zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Kumekuwepo na propaganda ya miaka mingi kuwa CCM inajua kuandaa na kulea viongozi sio tu ndani ya nchi mpaka nchi jirani (Enzi za Mwalimu) nakumbuka hta Mhe.Polepole alisema wana master plan ya kuongoza nchi mpaka 2075!!
Kinachonishangaza toka Mama SSH aingie madarakani ni kama vile CCM haikumuandaa wala haikumtarajia kuwa Rais. Ilifika mahali wanaona bora katiba ingebadilishwa turudi kwa uchaguzi. Watu kama kina Polepole nao wamegeuka na kudai chama kimeshikwa na wahuni.
Sasa nachojiuliza kama CCM ni mabingwa wa siasa inakuaje hawakujiandaa na mbadala wa JPM (maana ugonjwa wake ulifahamika) kiasi walalamike as if SSH ni zao la CUF au TLP?
Kingine kama SSH anaonekana ni unfit kuwa Rais, ilikuaje akapitishwa kuwa makamu wa Rais on the first place? Ina maana unaweza kuwa makamu wa Rais bila kuandaliwa kuwa Rais ikitokea emergency??
Back to polepole, kama aliandaa master plan ya CCM mpaka 2075 inakuaje alalamike sasa ilihali Rais wa sasa ni zao la chama kile kile? Au plan haikujiandaa na mabadiliko ya Rais? Na kama haikujiandaa je ile propaganda kuwa CCM ni mabingwa wa succession na strategy politics ni uongo??
Cc The Boss MALCOM LUMUMBA Salary Slip