Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Nimekupa mfano wa kibinadamu lakini nikiwa nalenga hapo hapo kwenye swala la kihukumu.Unapinga mimi kutumia mifano ya mabadiliko ya binadamu na hali ya hewa unapinga kwa kusema kuwa mambo hayo ama mabadiliko hayo ni tofauti na sheria ama hukumu.
Wakati huo huo wewe unatoa mifano yako hii ya hesabu kujenga hoja ambayo unataka ikusapoti.
Sasa huu mfano wa hesabu ambao umeutumia kujenga hoja ya mapungufu manake ni kuwa hauhusiani na mambo ya sheria kwa sababu ni mbali mbali kabisa kama ambavyo wewe umeona mbali mbali mambo ya sheria na mabadiliko ya binadamu.
I
Nitasikiliza hoja zake za mabadiliko hayo.
Ikiwa atakiri kuwa amekosea 2+2 sio 7 basi hapo nitakubali kuwa alikosea ama alijichanganya.
Lakini akiwa na hoja zake mwenyewe siwezi kusema kajichanganya,sitohukumu moja kwa moja kuwa kajichanganya.
Kwa sababu anaweza kusema kuwa 2+2=7 but 2 ya mwisho inamuwakilisha 5,hivyo kwenye mbili ya mwisho ni tano hiyo.
Kwa hiyo itakuwa 2+5=7.
Sasa kwa hoja mfano wa hii siwezi kusema kajichanganya.
Mungu aliona sahihi kwa ndugu kwa ndugu kukutana kimapenzi lakini huyo huyo anakuja kukataza kuwa sio sahihi kuingiliana kimapenzi ndugu kwa ndugu.
Hapa unaona ni namna gani Mungu anajichanganya kwa kutoa kauli mbili mbili