Je, CCM na TISS wanakuzwa nguvu zao kuliko uhalisia (Overrated)?

Kumekuwepo na propaganda ya miaka mingi kuwa CCM inajua kuandaa na kulea viongozi sio tu ndani ya nchi mpaka nchi jirani (Enzi za Mwalimu) nakumbuka hta Mhe.Polepole alisema wana master plan ya kuongoza nchi mpaka 2075!!

Kinachonishangaza toka Mama SSH aingie madarakani ni kama vile CCM haikumuandaa wala haikumtarajia kuwa Rais. Ilifika mahali wanaona bora katiba ingebadilishwa turudi kwa uchaguzi. Watu kama kina Polepole nao wamegeuka na kudai chama kimeshikwa na wahuni.

Sasa nachojiuliza kama CCM ni mabingwa wa siasa inakuaje hawakujiandaa na mbadala wa JPM (maana ugonjwa wake ulifahamika) kiasi walalamike as if SSH ni zao la CUF au TLP?

Kingine kama SSH anaonekana ni unfit kuwa Rais, ilikuaje akapitishwa kuwa makamu wa Rais on the first place? Ina maana unaweza kuwa makamu wa Rais bila kuandaliwa kuwa Rais ikitokea emergency??

Back to polepole, kama aliandaa master plan ya CCM mpaka 2075 inakuaje alalamike sasa ilihali Rais wa sasa ni zao la chama kile kile? Au plan haikujiandaa na mabadiliko ya Rais? Na kama haikujiandaa je ile propaganda kuwa CCM ni mabingwa wa succession na strategy politics ni uongo??

Cc The Boss MALCOM LUMUMBA Salary Slip
Tiss wamezidiwa ujanja na wanasiasa.
 
Wamejifunza Sasa kuhusu Makamu wa Rais, next time watamchukulia Kama the next president ikitokea dharura, so wataongeza umakini.
 
Lakini mkuu unafahamu kukosekana consistency ya kisera ndio kunaua uchumi wetu?

Mfano tulikubaliana gesi ndio solution ya umeme, ghafla tunaambiwa Stieglers ndio suluhu ya umeme. Same to JK alitaka katiba mpya ghalfa JPM anakuja kusema sio kipaumbele chake ilihali pesa zaidi ya Billion 20 ilitumika kwenye mchakato wa katiba!!! Mpka unajiuliza je CCM ni ile ile au viongozi hawaandaliwi kufuata sera na mrengo wa chama ili wawe na fikra moja tofauti ni strategy tu!!

Trust me 2025 kama atapita Rais Mwingine say Majaliwa utasikia chanjo NO, mara Stieglers gorge isubiri, mara tutumie umeme wa upepo n.k so unakuta nchi inakosa shabaha.

Ndio hapo hoja yangu inakuja je kweli CCM na TISS inaandaa viongozi? Kwanini wakinzane? Chama hakina mfumo wa kujua like-minded candidates to ease transition between phases?

Cc Gerald Magembe
Sasa huyo Maghembe yeye anachoangalia ni yule aliyetoa hela nyingi tu
 
Yaani Mtu akitoboa kwa juhudi zake mnakimbilia kusema eti aliandaliwa.

Weka dhamiri , wake bidii, jiunge na kundi au watu sahihi, heshimu itikadi uliyopo, kuwa muadilifu, hoja zenye mashiko UONE KAMA WENZAKO HAWATAKUKUBALI.

ISUE YA KUANDALIWA HUZUNGUMZWA BAADA YA KUTOBOA
Kwani unadhani kuandaliwa ni kuogeshwa, kupakwa mafuta na kuvalishwa nguo?
 
Kiukweli hakuna Master-Plan wala utalaamu wowote ule ndani ya TISS na CCM. Taasisi za utawala nchini Tanzania zinaonekana zina nguvu kwasababu watanzania wengi tuko gizani kifikra: Hivyo naweza kusema TISS/CCM ni sawa na A BIG FISH IN A LITTLE POND. Wanaweza tu kutuonea sisi, lakini nguvu yao haivuki mipaka ya Tanzania kama ilivyokuwa zamani, huko nje wakicheza vibaya wataliwa vichwa....(Raisi Magufuli alitaka kumuiga Nyerere akaona chamoto)

Pili, TISS/CCM ni vyombo ambavyo vilivamiwa (Got Hijacked) kitambo na kundi la watu wanaojiita wenye nchi au wazee wa nchi. Humo ndani kinachoendelea ni ELITISM, NEPOTISM and CRONYISM. Ndiyo maana hata marehemu Raisi Magufuli alipojaribu kutunisha msuli walimshinda. Sasa madhara ya huu mfumo ndiyo huzaa uzembe, rushwa, ufisadi na kukosa weredi.

