Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?


Kwanza mimi sijasoma theology. Nasoma biblia kujifunza tu.

Documentary Hypothesis
nimeiosoma ila ni mawazo ya wanadamu tu hasa wanatheology wanaotumia hekima za kibidamu yenye kikomo, ndio maana kuna mambo mengi watu wameyatambua mpaka kwenye ujio wa Yesu alipokuja. D hypothesis kama ni kwel basi biblia yote haina maana ni story za kusadikika.

Ukiangalia matukio ya Mwanzo 12;12-20, 20:1-8, 26:6-10 ni tofauti kabisa japo yanafanani. Ila ni Mungu ndio aliyefanya kwasabab hawezi kuchanganya uzao wake na wanadamu ndio maana kila wakati alikua anazui hichi kitu. Soma Mwanzo 6.

Twende kwenye maswali yako.

Beersheba inaanza kuonekana kwenye Mwanzo 21:14 kuwa palikua na jangwa la Beersheba Ibrahimu na Ismael walipita tu kwenye jangwa hili. Mwanzo 21: 21 inaonesha Ibrahimu na Ismael alilipita jangwa la Beersheba akenda mpaka jangwa la parani ambapo Ismael aliishi parani.

Kwaio hapa tuna miji mitatu Hebron, Beersheba na parani utasoma hizi sehem tatu vizur.

Mwanzo 21;22 Abimeleki baada ya kuona Ibrahimu amemsogelea kwa kuogopa yaliomtokea miaka ya nyuma kwenye Mwanzo 20. Ndio maan alikuja kutafta mapatano na Ibrahimu. Ibrahimu alikua anashuka kusini kwasabb ya njaa kali na kusini palikua kuna hauweni ya malisho kwa ajiri ya mifugo yake. Mwanzo 26:1.

Mwanzo 22:19 baada ya jaribu la kumtoa isaka kafara. Ibrahimu alirudi mpaka Beersheba, inaonesha makazi ya Ibrahimu na Isaka ilikua ni Beersheba kama Mwanzo 21:34. Inayosema Ibrahim alikaa na wafilisti miaka mingi kabla ya jaribu la kumtoa kafara Isaka.

Hata ukisoma Mwanzo 28:10 na Mwanzo 46:5 yote yanaonesha Beersheba waliishi Ibrahimu na Isaka. Maana ibrahim, isaka na yakobo wote waliishi hapo kama Mungu anavyojitambulisha.

Hapa nakujibu swali la umri wa isaka wakati wa kutolewa kafara hakuwa mchanga. Kama unabisa lete ushaidi wa maandiko. Kama utatumia Qur'an pia itakua vizur
 
Safi sana Kuna wengi elimu hii hawana
 
Agano lilifungwa Kipindi Ambacho Isaka hajazaliwa sasa sjui unazungumzia Agano lipi..
Na agano lilikuwa ni Kutahiriwa na Ishmael alitahiriwa ndani ya Agano
Wakati Mungu anmtembelea Ibrahim kwenye mialo ya Mamre alikua tayari ana Ismael lakini alimwambiaje Sara? Utakua mama wa mataifa. Hakuambiwa Hajiri Mmisri wala uzao wake. Pia angalia singularity ya neno mzao na sio wazao. Unatrace uzao kwenye ndoa na ndio maana hata Leo mtoto wa ndoa anatambulika mpaka na mamlaka.
Alitahiriwa maana maagizo yalikua ni watu wote wa nyumbani kwake. Pia kama amemrithi baba yake kwa nini mama amtafutie mke? Kwa Nini mama ndo angolee mahari ya mwanae na baba alikua hai? Mbona Isaka Mzee alimtafutia mke? Unajua Kwa Nini hakumchukulia mke huko Kanaani alikoishi Hali ya ugeni?
 

