Je, harusi ya Adam na Hawa ilifanyikia wapi, nani aliwafungisha ndoa?

Je, harusi ya Adam na Hawa ilifanyikia wapi, nani aliwafungisha ndoa?

Haya sasa, wataje binadamu wa kawaida, au manabii, au mitume waliofikia ukamilifu kwa kutumia hizo ala, walau hata 10 tu
Niwataje mara ngapi mzee ?

Mitume wote wamefikia huo ukamilifu sababu mwisho ni pepo na moto. Na wapo wasio kuwa mitume ba wapo wa elfu 70.

Sasa idadi uliyo itoa ni ndogo sana mzee, na nimekupa hiyo na ziada.
 
Hili tatizo naona unakimbia jukumu la swali. Mimi ukiniambia kaulo hii sikanushi zaidi ya kukuhoji na unipe ithibati. Sasa unaposema ndiyo hivyo hivyo kama katika suala la hadithi, wewe ndiyo ulikanusha sasa inabidi ututhibitishie ya kuwa Hadithi zimetungwa, na mimi nilikuhoji na mimi sija kanusha. Sasa usibishe kwenye hakuna sababu umekanusha.
Exactly my point, kitendo cha wewe kuhoji na kutaka uonyeshwe mahali kinyesi kilipo ndivyo vivyo hivyo na sisi tunavyohoji juu ya uhalisia wa hizo hadithi. Sasa sisi tunapokuhoji utupe udhibitisho wa hizo hadithi kama ni za kweli , wewe badala ya kutupa udhibitisho unataka sisi ndio tukupe udhibitisho kwamba ni za uongo. Sasa kama hapa unapohoji nikuoyeshe mahali kinyesi kilipo, nami nakwambia dhibitsha kwanza kwamba hakipo.., utajisikaje? Yaani umenihoji mahali ninyesi kilipo, halafu badala ya mimi kukuonyesha kilipo kinyesi kama ulivyohoji, mimi najitoa akili halafu nakwambia, kabla sijakuonyesha, dhibitisha kwanza kwamba hakipo, hivi utajisikiaje nikafanya hivyo?!

Maana mtu anakaa tu anaanza kuandika hadithi kwamba mwanzo kulikuwa na mtu mmoja tu Adam, halafu kwenye ubavu wake akatolewa Hawa, halafu wakazaa watoto, na hao watoto wakaenda nchi za mbali na wakaenda kuoa na kuolewa huko kwenye nchi za mbali, hivi hao waoaji na waolewaji wa hizo nchi za mbali walikuwa ni mbwa au ni binadamu? Na walitoka wapi kama hapakuwa na binadamu kabla ya Adam? Sasa tukihoji juu ya uhalali wa hizi hadithi ni kwa sababu ya mkanyiko kama huu..,sasa dhibitisheni hizi hadithi...
 
Niwataje mara ngapi mzee ?

Mitume wote wamefikia huo ukamilifu sababu mwisho ni pepo na moto. Na wapo wasio kuwa mitume ba wapo wa elfu 70.

Sasa idadi uliyo itoa ni ndogo sana mzee, na nimekupa hiyo na ziada.
Kwahiyo mitume wote ni wakamilifu? Hata yule aliyemsaliti Yesu kwa vipande vya fedha? Au huo ukamilifu waliufikia wakiwa wameshakufa?
Na mwisho kuwa pepo na moto kunawafanya vipi mitume kufikia ukamilifu? Na hao elfu 70 wasio mitume ni akina nani, sisi tumehitaji majina 10 tu unaowafahamu
 
Exactly my point, kitendo cha wewe kuhoji na kutaka uonyeshwe mahali kinyesi kilipo ndivyo vivyo hivyo na sisi tunavyohoji juu ya uhalisia wa hizo hadithi.
Nionyese wapi ulipo hoji au wapi mlipo hoji juu ya hadithi zaidi ya kukanusha. Inaonekana hujui maana ya kuhoji na kukanusha.

Hili ni tatizo la kuvamia hoja kichwa mchunga. Nilikosea sana hapo awali kujadiliana na nyinyi kabla ya kuwafundisha. Naona sasa somo limeingia na umelielewa, sasa ikitokea umehoji nistue nikuthibitishie, ila kabla ya hapo thibitisha uongo wa hizo hadithi na utuonyeshe ya kuwa ni hadithi za kutungwa.

Ahsante.
 
