Je, Cheti cha ndoa kimetajwa popote kwenye biblia au Quran?

Je, Cheti cha ndoa kimetajwa popote kwenye biblia au Quran?

cheti sio cha dini wewe, ni cha serikali, hata ukifunga kimila kitasajiliwa na serikali, labda dini ya kiislam wanavyo vyao na hupeleka serikalini kopi kusajiliwa
Eheee mkuu hapo kwenye kimila huwa inakuaje mpaka kinasajiliwa kiserikali?
 
Sijui kwa waislamu. Lakini biblia haijataja.

Wakristo wanatoa cheti kwa kutii matakwa ya kiserikali, na vyeti hivyo wanavichukua serikalini. Hawatengenezi wao.
vya waislam wanaviita shahada kuipata ni elfu hamsini na kwa wakristo wanaviita vyeti hivyo hivyo kuipata ni elfu ishirini kwa sasa. Hivyo vyeti vinatoka serikalini
 
Ukifunga ndoa Kanisani au msikitini bila cheti, hiyo ndoa ni halali kidini?

Serikali ikiamuru makanisa na misikiti yaweke sanamu la shetani kwenye nyumba za ibada, watatii?
Duh akili kisoda muda mwingine sio lazima kuleta uzi kama huu wakati ungeenda kuongea na viongozi wa dini wangekupa majibu. Akili ndogo sana asee
 
Kilichotajwa katika Biblia ni Posa / Mahari...na hata Manabii walitoa mahari wakati wa kuoa kama Musa, Yakobo n.k

Suala la Cheti cha ndoa, Pete, Sherehe za harusi, Wadhamini n.k ni mambo yaliyokuja baadae kwa mipango ya Binadamu tu
 
Back
Top Bottom