Je, Afande Sirro ana chuki binafsi na Tundu Lissu? Kwanini atoe kauli kama hizi dhidi yake?

Je, Afande Sirro ana chuki binafsi na Tundu Lissu? Kwanini atoe kauli kama hizi dhidi yake?

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Katika Mkutano wa Tume ya Uchaguzi, Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, na Jeshi la Polisi, IGP ametumia muda mrefu kumshambulia Tundu Lissu na CHADEMA.

Hali hiyo ilisababisha mpaka Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, Benson Kigaila, kuingilia kati ya kumtaka Mwenyekiti wa Tume, Jaji Kaijage, umuelekeze IGP Sirro kutokuishambulia CHADEMA.

IGP alitoa kauli mbalimbali za chuki na vitisho, lakini mbaya kuliko zote ni pale alipotamka, "KAMA UNATAKA KUFA, SUMU SI ZIPO."

IGP anafanya kazi yake, anakemea lugha zinazochochea uvunjifu wa amani
Sasa kama mtu hajajiandaa kushinda ila anaanza kuhamasisha watu kuingia barabarani ndio nini
Ni lugha ipo inayo chochea uvunjifu wa amani, mtu akikuambia kuwa Safari hii mkiiba kura hapatatosha kwako hiyo Ni lugha ya kichochezi kweli ? Mbona anapo sema kuwa Kama atashindwa kiuhalali atakubali matokeo mbona kwa Hilo hamliungi mkono ?.
 
Ninachoona ni kuwa wanajiandaa kwa matukio baada ya matokeo kutoka kufuatia kauli ya Lissu kuwa akishindwa kwa kuonewa anaingiza watu barabarani.

Swali ni je wanajua matokeo yatakuaje?
Hivi huyo mwenye kutaka kuingiza watu Barabara kawafanya wa Tz mabwege, eti waingie barabarani kisa yeye kakosa fursa au nafasi ya Urahisi
 
Kila mtu anayefanya kazi yake.. munataka awataje hao viongozi wasio na sifa.. kama vile IGP ni wa Chadema.. kama vile Lissu ni mfalme.. huku ni mwananchi tu sasa na baada ya uchaguzi..

Mupunguze.. kutunga tunga kisa.. munajuwa hana sera za kuvutia.. watanzania hatupo munafikiri.. Magufuli katuimarisha na fikra awamu hii..
 
Ni lugha ipo inayo chochea uvunjifu wa amani, mtu akikuambia kuwa Safari hii mkiiba kura hapatatosha kwako hiyo Ni lugha ya kichochezi kweli ? Mbona anapo sema kuwa Kama atashindwa kiuhalali atakubali matokeo mbona kwa Hilo hamliungi mkono ?.
Swali ni atasibitisha vipi kama ameshindwa kuhalali wakati hamuamini tume, wala polisi wala chombo chochote cha serikali ?
Emu nisaidie nifahamu namna atakavyothibitisha?
 
Kila mtu anayefanya kazi yake.. munataka awataje hao viongozi wasio na sifa.. kama vile IGP ni wa Chadema.. kama vile Lissu ni mfalme.. huku ni mwananchi tu sasa na baada ya uchaguzi..

Mupunguze.. kutunga tunga kisa.. munajuwa hana sera za kuvutia.. watanzania hatupo munafikiri.. Magufuli katuimarisha na fikra awamu hii..
Mupunguze , munataka , munajua!!

We ni mrundi au mcongo?
 
Ni lugha ipo inayo chochea uvunjifu wa amani, mtu akikuambia kuwa Safari hii mkiiba kura hapatatosha kwako hiyo Ni lugha ya kichochezi kweli ? Mbona anapo sema kuwa Kama atashindwa kiuhalali atakubali matokeo mbona kwa Hilo hamliungi mkono ?.
keshasema na kutangazia uma kwamba hana imani na Tume ya uchaguzi, maana yake tayari anajiandaa kwa shari maana anajua hatashinda.

Sent from my G3226 using JamiiForums mobile app
 
This guy is very unfortunate to be IGP in this term Government. He knows it, however what can he do??!-- he is protecting his position so he has to please "the king".
 
Ninachoona ni kuwa wanajiandaa kwa matukio baada ya matokeo kutoka kufuatia kauli ya Lissu kuwa akishindwa kwa kuonewa anaingiza watu barabarani.

Swali ni je wanajua matokeo yatakuaje?
Hawakujiandaa na hali hi Nguvu ya losusiyo yaKawaidaUmma umeamua uhuru na kazi ni yeyey2020
 
Mbona jiwe kila siku anakesha kwenye madhabahu za kidini Tena mbaya kabisa anazitumia kwa kutola rushwa.
Vipi mama Daudi ebu kuwa mpole.
Kushinda madhabahuni ndio tabia yake na mapenzi yake kwa mwenyezi Mungu. Tena tumshukuru sana anaiongoza nchi kwa kumtegemea Mungu
 
Kushinda madhabahuni ndio tabia yake na mapenzi yake kwa mwenyezi Mungu. Tena tumshukuru sana anaiongoza nchi kwa kumtegemea Mungu
Ndio atumie mimbari kwa kutoa rushwa, naelewa kuwa hata shetani anayambua kuwa Mungu yupo na anatetrmeka anapo kusikia Hilo jina. Mama Daniel wewe VP mbona hivyo.
 
Back
Top Bottom