Sasa sisi tunapokuhoji utupe udhibitisho wa hizo hadithi kama ni za kweli , wewe badala ya kutupa udhibitisho unataka sisi ndio tukupe udhibitisho kwamba ni za uongo. Sasa kama hapa unapohoji nikuoyeshe mahali kinyesi kilipo, nami nakwambia dhibitsha kwanza kwamba hakipo.., utajisikaje? Yaani umenihoji mahali ninyesi kilipo, halafu badala ya mimi kukuonyesha kilipo kinyesi kama ulivyohoji, mimi najitoa akili halafu nakwambia, kabla sijakuonyesha, dhibitisha kwanza kwamba hakipo, hivi utajisikiaje nikafanya hivyo?!
Hamjawahi kuhoji hilo, landa muhoji sada, bali huwa mnakanusha na mnapo kanusha sasa sisi ndiyo tuna wahoji na kutaka mtuthibitishie, lakini hili mnalikwepa sababu mnajua ya kuwa hamuwezi kuthibitisha hilo. Ili nikuonyeshe hata sasa hili hamliwezi, wewe nithibitishie ya kuwa hizi hadithi ni za kutungwa, ukiweza mimi kauli yangu ni ile ile, nitaomba hii ID ifungiwe na wewe utakuwa shahidi. Hasa tujikite katika masimulizi ya Uislamu.

Kujitutumua kote hata tofauti ya kuhoji na kukanusha huijui, halafu mnakuja kusumbua watu. Hatulei ujinga.

Ahsante.
 
Kwahiyo mitume wote ni wakamilifu? Hata yule aliyemsaliti Yesu kwa vipande vya fedha? Au huo ukamilifu waliufikia wakiwa wameshakufa?
Na mwisho kuwa pepo na moto kunawafanya vipi mitume kufikia ukamilifu? Na hao elfu 70 wasio mitume ni akina nani, sisi tumehitaji majina 10 tu unaowafahamu
Tuliza akili na usome nilichokiandika na usihoji kile ambacho hakipo hata nikikwambia unionyeshe huwezi.

Ama kuhusu mitume na manabii hili nijambo sahali sana kwangu.

Ibrahiim, Is'haaq, Ismaeli, Nuhu, Dawood, Saleh, Musa, Issa, Muhammad, Yunus, Idrisa, Suleymaan, Yaqoub, Huu, Luut.
 
Nionyese wapi ulipo hoji au wapi mlipo hoji juu ya hadithi zaidi ya kukanusha. Inaonekana hujui maana ya kuhoji na kukanusha.

Hili ni tatizo la kuvamia hoja kichwa mchunga. Nilikosea sana hapo awali kujadiliana na nyinyi kabla ya kuwafundisha. Naona sasa somo limeingia na umelielewa, sasa ikitokea umehoji nistue nikuthibitishie, ila kabla ya hapo thibitisha uongo wa hizo hadithi na utuonyeshe ya kuwa ni hadithi za kutungwa.

Ahsante.
Kwahiyo tunapohoji juu ya mambo mengi lukuki juu ya hizo hadithi wewe huwa unaona huko si kuhoji? Nikupe Mfano mmoja katika mingi : Hadithi inasema kwamba binadamu wa Kwanza Adam, alipata mke wake tokea ubavuni kwake halafu wakazaa watoto, hao watoto wakaenda nchi za mbali kuoa na kuolewa, sasa kwa akili za kawaida tu, hao watoto walienda kumuoa nani au kuolewa na nani huko nchi za mbali?
 
Hamjawahi kuhoji hilo, landa muhoji sada, bali huwa mnakanusha na mnapo kanusha sasa sisi ndiyo tuna wahoji na kutaka mtuthibitishie, lakini hili mnalikwepa sababu mnajua ya kuwa hamuwezi kuthibitisha hilo. Ili nikuonyeshe hata sasa hili hamliwezi, wewe nithibitishie ya kuwa hizi hadithi ni za kutungwa, ukiweza mimi kauli yangu ni ile ile, nitaomba hii ID ifungiwe na wewe utakuwa shahidi. Hasa tujikite katika masimulizi ya Uislamu.

Kujitutumua kote hata tofauti ya kuhoji na kukanusha huijui, halafu mnakuja kusumbua watu. Hatulei ujinga.

Ahsante.
Just incase hukuona watu wakihoji, basi nimekupa moja ya wanayoyahoji hapo juu, na hiyo ni moja wapo katika maelfu ya inconsistency wanazohoji watu. Mfano, imekuwaje hiyo hadithi haisemi chochote kuhusu maisha ya yesu kuanzia miaka 18 - 30, kipindi ambacho tulitegema Yesu angekuwa akitongoza wasichana na kuwapa mimba kama vile vijana wenzake wa umri huo huwa wanafanya, ni kwanini hiyo section ya umri wake iko blank? Au hizi si hoja ambazo watu wanahoji kila siku? Unataka wahoji nini ndio uone wana hoji?!

