Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #161
Kuna watu wako slow tu; tunapenda kuangalia vitu kimoja kimoja badala ya kujumlisha picha nzima. Ni sawasawa na puzzle...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona kuna wahindi wengi wa Kenya wapo Tanzania wanafanya biashara kubwa kuliko za JB hamuhoji uhalali wa biashara zao?
Wale waganda wa Kinondoni pia walikuwa wafanya biashara mazee, tusiwe wavivu wa kufikiri
Waganda waliotuhumiwa kuua askari, mbwa waachiwa
Posted on March 10, 2008 by admin
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya watano Raia wa Uganda waliokuwa wakituhumiwa kuua askari watatu pamoja na mbwa.
Mahakama iliwaachia huru raia hao wa Uganda mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Thomas Mihayo baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwasilisha nolle akiiomba mahakama kuwaachia huru kutokana na kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaki.
Kwa mujibu wa nolle iliyowasilishwa mahakamani hapo, iliwataja washitakiwa ambao DPP hana nia ya kuendelea kuwashitaki, ambao ni
Bw. Mawanda Maalo, Bw. Hawalulema Venist, Bw. Sylvester Salugo na Bw. Mohamed Simbwa Mohamed.
Uamuzi wa DPP wa kuwafutia washitakiwa wanne pia uliambatana na uamuzi wa kuendelea kumshitaki mshitakiwa mmoja ambaye pia ni raia wa Uganda Bw. Abdul Karim Msanje, ambaye atakabiliwa na mashitaka hayo ya mauaji.
Mshitakiwa huyo anatumikia kifungo cha miaka 15 jela kufuatia makosa ya kupatikana na silaha pamoja na risasi ambapo alikamatwa na bunduki mbili aina ya SMG AK 47 zenye namba 1975-230912 na 56-3903138 pamoja na risasi 87 ambazo zinadaiwa kutumika kwenye mauaji ya hao askari na mbwa.
Watuhumiwa hao walidaiwa kuwaua askari namba D.1672 Koplo Hassan, E.7324 D/C Ramadhani na E.7999 D/C Deogratius mnamo Mei 25, 2003 huko Kawe, Dar es Salaam.
Mbali na kuua maaskari hao pia walidaiwa kuua mbwa wa polisi, Rogger ambao walikuwa wanatumika katika doria ya siku hiyo.
Ilidaiwa kuwa, majambazi hao walianza kuwafyatulia risasi polisi wakati dereva anataka kuondoa gari hivyo kupoteza mwelekeo na kuacha barabara na kupindukia mtaroni, wakati huo huo majambazi wakiendelea kufyatua risasi.
Mapolisi watatu walikufa papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya ambapo Siku chache baadaye waliwakamatwa Waganda hao kwa tuhuma za mauaji hayo.
Polisi pia walimpiga risasi raia mwingine wa Uganda, Bw. Emmanuel Lugema, ambaye alikuwa akituhumiwa kuwa ni miongoni mwa wavamizi waliokuwa wakijaribu kukimbia.
Source: Majira
Ujinga kama huu wako ndio janga halisi la kitaifa-watu kupenda uzushi au ku-conclude mambo bila hoja au ushahidi wowote!JB(ingawa simjui) ni janga la taifa kivipi?Halipi kodi?Yeye ndie anayefanya sisi tusifanye kazi na kuishia kuimba nyimbo za ufisadi na freemason?Kuna mtanzania amezuiliwa kufanya biashara Uganda?Tatizo letu ni elimu ya kukariri na kujibu mitihani ya darasani tu.Huu ndio utandawazi uliokariri darasani,watu wanazunguka dunia nzima kutafuta business opportunities.Acha JB afanye kazi huku sisi tukiendeleza porojo zetu za kuogopa kujiunga na EAC kwa sababu ya uvivu wetu.Unamwita JB malaya na kusahau kuwa kama ni umalaya si anaufanya na Watanzania wenzetu,kwa nini tusiwalaume hao watanzania wenzetu,let's deal with our own failures first.
Kuna watu wako slow tu; tunapenda kuangalia vitu kimoja kimoja badala ya kujumlisha picha nzima. Ni sawasawa na puzzle...
