Je, Binadamu tulikuja duniani kimakosa au ni mipango ya Mungu?

Biblia inasemaje kuhusu mtoto wa Adam mkubwa kumuua mwenzie mdogo....Mimi ninavyojua kisa kilikua kwamba Mtoto mkubwa wa Adam hakutaka pacha wake aolewe na mdogo wake
Mkuu unahitajia kitu gani mana ulishatoka nje ya uzi tayari
 
Kujua tulipotoka
Umeshajua tayari kwamba ni kutoka kwa Adam na Hawa,sasa unaulizia watoto wake?

Nakushauri tu ukajikite kusoma history kwa mujibu wa vitabu vya imani yako na sio unauliza humu kila mtu anatoa uoni wake,huwezi kujifunza kwa hakika humu
 
Umeshajua tayari kwamba ni kutoka kwa Adam na Hawa,sasa unaulizia watoto wake?

Nakushauri tu ukajikite kusoma history kwa mujibu wa vitabu vya imani yako na sio unauliza humu kila mtu anatoa uoni wake,huwezi kujifunza kwa hakika humu
Sitaki nisimamie upande mmoja ndio maana nipo humu nipate data mbalimbali....nimeona vitabu vya dini hizi kuu kutofautiana kwenye Eden wengine wanasema ilikuwepo hapa duniani wengine wakisema ilikuwepo mbinguni....naendelea kukusanya data nakupima
 
Sitaki nisimamie upande mmoja ndio maana nipo humu nipate data mbalimbali....nimeona vitabu vya dini hizi kuu kutofautiana kwenye Eden wengine wanasema ilikuwepo hapa duniani wengine wakisema ilikuwepo mbinguni....naendelea kukusanya data nakupima
Safari njema
 
Mkuu naomba kukuuliza...kipi kinakufanya uone ukristo ni imani sahihi?
 
Mkuu naomba kukuuliza...kipi kinakufanya uone ukristo ni imani sahihi?
Nimeprove beyond doubt,hapa naongelea mkristo anayejitambua siyo waigizaji.Sasa usiwaone wengine huko wasiojua inamanisha nini kuwa mkristo ukazani huo ndiyo ukristo.Wakati wewe uko shule kama ulikuwa unaenda library mimi pia nilikuwa naenda kufuatilia kuhusu dini ya ukristo.Niamini otherwise utasubiria sana au kama una muda na wewe mwombe Mungu akusaidie,ukristo ni njia ya kweli kwa yule atakayekuwa amempokea Yesu kwa kumanisha na kujitenga na dhambi otherwise wengi ni wakristo kwa maana wanajaza kwenye document tu.Yesu alikuwa wazi alisema"mtawatambua kwa matunda yao".Kama wewe ni mkristo unajiita na unaendeleana uzinzi,uasherati,uongo,unaenda disco,singeli,wizi,ulevi na kanisani unaenda ,jitafakari unapoteza muda wako.Biblia inajua kuna wasanii ikasema "wengi watatamani lakini wasiweze" na ukisoma Yohana 11:12,Tangu enzi za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni unatekwa na wenye nguvu.
Kama siku inapita au wiki hujafikiria jambo lolote juu ya ufalme wa Mungu uko busy na maisha yako wewe huna safari ya mbinguni.Ukisimamam vizuri tabia za uungu zinaumbika kwakoau kwa lugha nyingine ni "kumlingana Kristo".
Mkuu mambo mengine siwezi kuyaweka hapa kwa sababu fulani lakini mimi ni mwanadamu naishi na watu pia,nawajua hao wengine.Mkristo anayejitambua si mtu wa kawaida.Wengine wanasaidiwa na adui nao wameteka wengi.kama ulikuwa hujui shetani amegundua akitumia dini feki au watumishi feki anawapata wengi na hiki ndicho kipo na kimekuwepo duniani muda sasa.
Nina mengi ila siwezi kuyatoa hapa,karibu kanisani ufundishwe.
katika waanzilishi wote wa dini ni Yesu pekee alisema "naenda kuwaandalia makao ili nitakapokuwepo na ninyi muwepo" wengine hatujui watawapeleka wapi wafuasi wao.Ni Yesu pekee aliwaambia wanafunzi wake "mkiniamini mimi mtatenda hata makuu kuliko haya".Kuna dini waanzilishi wao walifanya miujiza baada ya hapo uwezo huo wa kufanya miujiza haupo kwa wafuasi wao ila kwa wakristo wa kweli wameendelea kufanya miujiza.Please note simanishi kila penye miujiza pana Mungu wa kweli,dini si miujiza tu.
Yesu pekee alikufa akafufuka ingawa zimekuwepo propaganda kuonyesha hakufufuka,lakini hii haiondoi ukweli.Ukiacha biblia Mungu wa Israel hata leo anaongea na watu na kuwa juza mengi yanayokuja,kuna watu wanaamini Mungu aliishia kuongea na wanadamu kwa Mussa tu.Kama Yesu alikufa kisha akafufuka maana yake aliishinda mauti nasi tutafufuka,wengi wanaishi maisha ya dhambi wakitegemea kuombewa siku wakifa.Hakuna sala za marehemu ya kumtoa mtu kuzimu kwenda mbinguni kama hizo sala ni kweli basi Mungu ni mwongo kitu ambacho si kweli kwa maana kila anayekufa wanasema "alazwe mahali pema peponi" kwa hiyo jehanamu hakuna watu si wote wako peponi kama sala hizo zimesikilizwa.
Tusidanganyane maisha ni kuchagua haiwezekani uishi maisha ya dhambi kisha ukifa uende mbinguni hizo siyo principle za kiungu.Lazima uishi maisha matakatifu siku zote,ukifa tu hukumu,kabla hawajakuombea Mungu ameshahukumu,kwa hiyo hizo sala na maombi kwa marehemu ni mapokeo ya kibinadamu tu hakuna maandiko ya kwenye biblia.
karibu ujifunze,muda haupo fanya uamuzi leo hizi ni siku za hatari.
Regards
Aqua
 