Mfano, mabaki ya binadamu yamepatikana na kukutwa kuwa na umri wa mamilioni ya miaka, lakini hizo hadithi umri wake ni miaka isiyozidi hata elfu 10, ina maana kabla ya adam na hawa kulikwa na dunia nyingine tofauti na hayo madai ya hadithi kwa ndio binadamu wa kwanza? Unataka wahoji nini ndio uone kwamba wanahoji?
 
Tuliza akili na usome nilichokiandika na usihoji kile ambacho hakipo hata nikikwambia unionyeshe huwezi.

Ama kuhusu mitume na manabii hili nijambo sahali sana kwangu.

Ibrahiim, Is'haaq, Ismaeli, Nuhu, Dawood, Saleh, Musa, Issa, Muhammad, Yunus, Idrisa, Suleymaan, Yaqoub, Huu, Luut.
Katika hao uliowataja mi nimebahatika kumjua mmoja tu, nae ni Muhammad, huyo aliemiliki watumwa? Huyo alieenda vitani kupigania dini na kuua baba na waume za watu kisha kuchukua wake na watoto kama watumwa? Ukamilifu gani huo unazungumzia wewe?
 
Kwahiyo tunapohoji juu ya mambo mengi lukuki juu ya hizo hadithi wewe huwa unaona huko si kuhoji? Nikupe Mfano mmoja katika mingi : Hadithi inasema kwamba binadamu wa Kwanza Adam, alipata mke wake tokea ubavuni kwake halafu wakazaa watoto, hao watoto wakaenda nchi za mbali kuoa na kuolewa, sasa kwa akili za kawaida tu, hao watoto walienda kumuoa nani au kuolewa na nani huko nchi za mbali?
Kijana naona bado unakosea. Nukuu hadithi kama ilivyo, maana hata hadithi zina nidhamu zake za kunukuu.

Ngoja nikupe mfano wa Hadithi na namna inavyo nukuliwa.

Amesimulia Swahaba Abdullah ibn Mas'ud (Allah amridhie) "Amesema mtume wa Allah (Amani ya Allah iwe juu yake) yeyote akifa hali ana muabudu aisyekuwa Mola, basi huyo ni motoni" [Hadithi ameipokea Imaam al Bukhariy]

Hivi ndivyo Hadithi inavyonukuliwa. Hapo nimekuonyesha nani amesimulia toka kwa nani na hiyo Hadithi imepokelewa na nani na ipo katika kitabu gani.

Kwahiyo unukuzi wako una makosa mengi na unanifanya nikuulize maswali mengi kabla ya kujibu swali lako la msingi.

Sasa nukuj Hadithi kwa mtindo huu, hizi si habari za vijiweni.

Ahsante.
 
Kijana naona bado unakosea. Nukuu hadithi kama ilivyo, maana hata hadithi zina nidhamu zake za kunukuu.

Ngoja nikupe mfano wa Hadithi na namna inavyo nukuliwa.

Amesimulia Swahaba Abdullah ibn Mas'ud (Allah amridhie) "Amesema mtume wa Allah (Amani ya Allah iwe juu yake) yeyote akifa hali ana muabudu aisyekuwa Mola, basi huyo ni motoni" [Hadithi ameipokea Imaam al Bukhariy]

Hivi ndivyo Hadithi inavyonukuliwa. Hapo nimekuonyesha nani amesimulia toka kwa nani na hiyo Hadithi imepokelewa na nani na ipo katika kitabu gani.

Sasa nukuj Hadithi kwa mtindo huu, hizi si habari za vijiweni.

Ahsante.
Kuna namna nyingi za kufikishabtaarifa, unaweza ukasema exactly kilichosemwa kama hivyo, au unaweza ukasummarize hadithi ya page nzima kwa sentesi moja ili kurahisisha majadiliano, si kila ktu ana mida wa kusima aya nzima hapa. Ila hoja wanazohoji ni hizo nimekupa, labda useme kwa hivyo vipande vya hadithi havipo kwenye hivyo vitabu vya hadith, hapo sasa litakuwa ni jambo simple tu la kwenda kutafuta aya na mstari gani vilipo. Sasa jibu hizo hoja, au kama unabisha, basi sema wazi kwamba si kweli mfano: maisha ya yesu kutoka miaka 18 - 30 hayajaandikwa kitabu cha hiyo hadithi, then tokea hapo tutaenda kwenye hicho kitabu kuona kama maisha yake yameandika au laa, na katika hali kama hiyo sijui ulitaka niquote kitu gani kwa mtindo huo ulioeleza.

