shida yako ni kasi ya kumiliki ama uhalali wa umiliki?Inaonekana umeathiriwa na snail-pace attitude ya Kitanzania,ile ya mtanzania kununua kiwanja then anakaa miaka kumi ndio anaweka msingi.Waganda wanafanya kazi na wame-embrace ujasiriamali kwa moyo wa ujasiri na bidii.
mwaka fulani tuliletewa net group solution hapa bongo,ikawa maarufu hata kupewa Tanesco,ikaleta shida,tulipoenda South Africa walikotoka tukaujua ukweli kwamba kampuni ni ya mbongo mwenzetu na hata haikuwa kampuni yenye hadhi kubwa huko kiasi cha kumilikishwa Tanesco.Siku nyingine tukaletewa Dowans hapa,tukaambiwa wamarekani wale ni noma kwenye nishati,ikaleta shida,tukaenda marekani,cyprus na kwingineko,tukakutana na wabongo wenzetu again,sasa mie nauliza swali,huyo JB anaekuja juu kwa kasi hivyo,na anasema yuko karibu na familia ya kwanza,je,huko kwao Uganda ni maarufu pia?je,alikuwa nazo tangu akiwa kwao au kazipatia hapa bongo?
Ana hotel hata pale jengo la NSSF Jijini Mwanza niliwahi kupita siku moja nikaona jina la hiyo hotelil na magari aina ya NOAH kwa ajili ya wateja wa hotelini yamepaki nje ya hoteli.kama ni hivyo mhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!
Mzee Mwanakijiji,
Mr Justus Baguma, a Ugandan entrepreneur in Tanzania, owns the JB Belmont, Savannah and some shops at Quality Centre and has also been elected the chairman of the Ugandan Community in Tanzania.
He is a self-proclaimed self made man and attributes his success to hard work... Whether "hard work" means "trouble for Tanzania" I don't know....
Kagame and Museveni...have they planted people in our system as done in Congo DRC? What is it? Tutsi dominance or plans to rule East Africa?
nimewahi kukaa karibu na nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja mtz mwenye asili ya asia ambaye leo hii ana wadhifa mkubwa ktk chama tawala huko mikoani.tulizoeana sana na watoto wake.ilikuwa ni kawaida kwangu kumkuta M7 ndani ya nyumba hiyo hapa dar na alikuja mara kwa mara bila kutangazwa radio wala popote wala hakuna cha msafara wa rais wala nini.narudia tena,M7 hakuwa anakaa ikulu wala hakuwa na msafara.alikuwa akija specific kwa mahusiano yake ya kibiashara na huyo bwana.nyumba iliwekewa walinzi na FFU wakati akiwepo.dunia ina mambo hii...tena mengi...nijisongee nguna yangu nile miee..!na maswali sitaki!
Nimepita mwaka jana,uongo wangu uko wapi?Huwezi kulinganisha upande wa Tanzania na ule wa Uganda.Upande wa Uganda pamoja na kwamba kwa kipindi kirefu ulikuwa hauna umeme lakini bado maduka,hoteli,migahawa na hata benki viliendelea kujengwa.Miaka kumi ya wapi ?Kama private commercial bank inaweza kufungua tawi lake upande wa Uganda wakati the same bank imeona haina haja kufungua tawi hata Bukoba mjini,yaani bado tu hupati picha ya tofauti kwenye suala la kimaendeleo...
Si mpaka wa Mtukula tu,jaribu kwenda Sirari au Namanga ujionee tofauti ya uchangamfu kibiashara katika upande wetu na upande wa majirani zetu...Unapoona benki upande wa mwenzako halafu kwako hakuna sijui unapata picha gani kibiashara?Au unao ni uongo?
kumiliki siyo tatizo. Anamiliki kwa namna gani ndiyo la kujadili
Belmont...acha huyo tu, kuna waganda, makongo kibao wanaofanya kazi ya utapeli tu kwenye sekta ya madini..wanajiita generals, kanali, waasi kutoka kongo..kumbe matapeli wakubwa..mwaka jana walitutapeli fedha nyingi tu, wakakimbia zao kongo..lakini kibaya zaidi hawa jamaa huwa wakishatapeli hugawa fungu kwa polisi..ili wsikamatwe..wameharibu kabisa sekta yetu ya madini...na njia yao kubwa wanayotumia..ilikuishi hapa ni kuoa mabinti wa kitanzania na kuzaa nao ili kuhalalisha uwepo wao hapa nchini..nashangazwa na kusikitishwa sana na hali kama hii
Who told you najidharau?Najiamini naweza kupambana na mganda au mkenya na ndio maana nimekuwa nikiunga mkono na kuitetea hoja ya sisi kupambana katika jumuiya ya Afrika nasi kuonesha woga na kujidharau kwa kuikimbia.kamwe sitakubaliana na this kind of ---- ya kudiscuss maisha ya mtu,after all small minds discuss people...great minds discuss ideas.Sioni hoja yoyote ya sisi kuanza kumponda JB as long as he has not broken any law.acha kujidharau..hakuna uTanzania, u-ganda ama uMarekani kwenye ishu ya kutengeneza pesa...kinachojalisha ni juhudi yako na commitment na kuomba Mungu..mbona sisi tunao watu wa kujivunia tu ambao wamekua na bado wanaendelea kukua kwa kasi??,.Said Salim Bakhresa mfano??acha fikra za kitumwa...we are born equal...we fall at our own discretions!!!
Hicho chuo kimejaa watumishi hasa wahadhiri waganda ambao professional qualification zao ni questionable.
Sielewi TCU waliwezaje kuwapa ithibati ya kufanya kazi ya kutoa elimu kwa kiwango cha degree bila kuangalia viwango vya elimu vya wahadhiri.
Pia kuna taarifa za wafanyakazi wazawa kubaguliwa na kunyanyaswa na hao waganda wa KIU.