Adiosamigo
JF-Expert Member
- Oct 2, 2013
- 7,681
- 9,892
Sa we tulizana hata chakula cha moto ukikila unakipuliza utababuka, sisi tunapiga mlo taratibu hio Tel Aviv haiko mbali sana tutafika tu na kuisafisha.ivi we unafikiri kuna kitu ambacho mwarabu anakitamani kama kuisafisha tel aviv? shida sasa ni je ataisafishaje? au we unafikiri atatumia fagio?
Hehee umesikika mkuuWazee wa spana muacheni acheni kidogo peasant wa mpunga asikimbie mapema.
Duuu kumbe kichapo Waislam wa Palestine hawakipati tu Toka kwa Wayahudi bali hata Allah ameamua kuwarudiAnalia lia nani
Lini umeona hamas huko UN kaenda akalia lia
Hamas kasema wazi haitasimamisha vita wala kuwaacha magaidi wa kizayuni wanaowashikilia mpaka magaidi ya israhell yaondoke ghaza
Sasa sijui anaelia lia nani kati yako wewe na hamas
Hamas kundi teule
Excellent. Its a good review.Kwaza operation hapo Gaza sio baina ya taifa na taifa, hivyo sio kipimo sahihi cha uwezo wote wa kivita wa nchi. Ni kipimo cha kipengele kidogo cha uwezo wa kijeshi kufanya counter terrorism na missions within civilian populated areas controlled by your enemy. Hamas ni kundi la Wapalestina, sio Wapalestina wote ni wanachama wa Hamas ila ni almost Wapalestina wote hawaipingi Hamas (kuna wasioikubali kadhaa, nao sio hawaikubali totally bali njia zake zinazosababisha majibu kutoka Israel ndizo hawakubaliani nazo).
Kupigana na kundi lenye ideology ya kidini sio rahisi na haitumii muda mfupi.
Kinachoilinda Hamas ni kupigana na professional military inayojaribu kuzingatia sheria za kimataifa za kuendesha vita. Kama ingekuwa wote ni vichaa hapo Gaza pangekuwa pamejaa mashimo na watu laki kadhaa wamefariki. Na Hamas wanajichanganya na raia, hawana sare, hawana kambi, hawana ofisi. Wao kila kitu wanatumia cha raia wa kawaida kasoro silaha. Hivyo ukiwashambulia unazingatia kulinda wasio na hatia, raia waliokufa wote hao ni collateral damage ni bahati mbaya, ingekuwa Israel wanapiga tu vyovyote wakiona gaidi moja la kawaida limeingia sokoni kuna watu elfu moja hapo linadondoshwa bomu basi watu wengi wangekwishafariki.
Israel imejipa mwaka kumaliza hii operation na hadi sasa ina performance nzuri. Pale Syria walikuwepo waasi wakapigana na jeshi la Syria tangu 2011, Iran ikaingia 2013 au 2014 hivi, na jeshi la Urusi likaingia 2015 ila mpaka sasa Syria haijatawaliwa nzima na serikali. Ina maana Urusi, Iran na Syria nchi tatu zote kwa pamoja zina majeshi dhaifu dhidi ya waasi?
Mfano serikali ya Syria ilitumia mabomu ya sumu kwenye miji dhidi ya waasi yale mabomu yakaleta athari hadi kwa raia, wakimbizi walikimbilia Uturuki ila baadae wakajifungua walemavu sababu ya ile sumu
Mwishowe Assad akalaumiwa na jumuiya ya kimataifa kuwa mkatiri, wakati waasi na magaidi hawana masharti, wakiamua kuchoma moto mji wanachoma, wakiamua kukata watu koromeo wanafanya, wakiamua kulipua mifumo ya umeme na madaraja na ofisi mradi watie hasara serikali wanafanya. Ila professional military haiwezi fanya hivyo.
