Mama alishika 50 zake alituacha na baba yetu,yule mzee alipambana Sana alikuwa baba alikuwa ni mama pia.
Embu vuta picha alikuwa ni afsa wa police mkubwa Sana kavuka Revo zote za nyota kipindi hicho tunaishi urafiki maghorofani pamoja na ubize wake alikuwa anahakikisha wote tumekunywa chai tunaenda shule mchana tukiludi msosi upo mezani,sijui alikuwa anapika sa ngapi,alikuwa ananifulia Mimi na kaka yangu wa pili ila wa kwanza alikuwa la 7 kwahiyo alikuwa anajiweza.
Hakuoa,hakuwahi kutuonesha ujinga,alikuwa mtu wa watu,BABA yangu anasifa nyingi za kuwa baba Bora zaidi.
Alikuwa anasumbuliwa na Kansa hakuwahi kutuambia [emoji17][emoji17][emoji17][emoji17] so sad alikuwa akiingia kuoga analilia bafuni watoto wake tusione maumivu yake wala machozi yake.
Mama yupo zake huko na maisha yake,simchukii mother RIP nampenda pia sijui ugomvi wao ila nilipokuwa nilionao walichagua kuwa na amani.