Je, Bongozozo ana nia iliyojificha?

.
 
Kujipenyeza kuna hatua.... Hawezi toka 1 akarukia 9
 
Wengi hawatokuelewa katika hili,maana mambo haya huwa yanahitaji hisia zisizo za kawaida,hisia ambazo hutatuliwa na kiungoz kingine cha hisia ambacho ndichjo kinachoendesha hisia zote,jambo hili hawa watoto hawatokuelewa hata uwachape vipi.
 
Imefikia hata sijui nipo jukwaa gani, natamani nisijikute jamii intelligence... Maana JF itakuwa Imevamiwa na facebook users wanaopost picha wakiwa wanakula
 
kuna sehemu imezungumzia timu ya Taifa hapo..?, hivo ni vilabu, huyu mapenzi yake kayapeleka timu ya taifa, why asichukue uraia kabisa
Kipindi cha mashindano ya Euro na World Cup unakuaga wapi?!!
 
Kumfikiria mtu vibaya bila ushahidi ni jambo baya sana.
Ubaya siku akija kujua jamaa anafanya hayo kwa mapenzi yake tu atapiga kimya kimya. Ndivyo walivyo wabongo watakutangaza wewe shoga, fisadi, mwizi n.k halafu siku inagundulika sio kweli wanakaa kimya hawatii neno walau kuomba radhi. Wao ndio kwanza wanatafuta mwingine wa kumzushia.

Wanasema kati ya Watanzania Wanne mmoja ni kichaa lakini mimi nasema kati ya Watanzania Wanne mmoja ni mchawi.
 
Usisahau waliopiga kelele biashara ya utumwa ikakomeshwa ni baadhi ya Wazungu hao hao. Rejea upya matumizi ya neno "HAKUNA".
 
Lumumba wana hofu anamchunguza sizonje
 
Lolote laweza kuwa kweli hata hivyo naamini wahusika wetu hawajalala kama inavyodhani
Naamini wanamjua kuliko tumwonavyo sisi kwahiyo tuwe na amani tu kazi ilishafanywa inafanywa na itaendelea kufanywa
asante
 
Haaaaas agent wa CIA mbona wakitaka kuja tz wanakalibishwa ikulu kabisa na wapo tu kibao ubalozini kwani tz ni north Korea hata serikali ya tz aina tatizo inafanya nao kazi kila siku
Hoja yako sio ya kupuuzwa japo watu wanakupinga.. Unaweza kuta hata ni undercover agent wa CIA
 
Kuna mahali niliona MPAKA amepata access ya ubalozi wetu sijui Ni Korea ....sikumbuki.....Yuko ofisini kea balozi amejiachia kwelikweli.....

Kwenye historian Kuna yule mzungu nimemsahau jina alikaa na wenyeji miaka 30..... Kumbe kidogo kidogo ananunua ile kingdom na kusainisha machief makaratasi .... Na lugha ya Kabila Lile aliongea KABISA.....

Anaweza kuwa na Nia nzuri ila Ni vizuri akichujwa na kuchunguzwa .......

Wenyewe weupe wanasema no free lunch .....

Hivyo tusikenue kenue tu......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…