Mkuu naomba kukuuliza...kipi kinakufanya uone ukristo ni imani sahihi?
Nimeprove beyond doubt,hapa naongelea mkristo anayejitambua siyo waigizaji.Sasa usiwaone wengine huko wasiojua inamanisha nini kuwa mkristo ukazani huo ndiyo ukristo.Wakati wewe uko shule kama ulikuwa unaenda library mimi pia nilikuwa naenda kufuatilia kuhusu dini ya ukristo.Niamini otherwise utasubiria sana au kama una muda na wewe mwombe Mungu akusaidie,ukristo ni njia ya kweli kwa yule atakayekuwa amempokea Yesu kwa kumanisha na kujitenga na dhambi otherwise wengi ni wakristo kwa maana wanajaza kwenye document tu.Yesu alikuwa wazi alisema"mtawatambua kwa matunda yao".Kama wewe ni mkristo unajiita na unaendeleana uzinzi,uasherati,uongo,unaenda disco,singeli,wizi,ulevi na kanisani unaenda ,jitafakari unapoteza muda wako.Biblia inajua kuna wasanii ikasema "wengi watatamani lakini wasiweze" na ukisoma Yohana 11:12,Tangu enzi za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni unatekwa na wenye nguvu.
Kama siku inapita au wiki hujafikiria jambo lolote juu ya ufalme wa Mungu uko busy na maisha yako wewe huna safari ya mbinguni.Ukisimamam vizuri tabia za uungu zinaumbika kwakoau kwa lugha nyingine ni "kumlingana Kristo".
Mkuu mambo mengine siwezi kuyaweka hapa kwa sababu fulani lakini mimi ni mwanadamu naishi na watu pia,nawajua hao wengine.Mkristo anayejitambua si mtu wa kawaida.Wengine wanasaidiwa na adui nao wameteka wengi.kama ulikuwa hujui shetani amegundua akitumia dini feki au watumishi feki anawapata wengi na hiki ndicho kipo na kimekuwepo duniani muda sasa.
Nina mengi ila siwezi kuyatoa hapa,karibu kanisani ufundishwe.
katika waanzilishi wote wa dini ni Yesu pekee alisema "naenda kuwaandalia makao ili nitakapokuwepo na ninyi muwepo" wengine hatujui watawapeleka wapi wafuasi wao.Ni Yesu pekee aliwaambia wanafunzi wake "mkiniamini mimi mtatenda hata makuu kuliko haya".Kuna dini waanzilishi wao walifanya miujiza baada ya hapo uwezo huo wa kufanya miujiza haupo kwa wafuasi wao ila kwa wakristo wa kweli wameendelea kufanya miujiza.Please note simanishi kila penye miujiza pana Mungu wa kweli,dini si miujiza tu.
Yesu pekee alikufa akafufuka ingawa zimekuwepo propaganda kuonyesha hakufufuka,lakini hii haiondoi ukweli.Ukiacha biblia Mungu wa Israel hata leo anaongea na watu na kuwa juza mengi yanayokuja,kuna watu wanaamini Mungu aliishia kuongea na wanadamu kwa Mussa tu.Kama Yesu alikufa kisha akafufuka maana yake aliishinda mauti nasi tutafufuka,wengi wanaishi maisha ya dhambi wakitegemea kuombewa siku wakifa.Hakuna sala za marehemu ya kumtoa mtu kuzimu kwenda mbinguni kama hizo sala ni kweli basi Mungu ni mwongo kitu ambacho si kweli kwa maana kila anayekufa wanasema "alazwe mahali pema peponi" kwa hiyo jehanamu hakuna watu si wote wako peponi kama sala hizo zimesikilizwa.
Tusidanganyane maisha ni kuchagua haiwezekani uishi maisha ya dhambi kisha ukifa uende mbinguni hizo siyo principle za kiungu.Lazima uishi maisha matakatifu siku zote,ukifa tu hukumu,kabla hawajakuombea Mungu ameshahukumu,kwa hiyo hizo sala na maombi kwa marehemu ni mapokeo ya kibinadamu tu hakuna maandiko ya kwenye biblia.
karibu ujifunze,muda haupo fanya uamuzi leo hizi ni siku za hatari.
Regards
Aqua