Sasa ili kufahamu kwamba TISS/CCM wako overrated au lah, angalia aina ya viongozi wake waandamizi (Top-Brass)na vijana wao, halafu fananisha na viongozi wengine wa nchi jirani na duniani. Ukishafanya hivi utapata jawabu lako. Lakini hakuna Master-Plan, ndani ya TISS/CCM kwasababu hata sera za nchi (Strategic Policies) za miaka 15 ijayo hatuna. Kila mtu akiingia ikulu huja na yake, fujo-fujo tu (No Succession Plan).

Nashangaa sana umemleta Polepole wakati yeye ndani ya CCM ni mtu wa kuja na kuondoka na hana madhara yoyote. Aliyesema CCM ina wenyewe hakukosea, kile ni chama ni mali ya watu binafsi.....
 
Tatizo la siasa huwa limatengeza "Hang over" fulani ya madaraka.

Ona hali anayopitia Pole Pole. Angalia hali anayopitia wafuasi wa Magufuli mitandaoni.

Angalia hali anayopitia Sugu.

Ni kama wamekuwa mateja fulani wa madaraka na wameporwa ghafla hali waliokuwa wameizoea.

Na tatizo la wafuasi wa wanasiasa ni kuwa kwenye cult-followership. Yaani hutumii kabisa kichwa, mtu anameza kila anachoambiwa na mwanasiasa.

Yaani mtu na akili zako timamu unakaa unaamini kila anachosema pole pole, kweli ?

Mimi mtu akimtumia Magufuli kama standard ya Uongozi hata cha kumjibu nakosa
 
Kiukweli hakuna Master-Plan wala utalaamu wowote ule ndani ya TISS na CCM. Taasisi za utawala nchini Tanzania zinaonekana zina nguvu kwasababu watanzania wengi tuko gizani kifikra: Hivyo naweza kusema TISS/CCM ni sawa na A BIG FISH IN A LITTLE POND. Wanaweza tu kutuonea sisi, lakini nguvu yao haivuki mipaka ya Tanzania kama ilivyokuwa zamani, huko nje wakicheza vibaya wataliwa vichwa....

Pili, TISS/CCM ni vyombo ambavyo vilivamiwa (Got Hijacked) kitambo na kundi la watu wanaojiita wenye nchi au wazee wa nchi. Humo ndani kinachoendelea ni ELITISM, NEPOTISM and CRONYISM. Ndiyo maana hata marehemu Raisi Magufuli alipojaribu kutunisha msuli walimshinda. Sasa madhara ya huu mfumo ndiyo huzaa uzembe, rushwa na kukosa weredi.

Sasa ili kufahamu kwamba TISS/CCM wako overrated au lah, angalia aina ya viongozi wake waandamizi (Top-Brass)na vijana wao, halafu fananisha na viongozi wengine wa nchi jirani na duniani. Ukishafanya hivi utapata jawabu lako. Lakini hakuna Master-Plan, ndani ya TISS/CCM kwasababu hata sera za nchi (Strategic Policies) za miaka 15 ijayo hatuna. Kila mtu akiingia ikulu huja na yake, fujo-fujo tu.

Nashangaa sana umemleta Polepole wakati yeye ndani ya CCM ni mtu wa kuja na kuondoka na hana madhara yoyote. Aliyesema CCM ina wenyewe hakukosea, kile ni chama ni mali ya watu binafsi.....

Kwa CCM ..Samia is far better than Magufuli..
Kwa maana Samia anaheshimu CCM family tree...

Na anaruhusu hata watu kubishana ndani ya Ccm...

Mleta Mada anasema Samia hakuandaliwa.
Je Magufuli aliandaliwa?Alikuwa better?Kwa vigezo vipi?
 
So wewe na ukoo wako mnaweza kupambana wakati hata pesa tu ya mlo ni shida

USSR
Siku hizi umechanganyikiwa sana mkuu hadi nakuonea huruma. Hivi kwanini mliwekeza nguvu kubwa kwa mtu binafsi badala ya taasisi?
 