Uturuki ina magaidi, India ina magaidi, Pakistan, Misri vilevile, Morocco ina waasi na zote hizo zimeshindwa kumaliza waasi na magaidi kwa miaka nyingine hata 50 ila zote hizo pia zina uwezo wa kuipiga nchi fulani ya Afrika Mashariki. Ila hiyo nchi haina waasi wala magaidi.
Wakati India haikutumia mwaka kuipiga Pakistan mara mbili tofauti, Israel ilipigana na Waarabu vita mbili moja ilitumia siku 6 nyingine ikatumia kama mwezi ila hizo nchi zinapata shida kupigana na magaidi sababu ni suala la ideology.
Hamas haipati msaada kwa sasa sababu supplies zote zinazoingia Gaza kupitia Rafar closing zinakaguliwa na IDF, ni silaha chache sana zinaweza penya. Wao walikuwa na stockpile miaka yote kumbuka muda wote wanatamani kuitoa Israel hapo, lifestyle yao ni kuwaza kushambulia. Silaha, mafunzo, ujuzi na ufundi wanapita
Narudi.....
Mkuu, picha nyingi za vita ya Gaza hasa upande wa madhara kwa raia zinarushwa na Tv za Aljazeera, na za Kiarabu. Na nyingi ni exaggerated wakitumia sana AI. Mimi nafuatilia sana vita hii. Mfano ni picha za watoto wadogo wanaokufa zinazalishwa several times. Cha ajabu miili iliyokwishafungwa kwa maziko mingi inayoonyeshwa ni ya watu wazima. Na definately ni wapiganaji wa Hamas, ambao Tv hizo huficha kutoa idadi.Tatizo lako uchambuzi wako siku hizi ulisha kaa kipropaganda zaidi.
Hoja yako ya Israel kuepusha mauaji ya raia ni mufisirisi kabisa kwa sababu Israel amesha vuka mipaka yote ya sheria za kimataifa hivyo hicho kisingizio hakina uzito.
Israel ingekuwa inazingatia maisha ya watu na sheria za kimataifa isinge kuwa inashambulia shule, hospital,kambi za wakimbizi magari ya wagonjwa ambazo anajua kabisa kuna maelfu ya watu wamejihifadhi kwa ajili ya kutafuta usalama.Ni leo tu waziri wa Ulinzi wa Marekani mdhamini mkuu wa Israel ameitadharisha Israel kuwa haifanyi vya kutosha kuepusha mauaji ya raia.
Jana Ujerumani ameimbia Israel kuwa ni razima ijitathimi kwa sababu mauaji ya raia hayaendani na uhalisia wa vita bali kinacho onekana ni mauaji ya kiholela.
Wiki chache zilizo pita raisi wa Ufaransa aliikosoa Israel na kuiambia kuwa inatakiwa ifuate kilicho wapeleka Gaza na sio kuuwa watoto na wanawake, leo tena rais wa kamisheni ya umoja wa Ulaya amesema uharibifu huko gaza ni zaidi ya ule uliotokea Ujerumani kwenye vita ya dunia maana yake ni kuwa uharibifu wa Israel huko gaza umevuka mipaka. Kwahiyo inataka kuniambia kuwa ww una uwelewa wa kijeshi kuliko viongozi hao.
Nimeamua nikuwekee nikuu za viongozi ambao mataifa yao ni waungaji mkono wa Israel maana ninge kuwekea za rais wa Iran au Uturuki ungesema kuwa wanafanya propaganda kwa sababu Israel ni mshindani wao.
Ina maana mpaka washirika wake wanashangazwa na mauaji na uharibifu wa kiholela unao fanywa na huyo mshirika wao walio amini kuwa ana weledi
Ww kama una hoja nyingine uiweke ila hiyo haiuziki kabisa.
