo kabla haijarekebishwa, mimi Pascal Mayalla naomba kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na taarifa ya awali ambayo haikuwa sahihi, sio sahihi. Naahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa serikali yetu kupitia Wizara ya Afya, na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu sahihi ya chanjo ya Corona.
Kunapotokea kosa lolote, katika jambo lolote, kitu muhimu sio tuu kuangalia kosa lililotendeka, (actus reus), bali nia ya mtenda kosa, kama alikuwa na nia ya kutenda kosa (mens rea)
Na mwisho naomba kusisitiza kuwa japo kwa sasa chanjo ya Corona ni hiari, kitu kinachohitajika kabla ya kusafiri nje ni cheti cha kupima Corona, na sio cheti cha chanjo. Lakini huko tuendako tutafikia mahali cheti cha chanjo ya Corona kitahitajika kabla ya kupata Visa za kuingia nchi fulani fulani, hivyo nitafika muda chanjo ya Corona itakuwa ni hiari ya lazima.
Pasco Mayalla