Je, dakika yake ya mwisho duniani alisemaje? Ilikuwaje?

Pole sana mkuu nyakati hizi ngumu huja na kupita.
 
Kuna mtu huko juu amenishauri niandike kisa changu ilikuwa 2019 august asubuhi siku ya ijumaa kuamkia jmosi. Saa tisa alfajiri niliota mtoto wangu wa kiume alikuwa analia mgongoni kwa mama yake. Sasa mimi nikamfokea kidogo kwamba anyamaze nikamshika mguu wake kumtingisha nikamwambia J acha kulia usiku sahizi wakati huo mimi nipo ndani ya chandarua na wao wamesimama nje ya kitanda na mama yake wanabembelezana. Huwezi amini kitendo cha kumuambia mwanangu J acha kelele basi eti akamfia mama yake mgongoni.

Nikastuka usingizini kwa hii ndoto mbaya sasa nikawa najiuliza inamaana nimemuua mwanangu? Nikajiskia vibaya sana baada usingizi ukanipitia tena nikalala. Kwenye saa 12 asubuhi napokea simu njoo haraka nyumbani umpeleke baba hospital. Ni umbali wa km 90 toka ninapofanyia kazi mpaka kwa mzee. Asubuhi hiyo hiyo nikajiandaa fasta huku moto mzito sana hasa nikiwaza ile ndoto.

Nafika umbali wa kama mita mia naona geti la nyumbani limefunguliwa na kuna watu nje. Nikastuka sana .Mama mzazi alikuwa jasiri sana (ila pia walishatengana na mzee kitambo) mama mzazi akaniwahi getini akanishika mkono akaniambia jikaze. Nikajua nimeshampoteza baba. Kufika chumbani kwake nikamkuta baba amelala kimya. Na wamemfunika kanga. Katika maisha yangu juu ulikuwa wakati mgumu kuliko yote toka nizaliwe!

Kukidhi matakwa ya uzi huu. Nikwamba niliongea nae kwenye simu two days before! Had I known that could be the last moments talking to my father I could have recorded his voice! We Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema naomba uendelee kumpatia baba yangu mzazi pumziko lenye amani ya milele. Amin.
 
Yuda iskariot kesho ndo siku rasmi ya usaliti, utatuambia Yesu alisema nini pale msalabani dakika za mwisho
 
Mi ndo natembea hivyo, changamkeni basi mik#nd# nyie nileteeni maziwa ya pakti hapa.

So sad[emoji24][emoji24]
 
Pole sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"https://jamii.app/JFUserGuide you! " maneno ya mwisho ya 2pac. Inasemekana ni baada ya nesi Wa kizungu kumuendea kitandani kwake akiwa hospitali na kumuuliza anajisikiaje!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kiongozi
 
Wanapenda sana kuomba maji ya kunywa...au kama alikuwa hoi kuinuka ghafla na kupiga stori akirudi kulala ndo imetoka hiyo.Mi baba alikufa anacheka ilikuwa kaz sana kuufumba mdogo alivyokata moto
 
Alituita watoto wake wote wa 3 akatupa mikono kwa tabu Sana akatuambia vitu vyangu vyote mnavijua chochote watakacho watakachosema ni Chao waachieni.kisha akamwambia brother wasimamie wadogo zako huku machozi yanamtoka.tukatolewa nje mshua alikufa kifo Cha maumivu Sana Mana akijua anatuacha kwenye mikono ya wadharimu watu wabaya tukiwa Bado wadogo Sana.
Na kweli kwenye nyumba 9 alizoziacha tumebakiwa na mbili tu.
Kwenye hekari 22 vikindu 1994.tumebakiwa na eneo iliyopita njia kuu.
Kila kitu chake waligawana ndugu zake kwa kweli maneno yake yalitimia.mshua pumzika kwa amani ulitabili ukifa tutapata tabu Sana na kweli walitunyoosha pa moja na wema wako wote ule waliyotutendea tumemuachia MUNGU.tumesahau now tunafuraha Tuna maisha yetu tunakukumbuka daima....
 
Pole Sana,be strong
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…