monomotapa
JF-Expert Member
- Oct 30, 2012
- 437
- 325
Tatizo tulilonalo wengi Tanzania watu wanamuona Lisu katika muonekano wa siasa zaidi, Kama vile yeye anaishi muda wote ndani ya siasa na uana sheria basi, wanasahau kuwa yeye kama binadamu wengine anaishi pia maisha mengine ya kawaida nje ya uana siasa na uana sheria, ana watu wanaompenda, wanaomchukia, kuna watu ameshakwaruzana nao nje na ndani ya siasa. Jaribu kujitathmini wewe binafsi kwenye maisha yako unakumbana na mambo gani na mangapi, Je yote yanatokana na kazi unayofanya?......Unavamiwa na vibaka ukitoka kazini utasema bosi wako kazini anahusika kisa mlikwaruzana kazini! Tanzania kuna watu bado wajinga sana wanaishi kwa kuhisihisi tu, ndio maana ushirikina upo juu sana nchi hii watu wanaishi kwa hisia hisia kuliko kisayansi ..Tuna safari ndefu sana sana kielimu na kisayansi....