Kwa CCM ..Samia is far better than Magufuli..
Kwa maana Samia anaheshimu CCM family tree...

Na anaruhusu hata watu kubishana ndani ya Ccm...

Mleta Mada anasema Samia hakuandaliwa.
Je Magufuli aliandaliwa?Alikuwa better?Kwa vigezo vipi?
Wenyewe.jpg

Kushika madaraka ili kuendeleza gurudumu la Elitism, Cronyism na Nepotism CCM huwa wanawekana tu. Raisi wa Tanzania huwa hatoki mbali na viunga vya wenye nchi (The Inner Circle). Ujio wa Raisi Magufuli was a malfunction in a system ndiyo maana ulitokea mtafaruku mkubwa sana. Sasa kukuthibitishia hili, nimekuwekea picha ambayo inaonyesha Kamati Kuu (KK) kipindi cha Mzee Mkapa, ambapo ndani yake tumepata Maraisi Watatu na Makamu wa Raisi Watatu. Raisi Magufuli was an outcast, ndiyo maana mfumo ulimishinda nguvu,......

Samia being better than Magufuli, on a personal level it is an undisputed: She's cool, calm and collected.
Samia being any better than Magufuli, on a statesmanship: This is highly debatable and yet to be seen....
 
Kiukweli hakuna Master-Plan wala utalaamu wowote ule ndani ya TISS na CCM. Taasisi za utawala nchini Tanzania zinaonekana zina nguvu kwasababu watanzania wengi tuko gizani kifikra: Hivyo naweza kusema TISS/CCM ni sawa na A BIG FISH IN A LITTLE POND. Wanaweza tu kutuonea sisi, lakini nguvu yao haivuki mipaka ya Tanzania kama ilivyokuwa zamani, huko nje wakicheza vibaya wataliwa vichwa....(Raisi Magufuli alitaka kumuiga Nyerere akaona chamoto)
Kwanza binafsi nilikuwa naamini hiki kitu, ila baada ya Magufuli kuingia madarakani nikaona dhahiri nchi hii hakuna nguvu ya ziada nyuma ya Urais.

Hizi stori zote za Deep state nilikuja kugundua kwa Tanzania Deep state ni Rais mwenyewe. Magufuli alithibitisha hili.

Magu alifanya vitu vya kutisha kwa maamuzi yake mwenyewe tena vingine vimeligharimu sana taifa ambavyo kama kweli kungekuwq na hiyo nguvu tungeona tofauti.

Nakuthibithia hata kama Magu angekataa kuachia madaraka hakuna mtu yeyete anagemfanya chochote, maana kila mtu alikuwa amesha-give up.

Alikuwa weka watu wake kote, kuanzia bunge, mahakamani ma serikalini.

Ukitaka kujua NGUVU aliyokuwa nayo Magu ni ile kauli yake kuwa hakuna mtu mzee kama Lukuvi au Kabudi anaweza kuwa Rais. Maana yake sasa yeye ndio alikuwa Deep state anayeamua ni nani awe Rais baada yake?
Pili, TISS/CCM ni vyombo ambavyo vilivamiwa (Got Hijacked) kitambo na kundi la watu wanaojiita wenye nchi au wazee wa nchi. Humo ndani kinachoendelea ni ELITISM, NEPOTISM and CRONYISM. Ndiyo maana hata marehemu Raisi Magufuli alipojaribu kutunisha msuli walimshinda. Sasa madhara ya huu mfumo ndiyo huzaa uzembe, rushwa, ufisadi na kukosa weredi.
Ugumu wa utawala nchi hii unatokana na ukubwa wenyewe wa serikali jinsi ulivyo, namna ya kuwapata wateule na njia za uwajibishaji kumtegemea zaidi mtu mmoja.

Hapo ndio kuna kuchoka na kuacha tu mambo yapite lakini binafsi sioni kama eti kuna nguvu nyuma.

Mfano, hata kama ni wewe watu walikusaidia kuingia madarakani, halafu ukawateua kwenye mashirika huku wakijua wapo kwasababu wewe upo.

Hivi katika mazingira hayo utaepukaje ubadhirifu na kutokuwajibishana.

