Je hapa Nina mke kweli?atumia laki tatu ndani ya wiki3 akiwa ugenini katika harus

T14 Armata

Amesema yupo nyumbani kwao kwa baba na mama.
Una watoto wachanga mkuu?

Mimi sina mtoto ila agemates wangu ninaofanya nao majukumu wenye watoto naona matumizi yao yalivyo makubwa. Kila muda mtoto malipo, matumizi, kuumwa, kukosa usingizi, kulia sana.

Sioni ajabu ya matumizi ya 16,600 kwa siku kwa mke na watoto wawili wadogo.
 
Ni hela ndogo ndugu Kwa wiki zote hizo. Watoto wawili, mbaya zaidi yupo kwenye shunguli. Hapo alihitaji walau milioni moja.
 

 
Sasa ualike watu nyumbani kwako mwezi mzima alafu huna budget yakuwahudumia
 
Sasa ualike watu nyumbani kwako mwezi mzima alafu huna budget yakuwahudumia
Ualike watu kwako mwezi mzima umekua bakhresa. Mtu na familia unaendaje kukaa kwa watu wiki 3 bila sababu maalumu na una kwako. Kwa style hii ndio maana siku hizi watu wanajenga servant quarters sio majumba makubwa kuepusha ugeni unao haribu budget.

Kwangu tu shule zikifungwa budget inaongezeka sembuse wageni na watoto wakae wiki 3
 
We ni akili kubwa sana... utafika mbali
Mi napenda kukaa kwangu kwa watu sisikii raha ,kuna watu wanapenda kuzurura kuna mke wa ndugu yangu ni safari kila mara mara harusi mara sijui mgonjwa akienda ameenda nadhan hampendi mmewe anaona tabu kuishi nae
 
Basi uwe na hicho kipato Ila kama ni KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA BASI HUWEZI KU SUSTAIN.

Mfano mtu Fulani anapata malipo ya 1,100,000 yupo dar es salaam unakuta haimtoshi.

Mfano nauli per day kwenda na kurudi home @ 7000 , chakula mchana @ 2000 , so kwa siku @ angalau 9000

Nyumbani una waachia @ 10,000 hapo NDANI Kuna kila kitu yaani mboga zoteee kuku,nyama,samaki, maini, soseji, mayai , nyanya ,hoho, karoti, vitunguu E.t.c

Unakuta hiyo pesa haitoshi ndani ya mwezi mmoja.

Kikubwa watanzania hatuishi ndani ya BUDGET na hatunaga budget kabisaa ndio maana huyo mwanamke kashindwa ku manage 350k ndani ya week 3
 
Yaan shida Sasa mkuu unaalikaje watu waje kwenye harusi nahujajipanga kuwalisha
 
Hii bajeti imenitoa roho 😂 hivyo vyote bado niache hela 🤔
 
Mkuu ndo mke amalize Hela zote hata dawa ya 3000 ya mtoto wake mwenyewe akose,basi atakua kageuka muhemeaji wa familia sasa
Sasa kaenda kwao na mume mapene unayo. Acha unaa anakujengea heshima ukweni kwamba ana mume mwenye nazo. Wewe tuma na mtumie nauli fasta arudi maana kwa mada hii unaonekana una upwiru mwingi. Kumbuka mke umleavyo ndivyo akuavyo.
 
Raha ya mwanamke ni kumuomba mwanaume walke hela. hata kama anayo inaashiria kwamba anakuheshimu na anatambua nafasi yako kama mwanaume na baba
 
PYaan shida
Sasa mkuu unaalikaje watu waje kwenye harusi nahujajipanga kuwalisha
Harusi ni siku moja na chakula kipo ukumbini. Wewe umempeleka akakae wiki 3 unataka alishwe na nani siku zote hizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…