Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 1,710
- 8,690
Kwanza ahsante kwa kunitia moyo.Binafsi nakupongeza na kukutia moyo kuwa pambana tulinde maadili yetu Kwa ajili ya vizazi vyetu
Kingine naona serikali haina utashi wa kuondosha huu uchafu wa ushoga.
Serikali inayoweza kupambana na vita ya madawa ya kulevya, ujambazi na Ugaidi haiwezi kushindwa kukomesha ushoga na usagaji
Serikali tuleteeni sheria Kali kuzuia haya mauchafu, msiogope agenda za wazungu, sisi ni nchi huru
Naona Kwa Sheria hizi Bado ni ngumu hata wewe kupambana na huu uhuni wa ushoga na usagaji
Pili, Jamani, Serikali Iko serious wewe huoni mimi pia ni Waziri napambana kwenye eneo langu? Au unadhani napambana kama Dorothy Gwajima?
Kuhusu Sheria, nimeshasema tutaboresha siyo kuandika tu bali, kuelimisha jamii pia maana naona zipo kibao zimeandikwa ila watu hawajui na wakikosea ukasema uchukue hatua wanaanza ohhhh msameheni hakuwa anajua. Sasa wakati tunaenda kuboreshwa, Mimi natangulia na Elimu kuboresha fikra za jamii wazijue hizi zilizopo. Hatupambani tu na ushoga Bali na tabia zetu zinazochochea ushoga. Hivi unaanzaje kufanya mambo ambayo Wala siyo Sanaa kwamba tunaelimisha jamii ila unajifanyia fanyia tu kisa biashara hata leseni ya matangazo hayo huna halafu unajivisha uhusika (impersonation) hata kwenye maisha yako halisi. Wewe hapo unaonaje?