Magu angewezaje kumwajibisha Dotto au Kalemani ?
Sasa ili kufahamu kwamba TISS/CCM wako overrated au lah, angalia aina ya viongozi wake waandamizi (Top-Brass)na vijana wao, halafu fananisha na viongozi wengine wa nchi jirani na duniani. Ukishafanya hivi utapata jawabu lako. Lakini hakuna Master-Plan, ndani ya TISS/CCM kwasababu hata sera za nchi (Strategic Policies) za miaka 15 ijayo hatuna. Kila mtu akiingia ikulu huja na yake, fujo-fujo tu (No Succession Plan).
Kuhusu TISS kuwa ya kawaida, nakunaliana kabisa na wewe. Sijui sababu kubwa inaweza kuwa siasa au aina ya recruitment wanayofanya.
Nashangaa sana umemleta Polepole wakati yeye ndani ya CCM ni mtu wa kuja na kuondoka na hana madhara yoyote. Aliyesema CCM ina wenyewe hakukosea, kile ni chama ni mali ya watu binafsi.....
In short, nchi yetu inaendeshwa kwa mtazamo tu wa Rais anayekuwa madarakani.

Ndio maana hata ndani ya CCM Magu aliwavuruga sana, mpaka kuvunja katiba ya chama na hakuna walichokifanya.

Kwa mtazamo wangu,

Naona CCM iliyokuwa na dira ilikiwa CCM ya Mwalimu Nyerere.

Ila baada ya sera za uchumi za Nyerere kushindwa, kilichopo sasa hivi ni kama CCM inashikilia madaraka kwa nguvu huku ikijitafuta.

Na ndio maana CCM imejitahidi sana kushikilia makundi yote muhimu ya kijamii kama vyama vya wafanyakazi, timu za mpira, viongozi wa dini, na wanamuziki.

Vile vile CCM imejishikanisha na Dola, hakuna namna utatenganisha ÇCM na Dola. Leo makanari wa Jeshi wanapewa ukuu wa mikoa, wialaya, ubalozi, nafasi kwenye mashirika n.k. hivyo hakuna namna hawa watu wakawa kinyume nao.
 
View attachment 2055912

Kushika madaraka ili kuendeleza gurudumu la Elitism, Cronyism na Nepotism CCM huwa wanawekana tu. Raisi wa Tanzania huwa hatoki mbali na viunga vya wenye nchi (The Inner Circle). Ujio wa Raisi Magufuli was a malfunction in a system ndiyo maana ulitokea mtafaruku mkubwa sana. Sasa kukuthibitishia hili, nimekuwekea picha ambayo inaonyesha Kamati Kuu (KK) kipindi cha Mzee Mkapa, ambapo ndani yake tumepata Maraisi Watatu na Makamu wa Raisi Watatu. Raisi Magufuli was an outcast, ndiyo maana mfumo ulimishinda nguvu,......

Samia being better than Magufuli, on a personal level it is an undisputed: She's cool, calm and collected.
Samia being any better than Magufuli, on a statesmanship: This is highly debatable and yet to be seen....
Magufuli aliwekwa madarakani na Mkapa. Ushahidi unaonesha hivyo.

Kwa CCM ..Samia is far better than Magufuli..
Kwa maana Samia anaheshimu CCM family tree...

Na anaruhusu hata watu kubishana ndani ya Ccm...

Mleta Mada anasema Samia hakuandaliwa.
Je Magufuli aliandaliwa?Alikuwa better?Kwa vigezo vipi?
Naheshimu Mchango wako mkongwe but quote me corrected "unazungumziaje Magufuli kabla na kutoka CCM, chama kilikua na hali gani kwa wananchi wa kawaida mitaani?

Viongozi na wanachama walikua hawana audacity hata ya kuvaa sare na mabango ya chama kitaa, vikaoni matawini walikua wanaenda na vibegi ama majaketi ya kubadilisha before and after vikao.

Na sasa hivi hao hao iliyotaka kuwafia CCM ndio wanapata kibass cha kuongea na kuiongelea CCM.

Trust it or not bila Magufuli ku step in Chama kilikua kinaenda kupasuka pasuka from the roots. A project is a project, mzigo mzito mpatie mnyamwezi. Hata Punda usiyempenda lengo lake ni kukufikishia mzigo salama.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Safi sana mkuu, umemaliza kila kitu
Hajamaliza alitakiwa agusie public investment option ambayo nchi na watu walitaka wa kufanya.
Minimum requirement na kufanya expert ya Gas ni USD 35 billion na wakati huo huo hiyo gas siyo mali ya serikali.
Faida ya moja kwa moja ingekuwa umeme tuu ambao gas bado tuanainunua..
Na Stigler Gorge investment ya kupata 2000 plus MW ni USD 5 to 7 billion, na ni mali yetu sio undeleze kitu cha mwenzako kwa kukimbilia kuvizia kodi tuu.
 
