Je, dini inaweza kukupeleka kwa Mungu?

Unaleta maswali ambayo unasema ni ya kiimani halafu unataka majibu ya kisayansi,

Unaleta imani kwenye sayansi inayo hitaji uthibitisho, uhakiki na ushahidi,

Huoni unachanganya mambo?
 
Reactions: 511
Nina swali mkuu, hivi shetani aliumbwa na Nani???

Swali la pili
Kwenye dini zote zinasema Mungu/Allah ni mjuzi wa Kila kitu anajua yaliyopita, yaliyopo na yajayo,

Pia Mungu anajua kila kitu kabla hata hajaniumba nitakachofanya duniani na siku nitakayokufa na kitu kitakachoniua na nikifa anajua kama nitaenda motoni au peponi

Sasa kama Mungu kaniumba nikafanya dhambi hapa duniani na nikafariki klnikiwa kwenye dhambi nikaenda motoni
Je nikisoma Mungu kaniumba ili niende motoni akinichome Moto nitakuwa nakosea????, ( kumbuka Mungu alikuwa anajua kila kitu hata kabla hajaniumba)
 
Dini ni nia ya mwanadamu kumtafuta Mungu, it is man made.

Wokovu ni njia ya Mungu kumtafuta mwanadamu kupitia Yesu Kristo.

Yesu ndie njia kweli na uzima, no other way.

Wengi wetu tumekuwa watumwa wa dini, tunzipenda kuliko kumpenda Mungu.

Yesu anasema, "Mkinipenda mtazishika amri zangu." Yohana 14:15
 
Umeandika
Maneno meeengi kumbe pumba tupu huna hojaaaa
 
Reactions: 511
Hapo kwenye shida ni baada ya kuasi eden aitoa adhabu kwa tutaishi kwa jasho.
 
Ungesoma kile nilichokiandika awali ungefuatilia comments zangu.


From Venus Star: God is anything which is beyond of your intelligent abilities. Mungu ni kitu chochote kilicho juu ya uwezo wako wa akili

Mtoto wangu mchanga ananiona mimi ni Mungu
Mungu ni concept iliyotokana na curiosity ya watu kutaka kujibu philosophical issues kuhusu existence.

It vary according to culture
 
😂😂😂
Mbona umeingiza swaga za mashahidi wa Jehovah ukaja ukaingiza na mambo ya mpira???
Pole Dada haya mambo ukiyafuatilia sana unakuwa kichaa. Ishi kwenye kusudi lako tu.
😂muache kutuwekea mipaka na huyo bwana mwenyezi wenu tuenjoy dunia bn hakuna sehemu yeyote utaeza ona jua mateso furaha ukweli au ungo nje na hapa duniani ninyi kazi mlioichagua ni kumtetea na kumpia promo muweza wa yote asiejiweza yeye kwanini?
 
Dini ni nia ya mwanadamu kumtafuta Mungu, it is man made.
Huyo Mungu anatafutwa kwani amepotea?
Wokovu ni njia ya Mungu kumtafuta mwanadamu kupitia Yesu Kristo.
Huyo Mungu anatafuta wanadamu kwani hawajui na kawasahau?
Yesu ndie njia kweli na uzima, no other way.
Muislamu akikwambia Muhammad ndiye njia ya kweli na uzima, no other way, Utakubali tu kwa vile umeambiwa hivyo?
Wengi wetu tumekuwa watumwa wa dini, tunzipenda kuliko kumpenda Mungu.
Huyo Mungu Alishindwaje kuumba binadamu watakao mpenda?
Yesu anasema, "Mkinipenda mtazishika amri zangu." Yohana 14:15
Huyo Yesu anataka apendwe kwani yeye amekuwa demu?
 
Usilazimishe watu waamini au wafikirie kama wewe. Waache watu waishi watakavyo. Tunajaribu kukufundisha ustaarabu, umekaza fuvu
 
Usilazimishe watu waamini au wafikirie kama wewe. Waache watu waishi watakavyo. Tunajaribu kukufundisha ustaarabu, umekaza fuvu
Unajaribu kunifundisha ustaarabu wewe kama nani?

Ustaarabu kamfunze mamako.

Kuna sehemu nimelazimisha mtu aniamini?

Nimeshika maisha ya watu niwazuie wasiishi?

Hakuna aliye lazimishwa kuwa hapa JF, Ukiona hupendezwi na maoni yangu au maoni ya mtu yeyote yule, Jamii forums imekupa option yaku ignore.

Otherwise kila mtu yuko huru kuchangia maoni na mawazo yake hapa JF.
 
Unaandika too manya words. Unaandika uozo.🤮🤮🤮
 
Nyie mlikua mazombi msio weza kufikiri wala kuhoji na ni wakengeufu mlio kana imani za asili za wazee wetu,hatuwaamini wala kuwasikiliza we follow our own path now relax.
 
