Je, Allah alikuwepo kabla ya kushuka Quran?

Mbona ujajibu yale maswali mepesi niliyo kupa ni matano yajibu kwa namba
1)......
2)......
3)......
4).......
5).......
Nataka refa FaizaFoxy na wasomaji waelewe hatua kwa hatua
Mbona nimejibu yote kasoro la kufa kwa nabii issa tu
 
Mbona nimejibu yote kasoro la kufa kwa nabii issa tu
Nilitaka unijibu kwa mpangilio kama yalivyo mfano swali la
1) jibu ni Issa siyo Mungu bali ni mtume wa mwenyezi mungu .
2)jibu Muhammad siyo mungu bali naye ni mtume wa mwenyezi Mungu..
Nilitaka ujibu kwa mtiririko ili wasomaji waelewe ...sasa wewe umeanza kujibu kwa kujishitukia na kutengeneza makisiyo yasiyo kuwa kwenye swali
 
Hapana hayo makisio ni koment nyengine ila Kuna koment huko juu nilikujibu labda tu useme sikueka namba kama ulivyo fanya wewe ndio tofauti
 
Mbona maswali haya mepesi sana mzeee issa ni mtume na Muhammad ni mtume mtume wa mwisho ni Muhammad s a w na issa kua hai ama kufa sina elimu nalo ila kwa hakika kila nafsi itaonja umauti
Lwiva au hukuiona hii ndugu yangu nilipo kujibu huko juu
 
Mbona maswali haya mepesi sana mzeee issa ni mtume na Muhammad ni mtume mtume wa mwisho ni Muhammad s a w na issa kua hai ama kufa sina elimu nalo ila kwa hakika kila nafsi itaonja umauti
Sasa kama swali moja kati ya hayo mepesi yamekushinda vp niendelee kukuuliza 🙄 ngoja tumwite Refa labda yeye ataokoa jahazi kuhusu swali la issa kufa au la FaizaFoxy njoo kuokoa jahazi
 
Sasa kama swali moja kati ya hayo mepesi yamekushinda vp niendelee kukuuliza 🙄 ngoja tumwite Refa labda yeye ataokoa jahazi kuhusu swali la issa kufa au la FaizaFoxy njoo kuokoa jahazi
Uliza maswali kijana unadhani kuna anaejua kila kitu au itakua majibu ya maswali uloyataka nimeshakupa ukitoa hilo la issa
 
Mbona maswali haya mepesi sana mzeee issa ni mtume na Muhammad ni mtume mtume wa mwisho ni Muhammad s a w na issa kua hai ama kufa sina elimu nalo ila kwa hakika kila nafsi itaonja umauti

Uliza maswali kijana unadhani kuna anaejua kila kitu au itakua majibu ya maswali uloyataka nimeshakupa ukitoa hilo la issa
Na kuhusu hayo maswali kuwa mepesi unayo sema mepesi ndiyo hayo hayo yaliwafanya mashekh kunyosha mikono juu...hadi shekh mmoja kutaka kukanusha kauli yake mwenyewe ya kuwa "issa ni mtume " ambayo kama ilivyo wewe umekili kuwa ni mtume yeye baada ya kuona swali gumu akataka kusema ni mja wa mwenyezi mungu ila siyo miongoni mwa mitume, ila mashekh wenzake wakamwambia wakubali tu kuwa,swali limewashinda kuliko.kuanza kukanusha utume wa issa😁😁😁
 
We jamaa unamaandiko yanayothibitisha hili ?

mgen inamankusweke Baljurashi Adiosamigo
 
Mbona kakujibu vizuri tu, hajui. Unataka aseme uongo?
Kazi ya refa ni ipi ...wewe toa jibu kwani hapa hakuna mashekh au na nyinyi mnaenda msikitini kama makondoo ..ndiyo maana nilichagua refa wa dini yake ...na ndiyo maana niliwaambia wale mashekh wawe 6 kila mmoja nitampa swali moja hakuna aliye weza kunijibu tena bila ya ubishi
 
Duh umeua naona shura ya maimam wa JF wamekula kona
 
Mpagani ni anaye abudu miungu wengi yey Alikuwa Ana amini mafundisho ya Ibrahimu na kufuata tamaduni za Ibrahimu.
ACHA zako bro!!...baba yake Muhammad alikuwa mpagani na walikuwa wanaabudu miungu mwingine tu hapo arabuni mixer kuuana na mpk Leo mkienda kuhijj Kuna kibox mnakizungukaga embu katafute historia ya vilivyomo mule ndani kama siyo hiyo ya hao wapagani wa hapo arabuni
 
Mimi nitakujibu kwa uchache kuhusu Uislamu, japo mimi ni mkristo.