Kuhusu waasi nchini Syria sehemu ambayo mpaka sasa haidhibitiwi na serikali ni jimbo la Idrib ambapo lina dhibitiwa na waasi wanao ungwa mkono na Uturuki na pia kule kuna wanajeshi wa Uturuki na Urusi ndo iliyo izuia serikali ya Syria kulishambulia eneo hilo kutokana na makubaliano na Uturuki, eneo lingine ni jombo la Raqaa ambalo linadhibitiwa na wakrudi wanao ungwa mkono na Marekani na pia kuna wanajeshi wa Marekani hivyo Syria haiwezi kulishambulia kwa kujizuia kuingia moja kwa moja kwenye mzozo na Marekani na pia wapiganaji wa kikurdi hawana uhasama wowote na Asad na wala hawajawahi kushiriki vita ya kumtoa Asad Madarakani.
miaka zaidi ya 50 sasa kuanzia mtimuliwe, mtafika lini?Sa we tulizana hata chakula cha moto ukikila unakipuliza utababuka, sisi tunapiga mlo taratibu hio Tel Aviv haiko mbali sana tutafika tu na kuisafisha.
Huu ndio ukweli!!Kama utakumbuka gogoro la Uikrane/Urusi mwanzoni mwa SMO, Putin alisema yeyote atakayeingilia atakiona Cha moto.Hili utathibitisha Hali ilivyo nchi za ulaya kiuchumi na nyinginezo.
Ukumbuke Urusi na Israel wanamahusiano mazuri,hasa Urusi iliwasaidia Waisrael Toka mikononi mwa Hitler,kosa watakalojutia ni kupeleka siraha kimya kimya Uikrane huku wakimwambia Putin tupo pamoja,Wala usijali.
Wagner walipotokomea nchini Belarus Toka Urusi,wapiganaji wapatao 20,000 WA Wagner hawajulikani walipo humo nchini Belarus,UK ililalamikia hili suala.Uk ikaenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa hao wapiganaji juu ardhi hawapo labda chini ya ardhi.Wiki mbili hazijapita kikawaka Israel.Mkong'oto aloupata Israel hatosahau na hatokubali Hali kama hiyo kujirudia.
Wafatiliaji wa masuala ya kivita wanapoangalia aina ya upiganaji WA Hamas hauna tofauti na Urusi.
View attachment 2840725View attachment 2840727View attachment 2840728
Hahaahaaa!.Kwaza operation hapo Gaza sio baina ya taifa na taifa, hivyo sio kipimo sahihi cha uwezo wote wa kivita wa nchi. Ni kipimo cha kipengele kidogo cha uwezo wa kijeshi kufanya counter terrorism na missions within civilian populated areas controlled by your enemy. Hamas ni kundi la Wapalestina, sio Wapalestina wote ni wanachama wa Hamas ila ni almost Wapalestina wote hawaipingi Hamas (kuna wasioikubali kadhaa, nao sio hawaikubali totally bali njia zake zinazosababisha majibu kutoka Israel ndizo hawakubaliani nazo).
Kupigana na kundi lenye ideology ya kidini sio rahisi na haitumii muda mfupi.
Kinachoilinda Hamas ni kupigana na professional military inayojaribu kuzingatia sheria za kimataifa za kuendesha vita. Kama ingekuwa wote ni vichaa hapo Gaza pangekuwa pamejaa mashimo na watu laki kadhaa wamefariki. Na Hamas wanajichanganya na raia, hawana sare, hawana kambi, hawana ofisi. Wao kila kitu wanatumia cha raia wa kawaida kasoro silaha. Hivyo ukiwashambulia unazingatia kulinda wasio na hatia, raia waliokufa wote hao ni collateral damage ni bahati mbaya, ingekuwa Israel wanapiga tu vyovyote wakiona gaidi moja la kawaida limeingia sokoni kuna watu elfu moja hapo linadondoshwa bomu basi watu wengi wangekwishafariki.
