Je, CCM na TISS wanakuzwa nguvu zao kuliko uhalisia (Overrated)?

JPM alisema chanjo haifai ila SSH kasema ni muhimu tuchanjwe afu kuna wana CCM wanashangaa hizi U turn!! Je kivp wanaduwaa wakati CCM ndio ilimuandaa kuwa Rais?? Au mnakiri kuwa hakuandaliwa kma mnavyojisifiaga!!
Kuandaliwa hakumaanishi ukubaliane na mtangulizi hata kama ni ya kijinga.
Lazima achukue yale mazuri na yale ya kipuuzi aache nchi isonge mbele.
Kumbuka kwamba kila binadamu ana mapungufu yake ambayo hutofautiana na wengine.
Hivyo SSH kutofautiana na JPM hakuna la ajabu, na ni uthibitisho kuwa aliandaliwa fika.
Asiyeandaliwa angefuata ya mtangulizi wake tu.
 
Tatizo ni fikra kwamba mtu akiwa na vyeti basi ana uwezo wa kiakili.
Hujaona professor mpuuzi kabisa akikufundisha? Utavumilia mambo yaende.
Vyeti ni kitu kimoja na akili ni kingine.
Kwa sababu jamii inathamini vyeti bila akili ya kawaida, na kwa kuwa wanasiasa ni wapenda sifa na kuenenda na mawimbi, lazima watafute vyeti kwa gharama yoyote.
 
1. Ingekuwa CCM haijui kuandaaa na kuendeleza viongozi isingedumu tangu 1977
2. Ingekuwa TISS ni dhaifu kama unavyodhani isingeweza kuimarisha tunu za Taifa kwa miaka 60 sasa.

kwa ufupi hizi taasisi zote mbili zimefanya kazi kubwa ya kuimarisha ustawi wa nchi yetu.
 
Tatizo ni fikra kwamba mtu akiwa na vyeti basi ana uwezo wa kiakili.
Hujaona professor mpuuzi kabisa akikufundisha? Utavumilia mambo yaende.
Vyeti ni kitu kimoja na akili ni kingine.
Hakuna sehemu duniani ambako yaliwahi kupatikana maendeleo na mapinduzi ya fikra bila wasomi.
Tutabishana usiku kucha kuhusu hili, lakini ukweli ndiyo uko hivyo: Wasomi hujenga jamii.
Kama kuna sehemu unaifahamu ambako kumeendelea bila wasomi nitajie....
 
... mfano Jiwe!
 
Sijaandika kuwa kuna maendeleo bila wasomi na hilo haliwezekani.
Kuna wasomi na wenye vyeti wasio wasomi (wasomi fake).
 
Stigler Gorge investment ya kupata 2000 plus MW ni USD 5 to 7 billion
thanks PhD for taking ur time to comment on the thread however I would like to object few things.

Kwanini umeangalia gharama tu mfano tukiangalia gharama huoni SGR ni bei kuliko conventional railways? Kma issue ni initial investment ina maana tubaki na reli ya kati na Tazara coz ni cheaper na tusiangalie ufanisi ama long term sustainability?? Mfano kina cha maji kikipungua ile hasara ya mgao uki calculate vis a vis realiable gas supply huoni hyo cheap itakua expensive cumulatively?

Kingine unaposema gesi sio yetu una maana gani?? Kwani concession agreements haitupi sisi mgao wetu pamoja na 16% Free-carried interest (Correct me kama haipo applicable kwa sheria ya mapato ya mafuta na gesi 2015 na amendment zake)? Mbona hta dhahabu ama Tanzanite sio za kwetu ila tunapata stahiki zetu (kodi na spillover effects zingine) ambazo tusingepata kama tungesubiri tupate mtaji wa kuchimba wenyewe!!? Tunapata hasara gani? In fact tumeanzisha sovereign wealth fund kumanage pesa za gesi huoni hyo faida yake in long run?

NB; Kingine TPDC kuna maeneo imeanza kufanya exploration wenyewe na kuchimba wenyewe so hya pia yanatupeleka in the right direction hta kma ni pilot projects tu

Faida ya moja kwa moja ingekuwa umeme tuu
Mbona mpango ulikua gesi ifike majumbani kma nishati mbadala hta kupikia so tungenunua kwa bei nafuu? Hyo recuperated cost ingetumika na raia kwa vitu vingine
na ni mali yetu sio undeleze kitu cha mwenzako kwa kukimbilia kuvizia kodi tuu.
Na ndio kiini cha mada sasa, kama CCM walijua gesi sio dili why watu set kuwa tunaeleka uchumi wa gesi afu ghafla mnakuja kugeuka alipoingia JPM na kudai HEP ndio way to go? Huoni inaonyesha hakuna consensus na continuity ndani ya CCM about the approach to crucial policy initiatives? And if that's the case je ile jeuri kuwa CCM ni makini katika kumanage transitions za serikali inakua rendered obsolete!
 
Sasa kama taasisi ndio inaandaa inakuaje inaruhusu viongozi wanaotofautiana kufuatana!! Yaani kma sera ya CCM ni kwamba watoto waliopata mimba warudi shule kivp anaingia mtu anasema hapana warudi shule then 2025 akiingia mwingine utaskia wajawazito hawaruhusiwi kurudi shule!! Hyo chaos ndio naongelea hapa maana inatucost sana wananchi.