Kumekuwepo na propaganda ya miaka mingi kuwa CCM inajua kuandaa na kulea viongozi sio tu ndani ya nchi mpaka nchi jirani (Enzi za Mwalimu) nakumbuka hta Mhe.Polepole alisema wana master plan ya kuongoza nchi mpaka 2075!!

Kinachonishangaza toka Mama SSH aingie madarakani ni kama vile CCM haikumuandaa wala haikumtarajia kuwa Rais. Ilifika mahali wanaona bora katiba ingebadilishwa turudi kwa uchaguzi. Watu kama kina Polepole nao wamegeuka na kudai chama kimeshikwa na wahuni.

Sasa nachojiuliza kama CCM ni mabingwa wa siasa inakuaje hawakujiandaa na mbadala wa JPM (maana ugonjwa wake ulifahamika) kiasi walalamike as if SSH ni zao la CUF au TLP?

Kingine kama SSH anaonekana ni unfit kuwa Rais, ilikuaje akapitishwa kuwa makamu wa Rais on the first place? Ina maana unaweza kuwa makamu wa Rais bila kuandaliwa kuwa Rais ikitokea emergency??

Back to polepole, kama aliandaa master plan ya CCM mpaka 2075 inakuaje alalamike sasa ilihali Rais wa sasa ni zao la chama kile kile? Au plan haikujiandaa na mabadiliko ya Rais? Na kama haikujiandaa je ile propaganda kuwa CCM ni mabingwa wa succession na strategy politics ni uongo??

Cc The Boss MALCOM LUMUMBA Salary Slip
Ccm hii ni chaka la majizi,maraisi wote waliopita na familia zao,ni majizi tu,taasisi za Ulinzi badala ya kufsnya kazi zao walizosomea,wanatumika kulinda majizi yaliopo Madarakani,
Hii TISS ikiamua kurudi kwenye misingi yake ya kipindi Cha Ukombozi wa Afrika,wakati tulipokuwa tunawanyoa makaburu bila maji,inaweza kutisha kuriko idara zote za ujasusi Afrika mashariki na kati.
Inaweza kutisha kama mossad ya Israel au mukabarat ya Egypt.
 
Kiukweli hakuna Master-Plan wala utalaamu wowote ule ndani ya TISS na CCM. Taasisi za utawala nchini Tanzania zinaonekana zina nguvu kwasababu watanzania wengi tuko gizani kifikra: Hivyo naweza kusema TISS/CCM ni sawa na A BIG FISH IN A LITTLE POND. Wanaweza tu kutuonea sisi, lakini nguvu yao haivuki mipaka ya Tanzania kama ilivyokuwa zamani, huko nje wakicheza vibaya wataliwa vichwa....(Raisi Magufuli alitaka kumuiga Nyerere akaona chamoto)

Pili, TISS/CCM ni vyombo ambavyo vilivamiwa (Got Hijacked) kitambo na kundi la watu wanaojiita wenye nchi au wazee wa nchi. Humo ndani kinachoendelea ni ELITISM, NEPOTISM and CRONYISM. Ndiyo maana hata marehemu Raisi Magufuli alipojaribu kutunisha msuli walimshinda. Sasa madhara ya huu mfumo ndiyo huzaa uzembe, rushwa, ufisadi na kukosa weredi.

Sasa ili kufahamu kwamba TISS/CCM wako overrated au lah, angalia aina ya viongozi wake waandamizi (Top-Brass)na vijana wao, halafu fananisha na viongozi wengine wa nchi jirani na duniani. Ukishafanya hivi utapata jawabu lako. Lakini hakuna Master-Plan, ndani ya TISS/CCM kwasababu hata sera za nchi (Strategic Policies) za miaka 15 ijayo hatuna. Kila mtu akiingia ikulu huja na yake, fujo-fujo tu (No Succession Plan).