All in All, hoja mojawapo kati ya hoja nyingi wazohoji watu juu ya hizi hadith ni hizo, zijibu sasa, hasa hiyo ya kwenda nchi za mbali na kuoa na kuolewa, walenda kumuoa na kuolewa na nani?
 
Jibu la hilo swali la Necta ni NDIO, Necta hutunga mitihani migumu ili wanafunzi wafeli kwa sababu Serikali haina pesa za kutosha za kutoa mikopo ya chuo kikuu, pia kuna vyuo vichache sana hivyo wakifaulu wengi kutakuwa na mrundikano na msongamano vyuoni. Labda uniambie kwamba huko mbinguni kuna uhaba wa bajeti ya kuhudumia watu watakaofanikiwa kuingia mbinguni, hivyo wanaweka mchujo mkali na masharti magumu
Sipingi jibu lako kwa uonavyo wewe.

Ka
Ningekuwa sijaisoma ningekujibu? Au unataka ujibiwe vile ulivyotegemwa wewe?
Sio ugomvi mkuu usipaniki.

Kuhusu suala lako kasome comment yangu nimejibu kwa urefu tu.
 
Just incase hukuona watu wakihoji, basi nimekupa moja ya wanayoyahoji hapo juu, na hiyo ni moja wapo katika maelfu ya inconsistency wanazohoji watu. Mfano, imekuwaje hiyo hadithi haisemi chochote kuhusu maisha ya yesu kuanzia miaka 18 - 30, kipindi ambacho tulitegema Yesu angekuwa akitongoza wasichana na kuwapa mimba kama vile vijana wenzake wa umri huo huwa wanafanya, ni kwanini hiyo section ya umri wake iko blank? Au hizi si hoja ambazo watu wanahoji kila siku? Unataka wahoji nini ndio uone wana hoji?!
Safi kabisa, kwanza naona umekiri na kukubali ya kuwa kuna kuhoji na kukanusha (Hapa badi unatafuta huruma na kukimbia jukumu lako).

Habari za Yesu/Nabii Issa katika ulimwengu wa Kiislamu zimeelezewa tangu utotoni na namna mimba yake ilivyo tungwa, hili lilitosheleza juu ya kukidhi haja ya kile alicho kuja nacho, lakini kawaida mitume au manabii kuna umri ambao huwa ukifika huanza kupewa ujumbe na kazi zao kuanzia hapo.

Suala la habari zake za baina ya miaka 18 mpaka 30 ukiona hazijaelezewa ujue ya kuwa hapakuwa na haja ya kuelezewa wala haziathiri lengo la yeye kuwa nabii, yaani kuelezewa kwake na kutokuelezewa kwake ni sawa.

Labda nikuulize tu swali la msingi, maana hapa nimeona unauliza maswali ya kipuuzi na yasiyo kuwa na tija, labda jalia ya kuwa alikuwa anatongoza mademu na mfano wake, je ilikuwa kabla ya utume au baada ya utume na je habari hizo zina athiri juu ya unabii wake ?

Lakini, kuhoji ndiyo jambo la msingi, ila watu wanatakiwa wahoji mambo ya maana na si ya upuuzi kwani kuhoji upuuzi ni matumizi mabaya ya akili.
 
Mfano, mabaki ya binadamu yamepatikana na kukutwa kuwa na umri wa mamilioni ya miaka, lakini hizo hadithi umri wake ni miaka isiyozidi hata elfu 10, ina maana kabla ya adam na hawa kulikwa na dunia nyingine tofauti na hayo madai ya hadithi kwa ndio binadamu wa kwanza? Unataka wahoji nini ndio uone kwamba wanahoji?
Huu ni upuuzi mwingine, kwanza nikuulize swali unao ushahidi wa kuwa mabaki hayo kweli yana umri wa mamilioni ya miaka au wewe baada ya kupewa hiyo habari ukatosheka na kumeza kama sponchi linaponyonya maji ? Je ulihoji kwa namna gani habari hizo za mabaki ni za kweli ?

Hakuna binadamu yeyote wala vitabu vya dini havijatuambia ya kuwa Adamu aliumbwa lini wala dunia iliumbwa, majibu ya umri wa viwili hivi anajua aliye umba.

Laiti kama mngekuwa watu wa kuhoji na kuhakiki habari, hizi habari za umri wa dunia mngezikadhibisha. Sasa usiendelee kuonyesha udhaifu wako wa kuhoji kwa kumili upande mmoja huki upande wa pili huna ithibati.

Nataka wahoji vya maana kwa kurejea habari sahihi, siyo wahoji upuuzi kwa kurejea upuuzi wa wanaikolojia na mfano wao.
 