Fikiria CCM walisema muswada wa mapato na gesi ulikua sahihi, anaingia JPM anasema ni wa kifisadi, ghafla tena akiingia SSH naye anaona shida tofauti. Sasa unajiuliza mbona chama ni kile kile na baadhi ya watendaji/watafiti/washauri ni wale wale je wanakwama wapi kuandaa succession management inayorandana na maazimio ya chama??

Hivi CCM si chama cha kijamaa? Nitajie mjamaa mmoja tu CCM yaani anayefuata zile principles za marxism!! Nitajie mmoja tu alafu utaona hoja yangu inapoanzia!!
 
Naongelea consistency sio uwezo wa kukaa madarakani, maana hta ZANU PF inatawala zimbabwe tokea uhuru ila nchi inazidi kudidimia tu!!! Sasa utawasifia kwa kubaki madarakani tu au unaangalia output?

Mfano kilimo kwanza yaliwekezwa mabilion ghafla tena bajeti ya kilimo kipindi cha JPM zikawa below 20% ya allocated development expenditure!!! Tutafika kweli kma hatuwezi kuanzisha jambo tukalisimamia mpka mwisho maana CCM si ile ile? Ssa inakwama wapi
 
CCM ilitanguliza tu ya kuwa na Makamu wa Rais mwanamke ,haikujiandaa kufiwa ilijua inamiliki kifo inamiliki ugonjwa.
Yametokea yaliyotokea TISS ipo kwa ajili ya kuendeshwa na CCM,unakuta wakati wa uchaguzi wa maoni wanaanza kufanya screening ya nani ni bora huko CCM badala ya nani anakubalika na wananchi huko mtaani kupitia vyama vingine.
 
Kama angekuwepo suitable replacement nadhani ingewezekana kumshauri huyu Mama ajiuzulu.
 
TISS hawana issue kabisa ni kitengo kimojawapo cha chama tawala wanaendeshwa kama gari bovu.Shughuli zao za kila siku wameweka kando kutwa kufatilia vyama vya upinzani tu.
 

Sio kwamba Magufuli aliifanya iwe na nguvu ya kisiasa, bali alitumia kiburi chake cha madaraka kuifanya CCM itambe. Kimsingi wakati wake CCM haikutamba kisiasa,bali ilitambia nguvu ya dola na kundi la watu wasiojulikana lililokuwa linamilikiwa na CCM. Usitake kupotosha kuwa Magufuli aliipandisha CCM, wakati hata kwenye chaguzi tulikuwa tunaona mabox ya kura yakiletwa kwenye vyumba vya kura, mbele ya polisi na tume ya uchaguzi.
 
Mkuu kesi ya Mbowe ambayo imezaa udhalilishaji wa makomando wastaafu na jeshi la polisi na taifa kwa ujumla ni ushahidi kuwa TISS na kamati kuu ya ccm ni MABOGUS sana!!!Leo tunachafuka kizembe kisa upumbavu wa wachache ndani ya nchi!!SAMIA HAKUJIANDAA kama Raisi asingeenda kusema BBC eti Mbowe ni Gaidi wakati shauri lipo Mahakamani!!JESHI LETU LIMEDHALILIKA KWA KUIONYESHA DUNIA ETI LIMETOA MAFUNZO YA KIGAIDI KWA MAKOMANDO WAKE!ETI MAFUNZO YA KIJESHI HAPA NCHINI YANAANDAA MAKOMANDO MAGAIDI!!!TISS na CCM wameonyesha Upumbavu wao wa kiakili tena wazi kabisa !!Nashangaa Diwani Athumani hajiuzulu kwa kutia aibu Taifa letu na nchi Ujumla!!Halafu NA ILE FILAMU YA UTALII YA SAMIA ILIKUWA YA NINI WAKATI UMESHATANGAZIA DUNIA KUWA MBOWE NA MAKOMANDO WASTAAFU WA JESHI ETI NI MAGAIDI??
 
Wale makomando sio kabisa.wanajitetea eti walipigwa hadi wakalia mwingine sijui luteni urio nae alionekana akilia baada ya kupokea kichapo cha nguvu kituo cha polisi Tazara.
 
Mkuu kwani ccm ndio chama pekee nchini?Huyo jpm angeandaliwa kwa kwenda NccR akashinda nchi ingekufa kibudu??Fikra mgando za Tiss ndio hizi za kuipigania ccm wakati tuna vyama vingi hapa nchini!kama Lowasa aliiteka ccm 2015 kwanini wasingeiandaa Chadema ya jpm akashinda Uraisi na hapo nchi ikaheshimika kimataifa?kuliko kuua watu na kuwabambikia kesi ili ccm iwe hai??UPUMBAVU UMEZIDI SIO KWA TISS TU HATA DEEP STATE YETU UJINGA UMETAMALAKI!!!KIFUPI NI HAYO TU!!
 
Binafsi nilishangaa sana na ninaendelea kushangaa, mbibi anayedate vijana wadogo tena wenye sifa za kishenzi kama Bashite anakuwaje Rais?

Akina polepole wana haki ya kulalamika na kumdharau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…