Watu wanaamini ukweli wa uwepo wa Mungu kwakuwa Kuna maswali hata ya Kisayansi ambayo hayajibiki hadi sasa.
Pia Kuna majanga ambayo yakitokea Binadamu ameshindwa kuyadhibiti hivyo kumzidi uwezo wake wa mwili na akili.
Mfano ni kweli Jua lipo na linatupa mwangaza na virutubisho vya uhai.
Je ikitokea Jua limepoteza nguvu zake yaani limeharibika ni Binadamu gani ataweza kulikarabati lirudishe uwezo wake ?
Ni kwamba hayupo, hata waungane Wana sayansi wote hawataweza.
Ndio hapo tunajiuliza, ni nani alilitengeneza Jua (hakuna jibu)
Na Tunaona umuhimu wa Jua katika maisha yetu.
Ni kwamba yuko Mtaalamu aliye tukuka sana, aliweka mfumo wa Jua ili kustawisha uhai wa viumbe vya ulimwengu na akalipanga kuongoza Solar System kwa umahili uliotukuka kabisa.
Pamoja na uzito mkubwa wa Solar System yaani Jua na Sayari zake lakini wanasayansi wanakiri kuwa hiyo System inaelea tu na haishikiriwi na nguzo au mihimili yoyote.
Vipi Solar System ikipoteza mwendo wake na Sayari zake kuporomoka, ni nani atazirekebisha.
Kutokana na hali hiyo Binadamu akapata uhakika kabisa kuwa kuna Mtukufu ndiye aliye pangilia hayo mambo yaliyo nje ya uwezo wa Binadamu.
Hivyo ili kubaki salama ni heshima kubwa kumheshimu huyo Mtukufu.
Na kwakuwa ni Mtukufu basi bila shaka anauwezo wa kusikia lugha yoyote ya Mwanadamu.
Ndio maana kila Kabila la watu hapa duniani hata Yale ambayo yapo Bado kwenje mfumo wa Ujima, wanaamini kuna pasi na shaka kuwa kuna Mtukufu anayestawisha maisha yao.
Na utawakuta Wana Imani ya Dini na kuongea na Mtukufu kwa Sala au Dua au Maombi kwa heshima na unyenyekevu wa kutosha kabisa wengine hadi wanalia kwa maombi yao mazito.
Sasa kama Wanasayansi waliobobea kwa maarifa ya Sayansi na kuthibitisha kuwa Mtukufu Yupo kutokana na wanavyo yathibisha Kisayansi.
Na pia Jamii za Kijima ambazo tuna amini kuwa hawana Upeo mkubwa wa kimaarifa nao pia wanathibitisha Mtukufu Yupo
Wewe unani ubishe ?
Huo ndio ustaarabu wa kuthamini kazi nzito sana alizozifanya Mtukufu yaani Mungu.
Hii leo kila jamii unamjua Mungu Mwenye Enzi. Na wanamwabudu kwa mitindo mbali mbali.
Hapa itambulike kuwa kuna maswali mengi ya Kisansi ambayo Hadi hii leo hayajapatiwa majibu.
Vipi wewe utake kupata jibu la huyo Mtukufu
anaishi wapi ?
anakula nini ?
Alitokea wapi ?
Nithibitishie kama Yupo
Kwani Jua unaloliona kwa macho yako
limetokea wapi ?
linafanyiwa service na nani?
kwa materia gani ?
Hivyo basi kwa Binadamu yeyote yule aliye timamu ki afya na akili.
Anatambua bila chembe ya shaka kuwa Yupo Mtukufu na anastahili kupewa heshima kubwa.
Yupo Mungu aliye umba Mbingu na Nchi na vyote viujazavyo, na kuvistawisha.
Zaburi (Psa) 14:1
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
The fool hath said in his heart, There is no God. They are corrupt, they have done abominable works, there is none that doeth good.
Asante
Venus Star, kwa uchambuzi mzuri kabisa.