Tena kwenye Quran waebrania waliotajwa ni ,
Tera(Azar) babaye Ibrahim , Sarah, Isaka, Ishmael, Yakub
 
Kitu muhimu ni tuutafute ukweli, Mungu hakuleta dini wale Yesu hakuleta dini!. Hoja hapa ni nani mkweli na nani muongo?. Mtoto aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni nani?.
P
Kila mtu alete mistari
Kwenye Biblia mambo yote yako bayana
Full story a to z

Kwenye Quran kuna utata kidogo

Ila yote kwa yote aliyetolewa sadaka ni Isaka kwa kuwa, Ishmael muda huo alishaondoka na Mama yake kwenda Mecca hadi kupata kiu na chemchem ya maji ya Zamzam kupatikana
 

Sarah kumpa Ibrahim Hajiri amfanye mkewe haibadili status ya Hajiri kuwa ni mke wa Ibrahim

Ndoa ni suala la kisheria na kimila. Sarah hana mamlaka wala uwezo wa kumuozesha Mwanamke yeyote kwa Ibrahim ilhali yeye ni Mke.

Huko mbeleni tunaona Ibrahim akimwambia Sarah kuwa huyo Hajiri ni kijakazi wake(wa Sarah) hivyo yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuamua uwepo au kutokuwepo kwa huyo kijakazi.

Pili, ishu ya wake za Yakobo ni walewale wawili. Recho na Leah. Hao vijakazi hawahesabiki kama wake Yakobo.

Watoto wa kina Bilha na zilpa walihesabika kwa sababu walikubali mfumo wa familia ha Yakobo. Hawakuwa wasumbufu kwa Mabosi zao.
 
Mtoto wa pekee alikuwa Isaka

Ishmael alishaondoka kwenda Mecca na mama yake Hajar hadi akapata shida jangwani Mungu akampa chakula na chemchem ya Zamzam ndo hadi leo wakienda Hijja ipo
 
Kamba hii
Ibrahim hakwenda nao (Hajir&Isma) Mecca

Alibaki na mkewe na Isaka
 
Nini kilimfanya Hajiri&Ismail kuondoka kwenda Mecca hadi kupata kiu na Mungu kuwapa chemchem ya maji ya Zamzam?
 
Quran haijataja hata jina

Biblia ndo full story kama video vile
 
Habari zote za Ishimaili na Isaka zimeelezwa kikamilifu katika Biblia, na ndio rejea kuu na pekee. Hizo habari haziko popote kwenye Quran.
Na bila ubishi wowote iliyetakiwa kutolewa sadaka ni Isaka.

Waislamu wanaaminishwa uzushi wa Ishimaili kutakiwa kutolewa sadaka pasipo rejea ya Quran.

Tuache kuisingizia Quran mambo ya uzushi na uongo.
 
Mkuu,..umri ni kigezo na ni njia rahisi zaidi ya kujua ukweli ni upi,...

Kwa mfano,..kama ikiwa tunaona kwenye Biblia kwamba wakati amri ya kuchinjwa inatoka.......mtoto aliyekusudiwa kuchinjwa tayari kwenye wakati husika alikua anaweza kuongea na kutembea umbali mrefu......

Inabidi tujiulize, Je, kati ya Ismail na Isihaka nani alikua kwenye umri wa kuweza kuongea na kutembea umbali wa zaidi ya km 300,. kwenye wakati huo?


Tukisema tupuuzie suala la umri,.. nadhani itakua tumeamua kwa maksudi kabisa kuukimbia ukweli.
 

Ndio maana nikakuambia Baada ya kuzaliwa Isaka Ibrahim ameishi miaka 70 mbele.
Akatafuta hadi mke
 
Kujadili hii mada inabidi tutambue mambo makuu mawili.
1. Rejea ya habari hizi zipo kwa kina na kikamilifu ndani ya Biblia pekee yako. Hazipo kwenye Quran
2. Biblia inamtaja Isaka kama ndiye mtoto wa ahadi, mtoto wa pekee wa ndoa ya Ibrahimu na Sarah na Isaka ndiye aliyepelekwa kutolewa sadaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…