Katika hao uliowataja mi nimebahatika kumjua mmoja tu, nae ni Muhammad, huyo aliemiliki watumwa? Huyo alieenda vitani kupigania dini na kuua baba na waume za watu kisha kuchukua wake na watoto kama watumwa? Ukamilifu gani huo unazungumzia wewe?
Sababu ulikosea tangu mwanzo basi usitarajie kupatia baada ya kukosea hili, ungekuwa na busara na umakino wa kukidhi haja, ungerekehisha ufahamu wako juu ya yale niliyo yawasilisha huko nyuma.

Naweka kumbukimbi sawa, nilisema hakuna mkamilifu katika Wanadamu bali ukamilifu unapatikana baada ya kutumia nyenzo na ala zitakazo tupeleka katika ukamilifu na ukamilifu wenyewe ni kulipwa pepo kwa wema na kulipwa moto kwa waovu. Maana yake kwa duniani hakuna mkamilifu. Sasa uliza swali lako upya kulingana na hiki nilichokieleza tangu awali.
 
Kuna namna nyingi za kufikishabtaarifa, unaweza ukasema exactly kilichosemwa kama hivyo, au unaweza ukasummarize hadithi ya page nzima kwa sentesi moja ili kurahisisha majadiliano,
Safi kabisa hili ni kwa habari na si kwa hadithi, tatizo ulilivagaa tamko Hadithi bila kujua mipaka yake, na lazima ukosee kama unavyo kosea sasa.

Sasa unaponukuu Hadithi ujue ya kuwa wewe umesikia mahala au umesoma mahala, sasa katika uhakiki wa habari lazima utuambie umeitoa wapi hiyo habari kisha tunaiweka katika mizani, na kupembua mbichi na mbivu, sababu si kila habari ni hadithi.

Mathalani hicho ulicho kisema wewe kwangu mimi ni kipya, sababu mimo ni mtu makini na nimesoma elimi ya uhakiki wa habari lazima ni kuhoji ili nijue naiweka katika kundi gani habari hii, je inaingia katika hadithi, au ni visa vya wana wa Israeli au pauka pakawa.
Ila hoja wanazohoji ni hizo nimekupa, labda useme kwa hivyo vipande vya hadithi havipo kwenye hivyo vitabu vya hadith, hapo sasa litakuwa ni jambo simple tu la kwenda kutafuta aya na mstari gani vilipo.
Ndoyo maana nilikwambia hapo awali ya kuwa habari uliyo itolea mfano inanipa maswali mengi, na ndiyo maana huwa tunawaambia habari hizi mtuambie mmezitoa wapi, lakini mwisho wa siku mnatokomea sababu katika vitabu vyetu habari hizi hatuzioni.

Lakini pia mnaonyesha udhaifu mkubwa sana na kutokuwa makini kwa kuchukua habari bila kuzihakiki na kuzinasibisha ba watu fulani, watu wenye akili timamu na umakini hawapo kama mlivyo nyinyi hivi.

Kwahiyo nahitimisha kwa kukwambia hivi, rekebisheni viti vyenu kwanza kabla hamjavitia nakshi. Mwenzako mmoja amekimbia na najua hatarudi tena sababu kazi niliyo mpa ya kuniletea andiko linalo onyesha kukaidi kwa Malaika. Sasa msiwe na sifa kama ya sponchi likiwekwa kwenye mkojo litanyonya mkojo, likiwekwa kwenye maziwa litanyonya maziwa, likiwekwa kwenye maji litanyonya maji.
 
All in All, hoja mojawapo kati ya hoja nyingi wazohoji watu juu ya hizi hadith ni hizo, zijibu sasa, hasa hiyo ya kwenda nchi za mbali na kuoa na kuolewa, walenda kumuoa na kuolewa na nani?
Safi kabisa ili nizijibi hoja hizi lazima kwanza uniambie habari hizi mmezipata wapi usiniambie tu watu wanahoji lazima tujue ukweli wa hoja zao maana katika vitabu vyetu hasa vya uislamu sijaona habari hizi.

Kwahiyo mkinionyesha kama zipo katika kitabu chochote katika vitabu vya Uislamu nitajibu hoja hizo.

Ila bado uba deni nakudai, nataka mtuambie na mtuthibitishie ya kuwa hizi hadithi ni za uongo.

Ila nitazidi kuwaona nyinyi ni watu wajinga wa muda wote, kama hizi habari mnazo ziweka humi kama hoja zenu hamjui zinapatikana wapi ? (Nacheka sana).

Nimemaliza kazi yangu ni mimi Zurri.
 
Back
Top Bottom