Je, hayati John P. Magufuli alidanganywa na vyanzo vyake vya habari? Maana sasa ni kama kufedheheshana

Je, hayati John P. Magufuli alidanganywa na vyanzo vyake vya habari? Maana sasa ni kama kufedheheshana

Mkuu kila zama na mambo yake na majira yake,usiishi kwa kukariri,kuna mada moja ilitolewa na mwanajf mmojavkuhusu Starlini waRussia .Akipofariki makamu wake akawa anabadili mambo,mmoja wa wajumbe akatuma memo kama kutoridhishwa.Mkuu akauliza nani katumavhuu vujumbe nimjibu?!Kimya.Akasema hata mimi nilikuwa nakaa kimya.Utakuwa umeekewa.🙆🙆🙆🙋
Hakuna aliyepinga mabadiliko, bali tunahoji haya madhaifu yanayoanikwa. Maana tulikuwa tunaambiwa kila kitu kiko sawa.
 
Au maza kashalishwa kaseti na yule mzee mwenye tabasamu muda wote,

au maza nae alimchukia hayati kama walivyofanya mabeberu?

Au maza kafurahi paka ametoka?

Au maza anajua yaliyomkuta mzee?

Au maza, au au au
Tulia ww kila zama na kitabu chake
 
JPM atabaki kuwa kiongozi bora wa kizazi hiki cha sasa ukitoa Nyerere

Najiuliza hv kazi ya makamu wa Raisi ni nini kwa hali inavyooneka tunawalipa watu mishahara na kuwatunza wasiotekeleza majukumu yao aiwezekani makamu wa Rais ambae umezunguka nchi nzima kwenye kampeni tena ukala kiapo cha kumshauri Raisi kwa hekima leo tunashangaa na ww unashangaa mambo yaliofanyika na kuyabadili kana kwamba hukushiriki ktk kuanzishwa kwake.
Jiwe alikua anafanya kazi peke yake yaani ni one man show. Hao wengine walikua wanafata matakwa yake
 
Ubora wake watakuja kuujua wajukuu zako si ww kama umefoji cheti na kuwazibia nafasi waliokesha miguu wameweka kwenye maji ukafukuzwa lazima utamuona ni mbaya lakini wale waliokuwa wanalia na kujipanga barabarani wanajua ubora wake
Hoja hapa sio kufukuza wenye vyeti feki. Tunahoji juu ya madhaifu yanayoanikwa sasa ina maana hakuwa anaambiwa ukweli?
 
Kumbukumbu zinabainisha ata JK alipomaliza muda wake maoni na michango katika mitandao yalikuwa yakionesha kama vile hakufanya chochote..ngoja tuone Mama kama atawakomesha mafisadi..
Ngoja tuone kama ajira zitaongezeka na gharama za kujiajiri kama zitashuka..
We kijana una umri gani? Madhaifu ya Jakaya yalikuwa wazi kabisa hata alipokuwa madarakani.
 
Suala la elimu bure kwa nchi hii wala sio jambo la ajabu kabisa sisi tumesoma elimu huku tukinywa uji,daftari likiisha unaonda kwa mwalimu wa soma anasaini unaenda zako stoo unapewa daftari,tulikuwa hatukai chini kama sasa hivi dawati moja wanafunzi wawili na madawati yanabaki ya kumwaga tu
Nadhani kipindi hicho we bado ulikuwa kwenye bomba
Labda ulisoma wakati wa Nyerere! Elimu ya bure ilitoweka kuanzania mwaka 1985, ikaanza kama mchango wa elimu Sh20 na kadri siku zilivyokwenda ndipo karo ilikuwa inaongeza; imepita miaka 30 ndipo elimu ya bure ikarudi tena.
 
Shida unaangalia Enrollment sio quality ya elimu. Yaani ina faida gani 98% wawe enrolled alafu takwimu zinaonyesha zaidi ya elfu 50 wana drop kila mwaka sababu ya ujauzito. Let alone umesikia wanaomaliza la saba hawajui kusoma wala kuandika, well hakuna madawati, Ufaulu la saba kati ya private na public n.k hivi hayo mambo hamyaoni au nyie mmekazana na enrollment tu.
Hii takwimu ya kuwa enrollment ni 98% alafu 50% wanaacha shule kwa ujauzito uliipata wapi?