Nashangaa sana umemleta Polepole wakati yeye ndani ya CCM ni mtu wa kuja na kuondoka na hana madhara yoyote. Aliyesema CCM ina wenyewe hakukosea, kile ni chama ni mali ya watu binafsi.....
Pengine wewe ndio hujatafuta ukweli katika baadhi ya hoja ulizoibua haoa katika kujaribu kutetea kupinga kwako.
1. Unasema kwamba nchi haina strategic policies za hata miaka 15 ijayo. Hilo sio kweli. Kwa sasa bado tupo kwenye Tanzania Vision 2025 ambayo iliandaliwa more than 25 year ago. Tuna mipango ya miaka mitano mitano kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa mpango huo mkubwa.
2. Unasema kwamba kuna nepotism ndani ya mfumo na chama tawala: Huu nao ni uongo. Hii ni nchi ambayo upendeleo uko chini sana katika mfumo wake wa utawala. Na wala usjijaribu kulinganisha na nchi jirani na hata za ng'ambo. Kwa nchi zingine basi watu kama kina Magufuli, kina Samia, kina Majaliwa, kina Mpango wasingeweza kufika pale juu.
Na hata katika vyombo vya usalama, mbona watanzania wa kada zote wapo.
Cha muhimu pia cha kujua na kutosahau, ni kuepuka kumbagua mtu au kumnyima mtu fursa au kumchukia kisa tu wanafamilia yake waliwahi kuwa viongozi kwenye chama tawala, kwenye utumishi au kwenye vyombo vya usalama. Huo pia ni aina ya ubaguzi.
3. Umeongelea pia kwamba wewe unaona viongozi wetu, cream ni dhaifu kuliko baadhi ya nchi jirani. Huo pis ni uongo unaousema bila kufanya utafiti.
Nchi yetu ina viongozi imara ndani ya chama tawala na ndani ya serikali. Ndio maana hii nchi haipati crisis kirahisi.
Unachotaka wewe ni kuona individuals wakiwa powerful wenyewe tu bila kufanywa powerful na mfumo.
Na katika ukanda wetu wa EAC, sioni nchi ya kulinganishwa nao.
Nchi nyingi za EAC zina powerful individuals. Hawana powerful political parties.
A powerful political party creates a system and produces effective succession in leadership.
 
Pengine wewe ndio hujatafuta ukweli katika baadhi ya hoja ulizoibua haoa katika kujaribu kutetea kupinga kwako.
1. Unasema kwamba nchi haina strategic policies za hata miaka 15 ijayo. Hilo sio kweli. Kwa sasa bado tupo kwenye Tanzania Vision 2025 ambayo iliandaliwa more than 25 year ago. Tuna mipango ya miaka mitano mitano kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa mpango huo mkubwa.
Una maneno mengi sana lakini ni matupu. Strategic Vision 2025 ina malengo makuu matatu:
1. Maisha bora kwa kila mtanzania (Achieving quality and good life for all)
2. Kujenga mfumo bora wa utawala wa sheria (Good Governance and Rule of Law)
3. Kujenga uchumi imara ambao utaleta ushindani duniani (Building resilient and competitive economy globally)

Lengo la huu mkakati lilikuwa ni kuubadilisha uchumi wa Tanzania (Transformation and Modernisation). Sasa ukiangalia tangu Mzee Jakaya ni mangapi yamefanyika kuakisi huu mkakati utafahamu ni machache sana. Miaka 5 ya Raisi Magufuli, mamilioni ya watanzania wameingia kwenye lindi la umasikini na utawala bora ulisiginwa. Naomba katika hili tuache mzaha. Hayo malengo makuu matatu hayajatimizwa kwasababu ya siasa za hovyo za nchi hii....

2. Unasema kwamba kuna nepotism ndani ya mfumo na chama tawala: Huu nao ni uongo. Hii ni nchi ambayo upendeleo uko chini sana katika mfumo wake wa utawala. Na wala usjijaribu kulinganisha na nchi jirani na hata za ng'ambo. Kwa nchi zingine basi watu kama kina Magufuli, kina Samia, kina Majaliwa, kina Mpango wasingeweza kufika pale juu.
Unaongea mambo mengi sana ya kusadikika, inaweza ikawa ni kweli. Lakini uhalisia mchungu ni kwamba sehemu yoyote iliyojaa rushwa kamwe hakuwezi kuwepo na usawa baina ya tabaka la juu na tabaka la chini. Haiwezekani, CCM is a GOLD-STANDARD OF CORRUPTION. Umewaongelea wakina majaliwa, hizo ni nafasi chache sana na za juu.

