safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Tatizo sio Mungu kuwa kigeugeu,tatizo ni sisi kuhisi hivyo na tunao uhuru wa kuwaza vyovyote kwa uwezo aliotupatia huyo Mungu mwenyewe.Kama Mungu akibariki na kukiruhusu jambo lifanyike halafu baada ya muda alione hilo jambo halifai, huoni linaleta sifa ya Mungu kuwa kigeugeu
Wewe unaweza kuwaza kuwa Mungu kigeugeu,lakini ndio kanuni ya Mungu mwenyewe hata nje na hapo utaona kuwa mambo mengi yana mabadiliko sio utaratibu wa Mungu tu.
Jua linabadilika badilika,asubuhi jekundu mashariki,mchana jeupe katikati,jioni jekundu magharibi.
Hapa sijui kama tutasema jua kigeugeu.
Usiku giza,mchana mwanga.
Sijui tutasema siku ni kigeugeu ama vipi.
Unaanza kuwa mtoto mdomo hauna meno,unakuwa kijana unota meno,unakuwa mtu mzima mwishoni unakuwa mzee kabisa na mvi.
Sidhani kama tutasema kuwa mwili ni kigeugeu hauelewei hauna msimamo.
Embe inaanza maua,inaanza kuwachanga,mwishowe inaiva,baadae inaoza.
Sidhani kama tutasema embe ni kigeugeu.
Kwa hiyo sio kwamba Mungu kigeugeu kwa kugeuza sheria,bali huo ndo utaratibu wake wa mambo mengi katika dunia alivyoyaweka.
Kusema kigeugeu unaweza kusema lakini ukitumia akili ya kawaida juu ya mambo mengine ya asili na ukaangalia utaona kuwa hakuna tatizo kufanya mabadiliko kutokana na zama ambazo yeye mwenyewe anazijua.
Bila shaka >ngekuwa anabahatisha basi hao ambao hawabahatishi wangekuja na utaratibu wao ambao upo costant haubadiliki.Huoni kama Mungu anakuwa hajui alifanyalo bali anabahatisha tu?
Yani wangekuja na binadamu ambao akizaliwa mpaka anakufa ananyonya,hakui yani yuko vile vile habadiliki.
Wangekuja na utaratibu wao wa jua kuwa likichomoza linabaki pale pale tu haliendi kokote mpaka leo.
Bila shaka maisha kwa ujumla ni mabadiliko na wenyewe tunashuhudia hili.
Mabadiliko katika maisha huwezi kuyanasibisha na kutokuwa na uhakika juu ya kile mtu anachofanya.
Kwa hiyo nikijibu swala lako ni kuwa mungu habahatishi na anajua afanyalo kwa sababu hiyo ndio system yake.