Una maneno mengi sana lakini ni matupu. Strategic Vision 2025 ina malengo makuu matatu:
1. Maisha bora kwa kila mtanzania (Achieving quality and good life for all)
2. Kujenga mfumo bora wa utawala wa sheria (Good Governance and Rule of Law)
3. Kujenga uchumi imara ambao utaleta ushindani duniani (Building resilient and competitive economy globally)
Lengo la huu mkakati lilikuwa ni kuubadilisha uchumi wa Tanzania (Transformation and Modernisation). Sasa ukiangalia tangu Mzee Jakaya ni mangapi yamefanyika kuakisi huu mkakati utafahamu ni machache sana. Miaka 5 ya Raisi Magufuli, mamilioni ya watanzania wameingia kwenye lindi la umasikini na utawala bora ulisiginwa. Naomba katika hili tuache mzaha. Hayo malengo makuu matatu hayajatimizwa kwasababu ya siasa za hovyo za nchi hii....
Unaongea mambo mengi sana ya kusadikika, inaweza ikawa ni kweli. Lakini uhalisia mchungu ni kwamba sehemu yoyote iliyojaa rushwa kamwe hakuwezi kuwepo na usawa baina ya tabaka la juu na tabaka la chini. Haiwezekani, CCM is a GOLD-STANDARD OF CORRUPTION. Umewaongelea wakina majaliwa, hizo ni nafasi chache sana na za juu.
Ukija kwenye ngazi zenye watu wengi ambazo hazionekani ndiyo utaona uozo wa CCM. Hivi mtu kama Raisi Magufuli alivyokuwa anawachagua wakina Kabula ambao ni wanawake zake alikuwa ana maana gani labda. Kura za maoni alishindwa lakini akapita. Hivi leo unadhani kabisa mama yako mzazi akienda kugombea jimbo la mama Salma, hata kama kamshinda vigezo anaweza kupita ??? Hawa wakina Nape walipokuwa na vyeo walifanya juu chini hadi wakwe zao wapenyezwe..Tuna mengi ya kusema ila niishie hapa
Iko hivi, binafsi sina tatizo kabisa na watoto wa vigogo. Hata mkitaka kuwaweka ukoo mzima wa Samia waweke tu. I COULD CARE LESS. Tunachotaka sisi ni weredi na uwezo, leo hii watanzania ambao ni viongozi wana uwezo mdogo kwasababu ya michezo yenu ya kamlete. Mbali na hapo mmeiga michezo ya Warusi ya NOMENCLATURA, kwamba mnaweka makada hadi kwenye nafasi ambazo hawatakiwi kuwekwa wanasiasa......SHAME
Ndiyo viongozi wengi waandamizi wa Tanzania (TOP-BRASS) ni watu wasiokuwa na uwezo. Kama unabisha leo hii omba uone PhD za hao vijana wenzenu Jafo na Dotto, au hata ili ya marehemu iliyofichwa. Lakini kuwa zaidi, akili ya mtu hatuipimi kwenye shule peke yake, tungaalia mambo mengi.
Akili ya viongozi inapimwa kwa kuangalia maamuzi yenye maslahi mapana ya taifa kwa muda mrefu (How often does a leader make correct and accurate decision affecting a large margin of a population). Sasa ukijiuliza kwanini wizara ilifanya maamuzi ya ajabu kama kufuta masomo ya kilimo, kuunganisha somo la fizikia/kemia na Raisi kusaini mikataba ya hovyo ya madini na kudiriki kabisa kutetea haya maamuzi, utapata picha nchi hii ina viongozi aina gani.
Tanzania iko kwenye Crisis. AU mwenzangu Crisis ni mpaka uone machafuko kama Rwanda na Kenya ???
No, No, No! This type of thinking is myopic, bismal, parochial and lackadaisical. Tanzania kuna tatizo la rushwa na ufisadi. Mfumo wetu wa elimu umevurugika, watoto wanaanza kidato cha kwanza hawajui kusoma na kuandika lakini walifaulu mtihani, kuna tatizo kubwa sana la ajira, kuna tatizo la mabadiliko ya hali ya nchi. Can't you see that these are national Crises ???
Tafadhali sana, usinilisha maneno.....
Suala siyo kuwa na chama, hata chama cha KINAZI cha Adolf Hitler kilikuwa na nguvu sana na taasisi imara. Lakini swali la msingi mno kujiuliza ni kwamba chama kinaifanyia nini nchi. Mfumo wa chama mliouiga kule Urusi ulifikirika kwamba ndiyo bora kabisa duniani, lakini baada ya miaka 88 nchi ikaangukia pua. Chama kilikuwa na nguvu kweli, lakini kilijaa rushwa, upendeleo na uhafidhina. Ndiyo CCM ni chama chenye nguvu nchini, hili halina ubishi.
Lakini tukiuliza kama CCM kinaisaidia nchi, hili ni swala ambalo wengi mtamung'unya maneno bila kutoa majibu yaliyonyooka.....