Hilo la kumaliza shule huku hawajui kusoma utakuwa upo sawa.
 
JPM atabaki kuwa kiongozi katili, mwizi na muongo kuliko marais wote hapa nchini.
Kweli vizazi havitamsahau.
 
Mimi binafsi hainingii akilini aliyekuwa msaidizi wako mkuu kama makamu wa rais afanye mabaliko makubwa kama haya kwa muda mfupi.

Kwamba malalamiko ya ukusanyaji kodi hayati JPM hakuyasikia? Malalamiko juu ya wawekezaji kusumbuliwa? Masuala ya ajira na mshahara unaotakiwa?
Je, hawaaminiki tena?
Huyo jamaa alikuwa jeshi la mtu mmoja
 
Hakuna aliyepinga mabadiliko, bali tunahoji haya madhaifu yanayoanikwa. Maana tulikuwa tunaambiwa kila kitu kiko sawa.
Hata JPM alikuwa sehemu ya Baraza la Mawaziri la Rais Mkapa na akadumu hadi baraza la Mawaziri la JK , amekaa 20 years as a minister, akauza nyumba zote za serikali, na akajiuzia na nyingine akawapa mahawara zake, huyo huyo alipoingia JK ikabidi JK ahangaike kujenga nyumba mpya maana viongozi wapya walikuwa wanakaa mahotelini na kwenye appartments and it was expensive and too risky.

Huyohuyo alipokuja kuwa president 2015 akaanza kuibua ya wenzake na kuongea shit nyingi sana na kujionyesha yeye ndio mzalendo na sio mwizi wala sio jangili.

Labda nikuulize, je unajua kwamba alikuwa waziri kwa muda wote niliosema hapo juu?

Na kama jibu ni ndio, je kwa nini nae aliibua hayo mambo alipoingia yeye wakati nae alikuwa sehemu ya hizo Serikali akiwa kwenye council ya ministers ambapo alikuwa sehemu ya maamuzi na baadhi yake yalikuwa na utekelezaji chini yake?

Je utabisha tukisema kwamba nae alikuwa mnafiki na amewasaliti watangulizi wake kwa kuamua kufuata njia zake za uongozi baada ya kuwa Rais na kuanza kuexpose mambo ambayo yalishapita?

Je nae tumuite msaliti?

Na kama jibu hapo juu litakuwa hapana, then kwa nini unamuita Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan majina ya kipuuzi??? Ni hayo machache tu.

I submit.
 
Mimi binafsi hainingii akilini aliyekuwa msaidizi wako mkuu kama makamu wa rais afanye mabaliko makubwa kama haya kwa muda mfupi.

Kwamba malalamiko ya ukusanyaji kodi hayati JPM hakuyasikia? Malalamiko juu ya wawekezaji kusumbuliwa? Masuala ya ajira na mshahara unaotakiwa?
Je, hawaaminiki tena?
Haya yote yanatokea hata shingo haijakatika
 
Kipindi unachosemea ww Watanzania hawafiki milioni 15 wanaenda shule ni chini ya 4% sasa hv mpo milioni 60 wanaoenda au waliofikisha umri wa kwenda shule 98% wanaenda shule uoni kuna tofauti kubwa ?
Hata uchumi wakati huo ulikuwa upo chini Sana na mazingira magumu mnooo,Sasa kwanini iliwezekana na kwa nini ishindikane leo?
 
JPM atabaki kuwa kiongozi bora wa kizazi hiki cha sasa ukitoa Nyerere

Najiuliza hv kazi ya makamu wa Raisi ni nini kwa hali inavyooneka tunawalipa watu mishahara na kuwatunza wasiotekeleza majukumu yao aiwezekani makamu wa Rais ambae umezunguka nchi nzima kwenye kampeni tena ukala kiapo cha kumshauri Raisi kwa hekima leo tunashangaa na ww unashangaa mambo yaliofanyika na kuyabadili kana kwamba hukushiriki ktk kuanzishwa kwake.
Kama ushauri wake ulikua hausikilizwi je
 
Back
Top Bottom