Biblia inasemaje kuhusu mtoto wa Adam mkubwa kumuua mwenzie mdogo....Mimi ninavyojua kisa kilikua kwamba Mtoto mkubwa wa Adam hakutaka pacha wake aolewe na mdogo wake
Mkuu maswali yako ulivyoanza nilikuuliza source ukasema umesoma Qurani,mimi nimekushauri usome Biblia pia.Tumia muda soma biblia utaujua ukweli,kumbuka ilianza Biblia na Qurani ikafuata baadaye,ushari wangu kasome kwanza Biblia.Michanganyo haitaisha ,unatakiwa kwanza ujenge msingi hata nikikujibu kama msingi hauko vizuri nyumba haiwezi kuwa imara.
 
Mkuu unazunguka zunguka mafumbo kwa sana sijui kwanini unafanya hivi?

Labda niseme tu kwamba usahihi wa imani haupimwi kwa kiwango/kiasi cha imani uliyonayo,ndio maana nikataka kujua ni jambo gani linalofanya uone ukristo ndiyo imani sahihi?
 
Mkuu sisi wengine hatusemi hivyo kwa mujibu wa hoja zetu sahihi,labda watu wa mitaani tu wasioelewa lolote .

Unaposema tunasema jua sio wote labda baadhi tu
Unasema hoja zenu sahihi kwa ithibati ipi? Unaweza kututhibitishia huo usahihi wa hoja zenu?
 
Hivi vitabu vya dini vitakuchanga sana kwa sababu vyenyewe tu vimejichanganya
 
Kwako wewe ushahidi uliokamilika ni upi ?
Nautokee wapi?

Ushahidi uliokamilika ni ule usiohitaji kuaminishwa hasa kwenye suala kama hili... mfano kula, kulala, kupumua etc... sihitaji someone else aniambie kuna supernatural power... kuna this and that..... suala hili linapaswa liwe natural na lisiwe tegemezi...

kumwambia mtu asome Quran au biblia ndio ajue ukweli... waliosoma quran wameishia kwenye quran na waliosoma biblia wameishia kwenye biblia na wachache wamebadili mtazano... kama wapo waliobadili manake yake ili universal set ikamilike watakaokacha lazima wawepo... na wamekacha for very good reasons... hatuendeshwi kwa imani bali tunaendeshwa base on principles. (Na binadamu aliyepiga hatua ni yule anaepigania kuziba gaps)
 
Mkuu unazunguka zunguka mafumbo kwa sana sijui kwanini unafanya hivi?

Labda niseme tu kwamba usahihi wa imani haupimwi kwa kiwango/kiasi cha imani uliyonayo,ndio maana nikataka kujua ni jambo gani linalofanya uone ukristo ndiyo imani sahihi?
Mkuu inawezekana kweli ukaona ninazunguka zunguka lakini mengine siwezi andika hapa,tuanaongelea imani za watu.Nchi yetu haina dini watu wake ndiyo wanadini,nimekushauri ufike kanisani ili kujifunza zaidi.
 
kwanza mwadam hajawahi kuishi mbunguni ila aliumwiwa hapa hapa duniani, refer Mwanzo 1 na hatavhadi mwanadam anarubuniwa na malaika muasi ilikuwa ni hapa hapa, na ikumbukwe kuwa si kwamba ni sayar yetu pekee ilirubuniwa hapa alijaribu kurubuni katika sayar nyingine pia ila wao hawakulubunika na hata kabla ya malaika mwovu kumlubuni mwanadam onyo lilitolewa kwa sayar zote kuwa kuna malaika ameasi na hana majazi hivyo akijaribu kuwarubuni basi msimkubarie
 
hii miaka ww umeanz kuhesabu toka kizazi cha ngapi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…