Prince Juzo
Member
- Feb 4, 2018
- 56
- 73
We Unahisi kwenye Hadithi Ya abimeleki Ilistahili kuwepo Hapo??
Mwanzo 21:22-34??
Mwanzo kabisa Nilizungumza Kitu kinaitwa Documentary Hypothesis au JEPD theory kama Umesoma Theology utanielewa Nachokisema..
Kama utaweza nenda Kapitie maana yake na usome pia kuhusu Mahusiano yake na Mpangilio wa Matukio kwenye Biblia Agano la kale Especially Torati..
Ngoja nichokoze kidogo Kitu kabla sijakujibu
Unafahamu kuhusu Beersheba na kuhusu kupewa Jina la beersheba unahisi Nani ana Authentification ya Hilo jina?
Ni Ibrahimu:-
Kama mwanzo 21:31
"Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili."
Au ni Isaka:-
Mwanzo 26:33
"Naye akakiita jina lake BeerShiba; kwa hiyo jina la mji huo likawa Beer-sheba, hata leo."
umewahi kusikia Story ya Abimeleki na Ibrahimu na Sara (Soma Kwenye mwanzo 20:1-18)?
Vipi inatofauti Gani na Story ya Farao na Ibrahimu na Sara ( Soma mwanzo 12:12-20)?
Sasa Tuache hao Inatofauti Gani kati ya Story hizo na Story ya Rebeca Na isaka ?(soma mwanzo 26:6-10)
Kuna Kitu Umegundua Kwenye Hizo hadithi?
sasa Nakushauri Soma Documentary hypothesis au JEPD theory tena siku hizi hakuna haja Uende kozi ya Theology uyajue haya..
Sasa Turudi kwenye Concern yako...
Eneo Ambalo Linatajwa Ni Eneo ambalo Ibrahamu alikuwa akiwa na Umri wa Miaka 100 na Ndyo muendelezo wa Hiyo mwanzo 22 ukitoa story ya Abimelek ambayo ukiisoma Utaona Ibrahim anatoka kanaani Kwenda moria..
Wakati huko nyuma tunaambiwa alikuwa anakaa nchi ya wafilisti Beersheba..
So story ya 21 na Story ya 22 Haziungani..
Ila zinaungana na Story ya Mwanzo 21:21..
Kwa hiyo story ya mwanzo 21:21 muendelezo wake ni mwanzo 22:1..
Ukijifunze Textual analysis Utagundua story ya Abimelek ni added Story muulize Mchungaji yoyote au Mtu yoyote aliyesoma Theology na aliwahi kusoma Course ya textual Critic au Textual analysis
Kwanza mimi sijasoma theology. Nasoma biblia kujifunza tu.
Documentary Hypothesis
nimeiosoma ila ni mawazo ya wanadamu tu hasa wanatheology wanaotumia hekima za kibidamu yenye kikomo, ndio maana kuna mambo mengi watu wameyatambua mpaka kwenye ujio wa Yesu alipokuja. D hypothesis kama ni kwel basi biblia yote haina maana ni story za kusadikika.
Ukiangalia matukio ya Mwanzo 12;12-20, 20:1-8, 26:6-10 ni tofauti kabisa japo yanafanani. Ila ni Mungu ndio aliyefanya kwasabab hawezi kuchanganya uzao wake na wanadamu ndio maana kila wakati alikua anazui hichi kitu. Soma Mwanzo 6.
Twende kwenye maswali yako.
Beersheba inaanza kuonekana kwenye Mwanzo 21:14 kuwa palikua na jangwa la Beersheba Ibrahimu na Ismael walipita tu kwenye jangwa hili. Mwanzo 21: 21 inaonesha Ibrahimu na Ismael alilipita jangwa la Beersheba akenda mpaka jangwa la parani ambapo Ismael aliishi parani.
Kwaio hapa tuna miji mitatu Hebron, Beersheba na parani utasoma hizi sehem tatu vizur.
Mwanzo 21;22 Abimeleki baada ya kuona Ibrahimu amemsogelea kwa kuogopa yaliomtokea miaka ya nyuma kwenye Mwanzo 20. Ndio maan alikuja kutafta mapatano na Ibrahimu. Ibrahimu alikua anashuka kusini kwasabb ya njaa kali na kusini palikua kuna hauweni ya malisho kwa ajiri ya mifugo yake. Mwanzo 26:1.
Mwanzo 22:19 baada ya jaribu la kumtoa isaka kafara. Ibrahimu alirudi mpaka Beersheba, inaonesha makazi ya Ibrahimu na Isaka ilikua ni Beersheba kama Mwanzo 21:34. Inayosema Ibrahim alikaa na wafilisti miaka mingi kabla ya jaribu la kumtoa kafara Isaka.
Hata ukisoma Mwanzo 28:10 na Mwanzo 46:5 yote yanaonesha Beersheba waliishi Ibrahimu na Isaka. Maana ibrahim, isaka na yakobo wote waliishi hapo kama Mungu anavyojitambulisha.
Hapa nakujibu swali la umri wa isaka wakati wa kutolewa kafara hakuwa mchanga. Kama unabisa lete ushaidi wa maandiko. Kama utatumia Qur'an pia itakua vizur