Je, dakika yake ya mwisho duniani alisemaje? Ilikuwaje?

Pole Sanaa,vipi mama hakuwepo? Nafurahi kuwa umeshakuwa mkubwa
 
Mie alinibusu mara ya mwisho kumbe alikuwa anaenda kuolewa na mwingine[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
[emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ila ndugu, imagine mnazaliwa na kukua pamoja toka utotoni hadi utu uzima. Unaanzisha familia wanaiona ila ukifariki wanadhulumu kila kitu. Siwezi patia picha huzuni ya mzee wako

Pole sana mkuu
 
Ila ndugu, imagine mnazaliwa na kukua pamoja toka utotoni hadi utu uzima. Unaanzisha familia wanaiona ila ukifariki wanadhulumu kila kitu. Siwezi patia picha huzuni ya mzee wako

Pole sana mkuu
Kaka acha tu.
Kuna maisha inatakiwa usimuliwe tu.jambo jema ni kwamba mzee alitufundisha kusameh na kusahau ki ukweli tukikutana nao wanakosa amani Sana 😁😁😁😁mpaka tunashindwa kwenda kuwatembelea Mana tunahisi wanajutia ila ndio hivyo ni watuwazima hawezi omba radhi.
 
Pole Sanaa,vipi mama hakuwepo? Nafurahi kuwa umeshakuwa mkubwa
Mama alishika 50 zake alituacha na baba yetu,yule mzee alipambana Sana alikuwa baba alikuwa ni mama pia.
Embu vuta picha alikuwa ni afsa wa police mkubwa Sana kavuka Revo zote za nyota kipindi hicho tunaishi urafiki maghorofani pamoja na ubize wake alikuwa anahakikisha wote tumekunywa chai tunaenda shule mchana tukiludi msosi upo mezani,sijui alikuwa anapika sa ngapi,alikuwa ananifulia Mimi na kaka yangu wa pili ila wa kwanza alikuwa la 7 kwahiyo alikuwa anajiweza.
Hakuoa,hakuwahi kutuonesha ujinga,alikuwa mtu wa watu,BABA yangu anasifa nyingi za kuwa baba Bora zaidi.
Alikuwa anasumbuliwa na Kansa hakuwahi kutuambia 😔😔😔😔 so sad alikuwa akiingia kuoga analilia bafuni watoto wake tusione maumivu yake wala machozi yake.
Mama yupo zake huko na maisha yake,simchukii mother RIP nampenda pia sijui ugomvi wao ila nilipokuwa nilionao walichagua kuwa na amani.
 

Nakuelewa mkuu tena ni kheri nyie mzee, wenu alikuwa na mali nyingi wakatapata vya kuwaachia, kuna manzi mmoja nilikuwa nae close kipindi nasoma

Huyo baba yake alikuwa mwanajeshi, alivyofariki Tu ndugu wakagawana kila kitu yaani hadi watoto, mama yao baada ya kuona watoto wake wametenganishwa huku wanateseka akaona bora awachukue awalee kwa huruma ya Mungu

Huo umaskini aliokuwa anauishi yule binti ilibidi toka O 'level ajifunze kutafuta pesa hivyo kuna vipindi hafiki shule hata wiki

Ila Mungu kamsaidia saa hii kidogo manisha yamemnyookea
 
Duh pole yake kwa Mtoto wa kike.
Hata Mimi nilipitia hiyo Hali nilianza kujitegemea la 4.maana brother alifaulu akapelekwa shule sumbawanga huko ikabidi Mimi na kaka yangu twende kwa mama mkoani ndani ndani huko na mama anaishi kwa vibarua kulima mashamba kwahiyo ikawa ni mwendo wa kushika jembe tu
Ikawa siku ambayo TREN la abiria linapita mi na kaka angu tunaenda kubeba mizigo ya wafanya biashara
Kuisaidia kugema ulanzi,kukamua komoni,kukamua kiambule.yani vulugu vulugu tu maisha ya kuonewa kwa asilimia 💯.

Now ni history tu nadhani Kuna nyakati tunazipitia ili kutuomarisha na kutukumbuaha zaidi.
Sina kitu ila Kila nikipata nawakumbuka wenye mahitaji maalumu sifungi vioo kioo changu kipo wazi naruhusu atakaye kuja dirishani nimpatie kidogo akale na aliyemtuma.
 
Duuuu,Mungu aliwapa mzee Bora sana
 
Bibi yangu alisema " Kuna watu wamevaa nguo nyeupe walikuja kunichukua, nashangaa wameondoka wameniacha"..huku akionyesha dalili zote kuwa alikuwa anahamu aondoke na hao waliokuja kumchukua. Baadae kidogo akalala milele
 
Na kweli mkuu imekuimarisha na imekufanya kujua ni nini maana ya maisha. Ukiona mtu kakosa unaelewa anajihisi vipi

Mungu akubariki brother
 
Bibi yangu alisema " Kuna watu wamevaa nguo nyeupe walikuja kunichukua, nashangaa wameondoka wameniacha"..huku akionyesha dalili zote kuwa alikuwa anahamu aondoke na hao waliokuja kumchukua. Baadae kidogo akalala milele
Duh!!!,hamkumuuliza jinsi watu hao walivyo??, Matharani je,Wana mabawa?.
 
Je, maisha yenu ya sasa ni mazuri? I mean ni standard?
 
Mmmh yaani alikuwa anaumwa kiasi cha kutoa machozi akiingia bafuni! So sad! Cancer ya nini? Hiyo cancer i hope si ya kawaida ilikuwa ni ya kutupiwa.
 
Safi, unamaanisha hujaweka geti nyumbani kwako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…