Kumekuwepo na propaganda ya miaka mingi kuwa CCM inajua kuandaa na kulea viongozi sio tu ndani ya nchi mpaka nchi jirani (Enzi za Mwalimu) nakumbuka hta Mhe.Polepole alisema wana master plan ya kuongoza nchi mpaka 2075!!
Kinachonishangaza toka Mama SSH aingie madarakani ni kama vile CCM haikumuandaa wala haikumtarajia kuwa Rais. Ilifika mahali wanaona bora katiba ingebadilishwa turudi kwa uchaguzi. Watu kama kina Polepole nao wamegeuka na kudai chama kimeshikwa na wahuni.
Sasa nachojiuliza kama CCM ni mabingwa wa siasa inakuaje hawakujiandaa na mbadala wa JPM (maana ugonjwa wake ulifahamika) kiasi walalamike as if SSH ni zao la CUF au TLP?
Kingine kama SSH anaonekana ni unfit kuwa Rais, ilikuaje akapitishwa kuwa makamu wa Rais on the first place? Ina maana unaweza kuwa makamu wa Rais bila kuandaliwa kuwa Rais ikitokea emergency??
Back to polepole, kama aliandaa master plan ya CCM mpaka 2075 inakuaje alalamike sasa ilihali Rais wa sasa ni zao la chama kile kile? Au plan haikujiandaa na mabadiliko ya Rais? Na kama haikujiandaa je ile propaganda kuwa CCM ni mabingwa wa succession na strategy politics ni uongo??
Cc
The Boss MALCOM LUMUMBA Salary Slip
CCM Kama chama Legacy yake kubwa inang’arishwa sana na Mwl JK Nyerere hapo ndipo kinapopata heshima kubwa na kuwa ni chama pendwa kwa wazee ,watu wazima na hata baadhi ya vijana (sio wote)
Kwa walio wengi wanakiona CCM ndio chanzo cha amani tulio nayo sasa (siwalaumu). Yawezekana kuna ukweli ndani yake lakini haiondoi ukweli kua mitazamo hiyo imejengwa kutokana na kua na chama kimoja madarakani tangu uhuru na kufumbata madaraka ya uongozi na kuminya kukua na kustawi kwa vyama pinzani (siwalaumu chama chochote kingefanya hivo)
Nje ya tanzania ni kweli CCM inaoneka ni chama imara na kinabeba sifa zote nzuri za uongozi tulizo nazo leo pamoja na amani amabayo tumekua tukisifiwa!!…
Sifa hizo ni pamoja na
-Kuwa chachu ya uhuru wa nchi nyingine za Africa ikiwemo Msumbini,SA,nk
-CCM inatajwa kua ndo kikwazo cha Rwanda kushindwa kuingilia mambo ya ndani hasa ukizingatia ndicho chama chenye nguvu na kilichoshika serikali !! Ikumbukwe kwamba Rwanda imeweza kua inaingilia mambo ya ndani ya nchi majirani DRC,Burundi na hata Uganda nchi ambayo wamekua marafiki kwene mikatakti yao!!..Hapa chanzo cha mzozo ni ushiriki wa Tanzania katika kutokomeza m23 mwaka 2013,pia mzozo wa PK na kikwete Uliopelekea operation ya kuwafukuza wahamiji haramu Kigoma miaka ya nyuma (katafute jikumbushie)
-Lakini pia CCM inatazamwa kama chama chenye ushawishi kwa nchi za SADC na nchi majirani
TISS kama Taasisi imekua imara tangu kipindi cha Mwalimu ambapo miaka ya 60 Tanzania ilikua n nchi yenye nguvu na ushawishi mkubwa kusini mwa jangwa la sahara!!
Lakini pia imekuja kung’ara kipindi cha Mkapa
ambapo nchi ilikua inapitia baadhi ya sintofahamu ikiwepo vurugu 2001,Vugu vugu za kidini na vitu vya ivo!!
-Pia awamu ya tano Taasisi hii nyeti iliboreshwa kwa mishahara minono na kupewa kipau mbele sana!!
-Taasisi hii pia imefanya kazi kubwa kutoa taarifa za muhimu juu ya kundi la kigaidi lililotaka kuo mizizi KIBITI, na kufanikisha kulisambaratisha kama si kulipoteza kabisa ndani ya nchi
- TISS imeonekana na kazi kubwa sana hasa ukizingatia Raisi aliyekua madarakani ali waamini sana na kuwa tumia kupita kiasi ukilinganisha na mtangulizi wake!!
Inadhaniwa katika kipindi hiki TISS ilikua inapitia Transformation ya hali ya juu!! Hasa kutokana na utofauti ambao raisi na serikali ilikua ikiufanya!!
-Uongozi uliokuepo ulitofautiana na serikali zingine hivo kuwakana au kuwageuka wanasiaasa na wafanyabiashara waliokua na mizizi katika serikali kwa zaidi ya miaka kumi hivo kuongeza maadui wa serikali ya kipindi hicho!! hivyo TISS ilipewa mzigo mkubwa kwani maaduni wa utawala waliongezeka
-Pia inasadikika TISS iliactivate /kuanzisha kitengo cha intelligencia ya uchumi , ambapo walikua wakifanya intervertion juu ya Mipango ya kiuchumi ya nchi za kigeni juu ya nchi ya tz!! Hilo lilileta taswira tofauti hasa kipindi cha korona,Ukuta wa merelani,Bandari ya bagamoyo, pia walisaidia kuanza ujenzi wa bwawa la Mwl nyerere katka mto rufiji ambalo hata Mwl nyerere alikaliwa kooni na nchi za magharibi hivo kushindwa kulianza ( Ikumbukwe kwamba kazi ya intelligencia ni kukusanya taarifa na kuisaidia kufanya maamuzi sahihi) hivo hayo mambo yaliyotajwa ndio mchango wake
-Pia Taasisi hii nyeti ndiyo ilimuwezesha raisi wa kipindi hicho kuwez kujua kila kinachoendelea nje na ndani ya nchi!! Ikiwemo kila taasisi zote za tanzania!! Mtu atajiuliza Raisi alikua anajuaje makosa/Madudu kwene wizara fulani hasa ukizingatia alikua abafanya ziara za kushtukiza !!Hapa ndipo kinapokuja hiki kitengo kuwa effective kwene kupeleka taarifa zote
-Pia kitengo hiki ndicho kilikua muhimili na usalama wa kiongozi wa nchi hadi sasa!!
Kufeli!!…
-Ccm na tiss kufeli…..Ndiyo
-CCM haikua imejiandaa wala kujipanga kwa mabadiliko ya haraka kiasi hiki!!.Kama ilivo kawaida hatukuwai kupata dharula kama nchi iliyopata ya raisi kufia madarakani (failure ya kwanza hawakuliona likija)
Ila walielewa kua VP ndiye raisi mtarajiwa pindi ambapo raisi atafariki akiwa madarakani lakini hawakuona uwezekano au walipuuza sana hilo kutokea (Hili linajidhihirisha walivopigwa butwaa pindi msiba ulivotokea iliwachukua muda kujipanga na hawakupangika hadi leo wanafuana)
-Hivo kitendo cha Raisi kutoka ilihali yupo madarakani na hajamaliza muhula ilivuruga mipango yoooote iliyopangwa (Na tuwe wawazi huu haukua sehemu ya mpango wao nadhani)
TISS nao hawakuliona hili ( So pamoja na effective yao lakini hili liliwaponyoka na hapo tunasema Failure of intellince of Tiss)