1. Uislamu Kabla ya Nabii Muhammad

Katika mtazamo wa Kiislamu, Uislamu si dini iliyoanzishwa na Nabii Muhammad (s.a.w.) pekee, bali ni dini ya kimapokeo inayojulikana kama Dini ya Tauhidi—imani katika Mungu Mmoja. Katika Qur’an, inaelezwa kuwa manabii waliotangulia kama Ibrahim (Abraham), Musa (Moses), na Isa (Yesu) wote walikuwa "Waislamu" kwa maana ya wale waliojitoa kwa Mungu Mmoja. Hii inamaanisha kuwa dhana ya Uislamu kwa msingi wa kiimani, yaani kumwamini Mungu Mmoja (Allah) na kumtii kwa maelekezo yake, imekuwepo hata kabla ya Nabii Muhammad (s.a.w.). Kwa hiyo, Uislamu kwa maana pana ya "kujisalimisha kwa Mungu Mmoja" unachukuliwa kuwa uliwepo tangu zamani.

2. Kitendo cha Nabii Muhammad Kusema "Mimi ni wa Kwanza Kusilimu"

Nabii Muhammad alipotamka kuwa yeye ni wa kwanza kusilimu, alimaanisha kuwa yeye ndiye wa kwanza kupokea na kutii wahyi wa Qur’an, ambayo ni ujumbe mpya ulioshushwa kwake ili kukamilisha na kusahihisha mafunzo ya vitabu na mafundisho ya manabii wa zamani. Hii haimaanishi kwamba hakukuwa na watu waliomwamini Mungu Mmoja kabla yake, lakini kwa mujibu wa Uislamu, mafundisho yao yalipotoshwa na wanadamu kwa vipindi tofauti vya kihistoria.

3. Uwepo wa Allah Kabla ya Qur’an na Vitabu Vingine

Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ni Mungu ambaye ameumba kila kitu na yupo daima. Vitabu kama vile Taurati (Torah), Zaburi (Psalms), na Injili (Gospels) vinatajwa katika Qur’an kuwa vilitumwa na Mungu kwa watu wa wakati huo kupitia manabii kama Musa (Moses), Daudi (David), na Isa (Yesu) kwa ajili ya kuwaongoza kwenye imani na matendo mema. Hata hivyo, waislamu wanaamini kwamba baadhi ya mafundisho ya vitabu hivi yalibadilishwa na wanadamu kwa muda na matukio tofauti ya kihistoria, na hii ndiyo sababu Qur’an ilishushwa kama mwongozo wa mwisho na ambao haubadiliki, kwa kuwa Mungu ameahidi kuulinda.

4. Kwa Nini Vitabu vya Zamani Kama Taurati, Zaburi, na Injili Havikulindwa?

Kwa mujibu wa tafsiri ya wanazuoni wa Kiislamu, Allah aliruhusu vitabu vya awali kuvunjika au kubadilishwa kwa kuwa vilikuwa kwa ajili ya makundi maalum ya watu, na vilikuwa na kipindi maalum cha muda. Qur’an inaelezwa kuwa ni ujumbe wa mwisho kwa wanadamu wote, na kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ameahidi kuulinda ujumbe huu dhidi ya mabadiliko ya wanadamu. Hii ndiyo sababu Qur’an inachukuliwa na waislamu kama mwongozo wa kipekee na wa mwisho.

5. Uislamu na Ufanano wa Qur’an na Vitabu vya Zamani

Uislamu unaamini kuwa mafundisho ya msingi kuhusu Mungu, uadilifu, na maadili ni ya kudumu na yamekuwepo kwa vizazi vyote. Qur’an inasema kuwa kuna mambo ya msingi yaliyoshirikishwa katika vitabu vyote vya mbinguni, kwa sababu ya ujumbe wa pamoja kuhusu Mungu Mmoja. Hata hivyo, Qur’an inajitofautisha kwa namna nyingi, ikiwemo jinsi ilivyoshushwa, mfumo wake wa lugha, na mwelekeo wa jumla wa kisheria na kijamii ambao unakidhi mahitaji ya wakati wote.
 
Refa kazi yake kuwa neutral.

Kama hujakubaliana na hoja yake leta yako.

Swali kakujibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…