Kwaza operation hapo Gaza sio baina ya taifa na taifa, hivyo sio kipimo sahihi cha uwezo wote wa kivita wa nchi. Ni kipimo cha kipengele kidogo cha uwezo wa kijeshi kufanya counter terrorism na missions within civilian populated areas controlled by your enemy. Hamas ni kundi la Wapalestina, sio Wapalestina wote ni wanachama wa Hamas ila ni almost Wapalestina wote hawaipingi Hamas (kuna wasioikubali kadhaa, nao sio hawaikubali totally bali njia zake zinazosababisha majibu kutoka Israel ndizo hawakubaliani nazo).
Kupigana na kundi lenye ideology ya kidini sio rahisi na haitumii muda mfupi.
Kinachoilinda Hamas ni kupigana na professional military inayojaribu kuzingatia sheria za kimataifa za kuendesha vita. Kama ingekuwa wote ni vichaa hapo Gaza pangekuwa pamejaa mashimo na watu laki kadhaa wamefariki. Na Hamas wanajichanganya na raia, hawana sare, hawana kambi, hawana ofisi. Wao kila kitu wanatumia cha raia wa kawaida kasoro silaha. Hivyo ukiwashambulia unazingatia kulinda wasio na hatia, raia waliokufa wote hao ni collateral damage ni bahati mbaya, ingekuwa Israel wanapiga tu vyovyote wakiona gaidi moja la kawaida limeingia sokoni kuna watu elfu moja hapo linadondoshwa bomu basi watu wengi wangekwishafariki.
Israel imejipa mwaka kumaliza hii operation na hadi sasa ina performance nzuri. Pale Syria walikuwepo waasi wakapigana na jeshi la Syria tangu 2011, Iran ikaingia 2013 au 2014 hivi, na jeshi la Urusi likaingia 2015 ila mpaka sasa Syria haijatawaliwa nzima na serikali. Ina maana Urusi, Iran na Syria nchi tatu zote kwa pamoja zina majeshi dhaifu dhidi ya waasi?
Mfano serikali ya Syria ilitumia mabomu ya sumu kwenye miji dhidi ya waasi yale mabomu yakaleta athari hadi kwa raia, wakimbizi walikimbilia Uturuki ila baadae wakajifungua walemavu sababu ya ile sumu
Mwishowe Assad akalaumiwa na jumuiya ya kimataifa kuwa mkatiri, wakati waasi na magaidi hawana masharti, wakiamua kuchoma moto mji wanachoma, wakiamua kukata watu koromeo wanafanya, wakiamua kulipua mifumo ya umeme na madaraja na ofisi mradi watie hasara serikali wanafanya. Ila professional military haiwezi fanya hivyo.
Uturuki ina magaidi, India ina magaidi, Pakistan, Misri vilevile, Morocco ina waasi na zote hizo zimeshindwa kumaliza waasi na magaidi kwa miaka nyingine hata 50 ila zote hizo pia zina uwezo wa kuipiga nchi fulani ya Afrika Mashariki. Ila hiyo nchi haina waasi wala magaidi.
Wakati India haikutumia mwaka kuipiga Pakistan mara mbili tofauti, Israel ilipigana na Waarabu vita mbili moja ilitumia siku 6 nyingine ikatumia kama mwezi ila hizo nchi zinapata shida kupigana na magaidi sababu ni suala la ideology.
Hamas haipati msaada kwa sasa sababu supplies zote zinazoingia Gaza kupitia Rafar closing zinakaguliwa na IDF, ni silaha chache sana zinaweza penya. Wao walikuwa na stockpile miaka yote kumbuka muda wote wanatamani kuitoa Israel hapo, lifestyle yao ni kuwaza kushambulia. Silaha, mafunzo, ujuzi na ufundi wanapita
Narudi.....