Hapa kuna mambo mawili wengi mmechanganya, kuna majadiliano na maafikiano. Inawezekana kabisa katika baadhi ya mambo Rais akamuita Makamu wake wakakaa kujadiliana. Haimaanishi kwamba Rais analazimika kukaa na Makamu wake kujadiliana kila jambo.
Lakini suala jingine ni kwamba, katika majadiliano hayo kama ikampendeza Rais kumuita Makamu wake wakajadili basi Rais hafungwi na ushauri wowote unaotolewa na Makamu wake.
Kwenye majadiliano na wakuu wetu wa kazi Mara nyingi kuna mengi yanaweza kujitokeza na katika hayo huwa unatokea kabisa boss wako akaamua kutokubaliana na ushauri wako simply ana maono yake especially kulingana na cheo alichonacho na legacy anayotaka kuiacha.
Kilichomkuta Rais Samia Suluhu Hassan sio kwamba tu alikuwa ushauri wake haupokelewi lakini waweza kuona wazi kwamba hakuwa kabisa na mtazamo wa approach za mtangulizi wake.
Mama approach yake ni diplomatic na anapenda majadiliano ukiangalia meko hakuwa mtu wa majadiliano akikupigia simu ni kuulizia jambo fulani au kukupatia maelekezo fullstop.
Jiwe hakutaka ushauri hata wa watangulizi wake waliompa uwaziri kwa miaka yote, alikuwa hapokei simu kabisa aliona Tanzania ni kama yake sasa. Only mtu aliyekuwa anamuweza ni uncle Ben.
Jamaa alikaa almost mwezi mzima hajaform baraza la mawaziri kajifungia tu pekee hataki hata Makamu wake ashiriki, mpaka mzee Mkapa alipoenda kumwambia usipotangaza baraza mapema kuna bunge fupi la November to December linakuja mawaziri wako watashindwa kutetea serikali watapigwa Pini, ndio akastuka na kutangaza.
Unaweza kuona huyu mtu alikuwa anajiona yeye ndio anafaa kushinda mtu yeyote. Kidogo hapa mwishoni naona na afya ilianza kuwa mbaya alikuwa anawaachia wafanye wenyewe wateule wake na ndipo walipompiga hela ya kutosha.
Nachoweza kusema ni kwamba, mama hakuwa kwenye nafasi ya kulazimisha jiwe apokee ushauri wake. So kwa sasa mwacheni afanye yake nae alikuwa na maono yake na kila mtu ana maono yake lakini bahati mbaya hatuwezi kuwa wote viongozi.
Kwa sasa legacy ni ya mama anasema KAZI IENDELEE let's hope nae atatupeleka kwenye stage nyingine nzuri zaidi.