Israel imejipa mwaka kumaliza hii operation na hadi sasa ina performance nzuri. Pale Syria walikuwepo waasi wakapigana na jeshi la Syria tangu 2011, Iran ikaingia 2013 au 2014 hivi, na jeshi la Urusi likaingia 2015 ila mpaka sasa Syria haijatawaliwa nzima na serikali. Ina maana Urusi, Iran na Syria nchi tatu zote kwa pamoja zina majeshi dhaifu dhidi ya waasi?
Mfano serikali ya Syria ilitumia mabomu ya sumu kwenye miji dhidi ya waasi yale mabomu yakaleta athari hadi kwa raia, wakimbizi walikimbilia Uturuki ila baadae wakajifungua walemavu sababu ya ile sumu
Mwishowe Assad akalaumiwa na jumuiya ya kimataifa kuwa mkatiri, wakati waasi na magaidi hawana masharti, wakiamua kuchoma moto mji wanachoma, wakiamua kukata watu koromeo wanafanya, wakiamua kulipua mifumo ya umeme na madaraja na ofisi mradi watie hasara serikali wanafanya. Ila professional military haiwezi fanya hivyo.
Uturuki ina magaidi, India ina magaidi, Pakistan, Misri vilevile, Morocco ina waasi na zote hizo zimeshindwa kumaliza waasi na magaidi kwa miaka nyingine hata 50 ila zote hizo pia zina uwezo wa kuipiga nchi fulani ya Afrika Mashariki. Ila hiyo nchi haina waasi wala magaidi.
Wakati India haikutumia mwaka kuipiga Pakistan mara mbili tofauti, Israel ilipigana na Waarabu vita mbili moja ilitumia siku 6 nyingine ikatumia kama mwezi ila hizo nchi zinapata shida kupigana na magaidi sababu ni suala la ideology.
Hamas haipati msaada kwa sasa sababu supplies zote zinazoingia Gaza kupitia Rafar closing zinakaguliwa na IDF, ni silaha chache sana zinaweza penya. Wao walikuwa na stockpile miaka yote kumbuka muda wote wanatamani kuitoa Israel hapo, lifestyle yao ni kuwaza kushambulia. Silaha, mafunzo, ujuzi na ufundi wanapita
Narudi.....
6 days war,wewe ulikuwepo? Advanced technology ya media ilikuwa ya kiwango gani hata tupate ukweli uliofichwa?.Wewe Hamas ni Muslim Brotherhood; kwa itikadi yao wana wafadhili ambao wamejipenyeza ktk nchi za Magharibi na upo mkakati wao kabambe wa kutekeleza Agenda yao ulimwenguni kote. Nitakurushia hapa. Ktk agenda hiyo hiyo, wanafadhiliwa na Qatar. Iran ingawa ni Mshia, amekuwa na mapenzi na Hamas kwa vile Hamas hawapatani na Majority Sunni States na vile vile Hamas ktk 1988 charter yao wanataka kulifutilia mbali Taifa la Israel. Hivyo, Iran anamsaidia sana Hamas kwa sababu wote Wana common enemies.
Kuhusu vita kwenda muda mrefu, ngoja nikwambie kitu, kama si kuhofia kuua raia wa kawaida Israel wangeisha maliza zamani vita hiyo. Ona walichoyafanya mataifa ya kiarabu ktk Ile 6 days war!
Africa ilitawaliwa na wakoloni zaidi ya miaka 100 hizo 50 ni midogo sanamiaka zaidi ya 50 sasa kuanzia mtimuliwe, mtafika lini?
Kwa Gaza hakuna sehemu inayoitwa karibu na shule au mbali na hospitali.Katika eneo dogo kama lile na msongamano wa watu ukitaka kujenga chini ya ardhi kila sehemu ni karibu na nyengine.Hii vita Israel kapihana kwa ustaarabu mkubwa sana. Karibia mwezi mzima hakuingiza keshi, ila ilikuwa mashambulizi ya angani tu kulenga popote Hamas na mali zao zilipo.