Kwa kiasi kikubwa inaonekana watu wanamjua kile kilichowekwa mbele yao. Kitu pekee ambacho naona kimekosekana sana ni kushindwa kuhusisha influx pia ya baadhi ya waganda ambao wameamua kubadilisha majina... ili kufanya biashara fulani fulani.
Kumbe marafiki wa JB wanajulikana,lol! Actions speak louder than words....
:yawn::yawn::yawn:Ngoja nikatafute ugali kwa mama kanjinji wa mtaa wa gerezani.Wewe si ndio mwenye ile sifa humu JF "Ufataani".
Ulisema sana humu kuhusu Richmond na Dowans ilipogeuzwa na kuwa Symbion ukakaa kimya na kuufyata, kwanini?
Hotel za East Africa Arusha ni za PPF. Hawa wasomali wanaendesha tu - management lakini majengo ni ya PPF.
Barre.
Lonestriker Mbona umetoka sana povu kwenye hii thread ndugu? What are you not telling us about this JB?
Udom ujenzi unaisha 2015. KIU NI KAMA BAFU TU.
Well said mkuu. Tumekuwa watu wa kufuatilia issue za watu (si vibaya kama kuna mashaka) na kila tunapoona wamefanikiwa harakaharaka tunawaza ni mafisadi. Ni afadhali mtu anayekuja na jina la JB humu jamvini aje na ushahidi unaoonesha uwalakini kwenye mali anazomiliki. Lakini kama ni kuumizwa na utajiri wake tu itakuwa haina maana yoyote.
Hii spirit ya kushindwa kuthubutu ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Leo hii Kenya Commercial Bank (KCB) ina matawi lukuki hapa kwetu lakini benki zetu kama za NMB, CRDB na NBC zimebaki zikiimba wimbo wa 'simbanking' na Mobile Branches humuhumu ndani. Hivi tumeshindwa kweli kupenetrate kwenye masoko ya EAC hadi kuanza kuoneana vijicho?
Hawa matajiri wetu (ambao wengi wao utajiri ni matokeo ya kufisadi fedha za umma badala ya kutumia njia halali kutajirika) wameshindwa kweli kutumia mapesa yao hayo walau kuwekeza kwenye ukanda huu wa EAC?
Ni bahati mbaya kwamba, Wabongo tumekuwa kama malimbukeni mtu anachuma mamilioni ya fedha badala ya kuwekeza wengi wanakuwa wa kuzunguka kwenye makasino, uzinzi wa kupindukia na anasa za kutisha. Kwa kuwa fedha zinatokana na uharamia + Ufisadi, uchungu unakuwa hakuna. Tunapaswa kubadilika mind set zetu.
kutokwa povu ndio nini?Sorry dude,not all of us entertain misemo isiyo na maana,I mean sio wote tulikulia vichochoroni.Simjui JB na wala sikuwahi kumsikia kabla lakini bahati nzuri nimefika mpakani mwa Tanzania na Uganda na kujionea tofauti ya wafanyakazi na sisi watu wa porojo.kwa mtu yeyote aliyefika mpaka wa Mutukula atakuambia tofauti ya kimaendeleo iliyopo katika upande wa kwetu na ule wa wenzetu wa Uganda.Binafsi roho iliniuma sana pale Mtanzania mwenzangu aliponiomba hela ya Uganda badala ya kitanzania tena katika ardhi ya Tanzania anapofanyia biashara yake ya mgahawa,do you know why?Ni kwamba vitu vingi wananunua sehemu ya Uganda kwa sababu Sehemu ya Tanzania hamna kitu,ni vibanda viwili vitatu tu.Huu ndio ujinga wetu unao nitoa povu.Na hali kama hii inajirudia katika mipaka yetu mingine.Tumelala then wakija wageni wachapakazi tunaanza kuropoka bila sababu za msingi.
What is your point?Yaani maelezo yawe mazuri lakini hayatakiwi...logic iko wapi?Umenikumbusha wale wabunge wetu ambao kila mwaka wanatoa kasoro mia na kuishia kuunga hoja.Mpaka sasa hakuna mtu aliyekuja na fact yoyote au hoja yoyote inayoonesha kuwa JB ni janga la taifa.So far watu wanaleta porojo zisizo na connection yoyote na ' JB kuwa janga la taifa'.maelezo yako ni mazuri lakini hapa si sehemu sahihi,rudia kusoma swali hapo juu..