Nyie mlikua mazombi msio weza kufikiri wala kuhoji na ni wakengeufu mlio kana imani za asili za wazee wetu,hatuwaamini wala kuwasikiliza we follow our own path now relax.
Wewe mbombo ngafu
mara leo hii ulilala kifudifudi , unaota ` unabarikiwa na baba mtakatifu wa vatikani na kuwashangalia mashoga wa TEC
Kesho unajifanya obi okwonkwo
 
Jifunze kuweka paragraphs,kumbe mungu si mtu wa mchezo mchezo je ni ke au me?
 
Watu wanaamini ukweli wa uwepo wa Mungu kwakuwa Kuna maswali hata ya Kisayansi ambayo hayajibiki hadi sasa.

Pia Kuna majanga ambayo yakitokea Binadamu ameshindwa kuyadhibiti hivyo kumzidi uwezo wake wa mwili na akili.
Mfano ni kweli Jua lipo na linatupa mwangaza na virutubisho vya uhai.

Je ikitokea Jua limepoteza nguvu zake yaani limeharibika ni Binadamu gani ataweza kulikarabati lirudishe uwezo wake ?
Ni kwamba hayupo, hata waungane Wana sayansi wote hawataweza.

Ndio hapo tunajiuliza, ni nani alilitengeneza Jua (hakuna jibu)
Na Tunaona umuhimu wa Jua katika maisha yetu.
Ni kwamba yuko Mtaalamu aliye tukuka sana, aliweka mfumo wa Jua ili kustawisha uhai wa viumbe vya ulimwengu na akalipanga kuongoza Solar System kwa umahili uliotukuka kabisa.

Pamoja na uzito mkubwa wa Solar System yaani Jua na Sayari zake lakini wanasayansi wanakiri kuwa hiyo System inaelea tu na haishikiriwi na nguzo au mihimili yoyote.

Vipi Solar System ikipoteza mwendo wake na Sayari zake kuporomoka, ni nani atazirekebisha.

Kutokana na hali hiyo Binadamu akapata uhakika kabisa kuwa kuna Mtukufu ndiye aliye pangilia hayo mambo yaliyo nje ya uwezo wa Binadamu.

Hivyo ili kubaki salama ni heshima kubwa kumheshimu huyo Mtukufu.

Na kwakuwa ni Mtukufu basi bila shaka anauwezo wa kusikia lugha yoyote ya Mwanadamu.

Ndio maana kila Kabila la watu hapa duniani hata Yale ambayo yapo Bado kwenje mfumo wa Ujima, wanaamini kuna pasi na shaka kuwa kuna Mtukufu anayestawisha maisha yao.
Na utawakuta Wana Imani ya Dini na kuongea na Mtukufu kwa Sala au Dua au Maombi kwa heshima na unyenyekevu wa kutosha kabisa wengine hadi wanalia kwa maombi yao mazito.

Sasa kama Wanasayansi waliobobea kwa maarifa ya Sayansi na kuthibitisha kuwa Mtukufu Yupo kutokana na wanavyo yathibisha Kisayansi.

Na pia Jamii za Kijima ambazo tuna amini kuwa hawana Upeo mkubwa wa kimaarifa nao pia wanathibitisha Mtukufu Yupo

Wewe unani ubishe ?
Huo ndio ustaarabu wa kuthamini kazi nzito sana alizozifanya Mtukufu yaani Mungu.

Hii leo kila jamii unamjua Mungu Mwenye Enzi. Na wanamwabudu kwa mitindo mbali mbali.

Hapa itambulike kuwa kuna maswali mengi ya Kisansi ambayo Hadi hii leo hayajapatiwa majibu.

Vipi wewe utake kupata jibu la huyo Mtukufu
anaishi wapi ?
anakula nini ?
Alitokea wapi ?
Nithibitishie kama Yupo

Kwani Jua unaloliona kwa macho yako
limetokea wapi ?
linafanyiwa service na nani?
kwa materia gani ?

Hivyo basi kwa Binadamu yeyote yule aliye timamu ki afya na akili.
Anatambua bila chembe ya shaka kuwa Yupo Mtukufu na anastahili kupewa heshima kubwa.

Yupo Mungu aliye umba Mbingu na Nchi na vyote viujazavyo, na kuvistawisha.

Zaburi (Psa) 14:1
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

The fool hath said in his heart, There is no God. They are corrupt, they have done abominable works, there is none that doeth good.

Asante Venus Star, kwa uchambuzi mzuri kabisa.
 
Mungu bila elimu ?

hebu tuambie what is the purpose of life ??
Mtaalamu Jagina, Naona uko vizuri kwenye maswala ya Kifilosofia.
Samahani Mheshimiwa watu humu jamvini wanakuuliza wewe ni ME au KE.
Maana jina lako ni la kike lakini maneno yako ni ya kiume.
Wanasubiri jibu wajiridhishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…