Safi kabisa hili ni kwa habari na si kwa hadithi, tatizo ulilivagaa tamko Hadithi bila kujua mipaka yake, na lazima ukosee kama unavyo kosea sasa.
Sasa unaponukuu Hadithi ujue ya kuwa wewe umesikia mahala au umesoma mahala, sasa katika uhakiki wa habari lazima utuambie umeitoa wapi hiyo habari kisha tunaiweka katika mizani, na kupembua mbichi na mbivu, sababu si kila habari ni hadithi.
Mathalani hicho ulicho kisema wewe kwangu mimi ni kipya, sababu mimo ni mtu makini na nimesoma elimi ya uhakiki wa habari lazima ni kuhoji ili nijue naiweka katika kundi gani habari hii, je inaingia katika hadithi, au ni visa vya wana wa Israeli au pauka pakawa.
Ndoyo maana nilikwambia hapo awali ya kuwa habari uliyo itolea mfano inanipa maswali mengi, na ndiyo maana huwa tunawaambia habari hizi mtuambie mmezitoa wapi, lakini mwisho wa siku mnatokomea sababu katika vitabu vyetu habari hizi hatuzioni.
Lakini pia mnaonyesha udhaifu mkubwa sana na kutokuwa makini kwa kuchukua habari bila kuzihakiki na kuzinasibisha ba watu fulani, watu wenye akili timamu na umakini hawapo kama mlivyo nyinyi hivi.
Kwahiyo nahitimisha kwa kukwambia hivi, rekebisheni viti vyenu kwanza kabla hamjavitia nakshi. Mwenzako mmoja amekimbia na najua hatarudi tena sababu kazi niliyo mpa ya kuniletea andiko linalo onyesha kukaidi kwa Malaika. Sasa msiwe na sifa kama ya sponchi likiwekwa kwenye mkojo litanyonya mkojo, likiwekwa kwenye maziwa litanyonya maziwa, likiwekwa kwenye maji litanyonya maji.