Je, baba alitutesa au alitufundisha maisha?

Kuna utafiti unaonesha watoto walioteswa au kuwa mbali na baba zao, hutafuta upendo kwa wanaume baki, au ikitokea mwanaume akamuonesha ukarimu na wema fulani, basi atakuwa karibu naye kwani hakuyapata hayo kwa Baba yake, na ukaribu ukupitiliza, yanatokea haya yanayopigiwa mwayo zama hizi.
 
tatizo wazazi wengi wanafikiri kufanya kukomeshea au kuonekana una hasira kunamfanya mtoto awe na tabia nzuri na huku kila mtu anazaliwa kivyake kama una asili ya uvivu ,ukaidi utakua hiyo..Kibaya zaidi unampoteza mtoto maana nayeye anaishi nyumbani kwa masharti ndio unampoteza maana hutakaa kama mzazi kufahamu changamoto binafsi za mtoto. Maana utakuta mtoto anaweza kuwa na shida ila umeshamounesha hii picha anaona anaweza kumuambia ukampiga, adhabu mwisho siku anaamua kukausha.....Ndio hapa unakuta mzazi anajua mwanae yuko hivi kumbe yuko tofauti...Wazazi tutumie mbinu tofauti kuwajengea uwezo, tabia, watoto huuu ubabe wa kipumbavu haufai,,,,Nazungumza hapa maana kaka yangu ni mlemavu baada ya mzee kulazimisha kumbebesha mzigo wa mahindi tena nakumbuka mama kamuambia mpunguzie aende arudie akakataa kaka akajitwisha mara ya kwanza akashindwa mama akasimama akamuambia mzigo ni mkubwa akalazimisha kaka yangu akajitwisha akaufikisha kichwani alitembea kama hatua tatu akaanguka basi akalia sana kwa maumivu kumsogelea hakuweza kusimama baba akawa anadhani anakiburi akatafuta fimbo akaanza kumchapa bro hakusimama mpaka masaa bado yuko chini kumpeleka hospitali wakasema uti wa mgongo umpata hitilafu..tokea siku hiyo akawa wa wheelchair ...i hate him
 
Fact mkuu Hilo halina ubishi wazazi wanatumia Sana force kwenye malezi
 
Inawezekana lakini sio wote yanachangia na malezi yako
 
Umefaidika aje na haya mateso? Pole kwa kufiwa na ndogo wako, natumaini hakufariki akiwa anapitia mateso ya mzazi wake.
Mkuu 50% yamenisaidia..tushapoa mkuu tunazidi kumuombea apumzike salama kifo Cha mdogo wangu ni mipango ya mungu
 
Mkuu Ilo kweri mzee alituanda kwa ajili ya maisha ya kesho ..Japo muda mwingine tuliteseka Ila heshima nyingi kwake mshua
 
Kwa heshima na taadhima kupitia ushahidi wa tukio la matofali napenda kukwambia kuwa baba yako alikua mshamba sana
 
Mshukuru Mungu hukawa shoga,umelelewa vyema malezi mabovu huharubu watoto
Kuwa shoga ni malezi au tabia Kuna mashoga wengine general wamezaliwa wako hivyo so unaweza ukapitia msoto mkali na mwisho wa siku ukawa shoga
 
BABA YAKO ALISHINDWA KUTOFAUTISHA MAISHA YA JESHI NA FAMILIA, YAAN ALIKUA ANAWAFANYIA YALE ALIYOFANYIWA JESHINI.
 
Mkuu tulifundishwa maisha na kudhamini na heshima so kwangu sijaona Kama Yuko hivo
Kwenye uzi wako umeuliza swali kwahiyo usitake kusikia majibu uliyojiandaa kuyasikia tu unatakiwa ukubaliane na majibu yote.

Baba yako alikua mshamba kwasababu alishindwa kutofautisha maisha ya kazini na maisha ya nyumbani hadi kwa majirani, kijeshi amefeli pia maana kashindwa kubadilika kuendana na hali ya mazingira yanayo mzunguka
 
BABA YAKO ALISHINDWA KUTOFAUTISHA MAISHA YA JESHI NA FAMILIA, YAAN ALIKUA ANAWAFANYIA YALE ALIYOFANYIWA JESHINI.
Mkuu pamoja na yote hatujawahi kujuta kwa malezi yake imetufanya tuwe strong kupambana na dunia na maisha ya sasa
 
Mshamba sio hoja nzuri mkuu inabid utoe hoja zenye mantiki ili tuweze kujifunza sis wenyew hatujutii kwa yote aliotufanyia kweny malezi yake kweny familia yetu pamoja na yote tunamkubali Sana
 
Mshamba sio hoja nzuri mkuu inabid utoe hoja zenye mantiki ili tuweze kujifunza sis wenyew hatujutii kwa yote aliotufanyia kweny malezi yake kweny familia yetu pamoja na yote tunamkubali Sana
Sasa kwanini umekuja kuuliza swali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…