ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 16,871
- 39,881
Manager na msimamizi wa mchezaji Clement Mzize amesema kuwa Yanga wana roho mbaya hawataki kumwachia Mzize akatafute malisho mzuri mahala pengine.
Amehoji kuwa club ya Al Masry ilikuja na dollar 600k Yanga wakagoma kuwa wanahitaji dollar 1m, akaendelea kusema kuwa Yanga kama walimuuza Mayele Kwa dollar 500k, kwanini wapate kigugumizi Kwa Mzizi
Amesema Mzize alikuwa akilipwa million 2 ila Kwa mkataba mpya analipwa milion 15 na kuwa Yanga wanamnyonya kijana
Amesema Yanga haina mchango wowote Kwa Mzize maana walikuwa washamfukuza under 20 na yeye Jasmine alishawishiwa na wazazi wake pamoja na coach Zahera kumsimamia
"Niseme tu Yanga wana roho mbaya hawataki kumwachia Mchezaji, Al Masry wamekuja na ofa ila Yanga wamegoma wanataka dola Million moja kumwachia wakati Mayele tu aliondoka kwa dola 500,000 niseme tu Yanga wana roho mbaya na hawataki kumwachia wao wana hela hivyo wana kiburi, walikuwa wanamlipa Million mbili ila ndio mwaka huu wamemlipa Million 15 ila hawataki akachukue zaidi, naiomba Serikali watazame sana usimamizi wa mpira, wengi wanadidimiza na kuwaonea Wachezaji kisa hali duni"
"Nimemchukua Clement Mzize wakati hana timu, Yanga walishamruhusu aondoke pale Under 20 ila Baba yake Mlezi pamoja na Kocha Zahera walikuja kuniomba sana nimchukue kumsimamia, hawajui namna gani Kijana ameteseka kufika alipo hapo, anategemewa na familia na yeye ndio kila kitu kwao, unadhani Yanga wamewekeza kiasi gani mpaka Mzize kufika hapo? Nafasi ya kuvunja Mkataba ipo ila kwasasa sitaki kumsumbua Kijana, acha alitumikie Taifa kwanza"