Ukija kwenye ngazi zenye watu wengi ambazo hazionekani ndiyo utaona uozo wa CCM. Hivi mtu kama Raisi Magufuli alivyokuwa anawachagua wakina Kabula ambao ni wanawake zake alikuwa ana maana gani labda. Kura za maoni alishindwa lakini akapita. Hivi leo unadhani kabisa mama yako mzazi akienda kugombea jimbo la mama Salma, hata kama kamshinda vigezo anaweza kupita ??? Hawa wakina Nape walipokuwa na vyeo walifanya juu chini hadi wakwe zao wapenyezwe..Tuna mengi ya kusema ila niishie hapa

Na hata katika vyombo vya usalama, mbona watanzania wa kada zote wapo.
Cha muhimu pia cha kujua na kutosahau, ni kuepuka kumbagua mtu au kumnyima mtu fursa au kumchukia kisa tu wanafamilia yake waliwahi kuwa viongozi kwenye chama tawala, kwenye utumishi au kwenye vyombo vya usalama. Huo pia ni aina ya ubaguzi.
Iko hivi, binafsi sina tatizo kabisa na watoto wa vigogo. Hata mkitaka kuwaweka ukoo mzima wa Samia waweke tu. I COULD CARE LESS. Tunachotaka sisi ni weredi na uwezo, leo hii watanzania ambao ni viongozi wana uwezo mdogo kwasababu ya michezo yenu ya kamlete. Mbali na hapo mmeiga michezo ya Warusi ya NOMENCLATURA, kwamba mnaweka makada hadi kwenye nafasi ambazo hawatakiwi kuwekwa wanasiasa......SHAME

3. Umeongelea pia kwamba wewe unaona viongozi wetu, cream ni dhaifu kuliko baadhi ya nchi jirani. Huo pis ni uongo unaousema bila kufanya utafiti.
Ndiyo viongozi wengi waandamizi wa Tanzania (TOP-BRASS) ni watu wasiokuwa na uwezo. Kama unabisha leo hii omba uone PhD za hao vijana wenzenu Jafo na Dotto, au hata ili ya marehemu iliyofichwa. Lakini kuwa zaidi, akili ya mtu hatuipimi kwenye shule peke yake, tungaalia mambo mengi.

Akili ya viongozi inapimwa kwa kuangalia maamuzi yenye maslahi mapana ya taifa kwa muda mrefu (How often does a leader make correct and accurate decision affecting a large margin of a population). Sasa ukijiuliza kwanini wizara ilifanya maamuzi ya ajabu kama kufuta masomo ya kilimo, kuunganisha somo la fizikia/kemia na Raisi kusaini mikataba ya hovyo ya madini na kudiriki kabisa kutetea haya maamuzi, utapata picha nchi hii ina viongozi aina gani.

Nchi yetu ina viongozi imara ndani ya chama tawala na ndani ya serikali. Ndio maana hii nchi haipati crisis kirahisi.
Tanzania iko kwenye Crisis. AU mwenzangu Crisis ni mpaka uone machafuko kama Rwanda na Kenya ???
No, No, No! This type of thinking is myopic, bismal, parochial and lackadaisical. Tanzania kuna tatizo la rushwa na ufisadi. Mfumo wetu wa elimu umevurugika, watoto wanaanza kidato cha kwanza hawajui kusoma na kuandika lakini walifaulu mtihani, kuna tatizo kubwa sana la ajira, kuna tatizo la mabadiliko ya hali ya nchi. Can't you see that these are national Crises ???

Unachotaka wewe ni kuona individuals wakiwa powerful wenyewe tu bila kufanywa powerful na mfumo.
Tafadhali sana, usinilisha maneno.....

Nchi nyingi za EAC zina powerful individuals. Hawana powerful political parties.
A powerful political party creates a system and produces effective succession in leadership.
Suala siyo kuwa na chama, hata chama cha KINAZI cha Adolf Hitler kilikuwa na nguvu sana na taasisi imara. Lakini swali la msingi mno kujiuliza ni kwamba chama kinaifanyia nini nchi. Mfumo wa chama mliouiga kule Urusi ulifikirika kwamba ndiyo bora kabisa duniani, lakini baada ya miaka 88 nchi ikaangukia pua. Chama kilikuwa na nguvu kweli, lakini kilijaa rushwa, upendeleo na uhafidhina. Ndiyo CCM ni chama chenye nguvu nchini, hili halina ubishi.

Lakini tukiuliza kama CCM kinaisaidia nchi, hili ni swala ambalo wengi mtamung'unya maneno bila kutoa majibu yaliyonyooka.....
 
Back
Top Bottom