Hamas walitumia muda mrefu kujenga mahandaki ya chini tena karibu na miundombinu ya kiraia kama shule, hospital na nyumba za ibada. Lakini pia wapiganaji wa Hamas wengi hawana sare ila wamevaa kiraia hata ukiwaua unaambiwa umeua raia.
Hivyo Israel amekuwa akipigana na watu wanajificha kwenye mahandaki na katikati ya raia. Hii siyo conventional war ila operation ya kusafisha mji.
Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
ndo wapambane sasa tuone kama watatoboaAfrica ilitawaliwa na wakoloni zaidi ya miaka 100 hizo 50 ni midogo sana
Wenzako wanawapigia magoti Hamasi kuomba vita isimame.ndo wapambane sasa tuone kama watatoboa
Itoshe tu kusema hii vita imejaa propaganda nyingiWakuu naamini muko buheri wa afya, pole kwa ambao wanapitia changamoto ya afya na Mungu awaponye.
Naombeni wanajukwaa munijibu swali langu kuhusu vita kati ya Hamas na jeshi la Serikali ya Israel. Nitashukuru iwapo jibu/majibu yataepuka yale maneno na misamiati ya "Wazee wa Makobazi", "migalatia" na mengine yenye kuashiria kuegemea upande flani ili kuweza kujifunza.
Japo nina imani yangu, lakini nauliza hili nikiwa neutral na dhamira kuu ni kupata maarifa kwa watu wenye utaalamu wa maswala ya kivita pamoja na siasa za kimataifa kwa hiyo naomba pia wenye kujibu wawe neutral.
Niende kwenye mada kama ilivyo kwenye kichwa cha habari hapo juu.
Hamas kwa uchache wao (kwa kuzingatia eneo la Kijiographia) sidhani kama wangekuwa bado wanapambana na jeshi la IDF takribani kwa miezi miwili bila kupata msaada wowote wa kijeshi iwe silaha,milltary personnel au hata upelelezi dhidi ya jeshi linaloaminika kuwa bora na lenye kupata back up kutoka kwa Marekani na washirika wake (kama wapo)
Kama wanasaidiwa, swali linakuja na nani na hiyo misaada inaingiaje kwenye eneo dogo na ambalo kwa kiasi kikubwa limezingirwa na linashambuliwa kwa makombora mazito ya kila siku na jeshi la Israel?
Kwa kuzingatia eneo dogo la ukanda wa Gaza na kuwa Palestina ni nchi (japo haina sovereignty) ambayo almost inazungukwa kila upande na Israel, nadhani siyo rahisi kuingiza silaha kutoka nje hasa kipindi hiki cha vita bila kufahamika na jeshi la IDF(niko tayari kurekebishwa kama nitakuwa nimekosea)
Rejea hapa [emoji116]
"With around 2 million Palestinians on approximately 365 km2 (141 sq mi) of land, Gaza has one of the world's highest population densities. The Strip contains eight refugee camps."(WIKIPEDIA)
Na kama hawana msaada (hususani wa kijeshi ndani ya eneo la kivita) nguvu hii ya kupambana hadi leo wanaitoa wapi na silaha zao mfano wa manati dhidi ya vifaru na ndege vita bora kuwahi kutokea. Au kwamba walidunduliza kwa kipindi kirefu kabla ya vita?
Mwisho kwa ajili ya kujifunza, nini hatma ya vita hii iwapo Israel itafanikiwa kuwaondosha Hamas katika ukanda wa Gaza? Je, eneo hili litakuwa mali halali ya Israel au wataachiwa Wapalestina wenyewe chini ya uangalizi wa Serikali Jerusalem?
Nawasilisha na naomba kujifunza kutoka kwenu.
Sasa mbona watu wanazidi kufa tuJamas wana msaada na wanasaidiwa sana kupita yeyote yule.
Wanasaidiwa na Allah.
Naam, nani ambae hatakufa?Sasa mbona watu wanazidi kufa tu