Anti-ship warfare ni ngumu zaidi na ya gharama. Meli ina countermeasures nyingi especially hii Anadolu inayoenda kuwa flagship ya Turkish Navy.
Mpaka uweze kuipiga meli inabidi uisogelee. Anadolu ina air defense system itaona ndege zinazosogea kufyatua air launched anti ship missiles. Meli yenyewe inakuwa na ndege zake palepale za kuilinda, hapa tunazungumzia drone carrier ambayo ni kama aircraft carrier ndogo.
Ingekuwa ni true carrier kama za China au Marekani zinazojitosheleza ingeenda na carrier battle group ikisindikizwa na submarine kwa ajili ya submarines za adui, destroyer kwa kupigia meli za adui, ndege za electronic warfare kuzuia mawasiliano ya adui, ndege ya airborne early warning kujulisha movements za silaha za adui, fighters kuzuia ndege za adui, helicopters kama sehemu ya anti-submarine force na za rescue missions, replenishment ship na mengineyo.
Melivita kubwa hazipigwi kirahisi hivyo na hata zikipigwa bado ni muhimu. Ni sawa useme tusipande magari kwa sababu yanapata ajari.
Hata hivyo leo wamefanya kuizindua, inahitaji process nyingine kuwa commissioned na Navy baada ya kupitia ukaguzi na zoezi la miezi kadhaa kupima mifumo yake. Kama Navy
View attachment 2584660 itakuta haikidhi inaikataa mpaka kampuni zinahusika pamoja na wizara ya ulinzi ziikamilishe. Na Anadolu imezinduliwa mapema kwa sababu za kisiasa, uchaguzi mkuu unakaribia na Erdogan anataka aitumie kama achievement ila in reality bado kwangu mimi naona inahitaji si chini ya miaka miwili kuwa relevant.
Kingine kuna ndege zinahitajika kutumika hapo ila hazijakamilika. F-35 ilibidi itumike kwake ila Uturuki iliondolewa kwenye programu. Drone yao TB-3 ya Bayraktar iko tiyari nimeona imepokea order kutoka kwa foreign customers mapema sana, labda kutokana na mafanikio ya TB-2. TB-3 ndio nyingi na lengo kuu la hii drone carrier ila bado meli inahitaji ndege za kuilinda
Sasa hapo Kizilelma ndio kwanza sijui imefanya test ya taxiing mwaka huu au jana mwishoni. Bado sana hiyo naamini miaka kama mitatu ijayo itakuwa bado. Ndege nyingine ya Hurjet ni light attack sidhani kama itakuwa ngumu ukizingatia Uturuki wana advanced trainer jet wanaongeza vitu vingine. Ndege za kutua kwenye carrier zina changamoto kidogo, unakuta runway haifiki urefu wa pitch ya mpira.
Classification ya Anadolu ni mpya kwenye majeshi ila Iran inayo meli kama hiyo moja imejaa kutu ilichukua meli kubwa ya kiraia ikakata sehemu yake ikajenga deck. Ukiiona tu unaona imetengenezwa kivyakevyake. Uturuki ndio wametoa class mpya, meli mpya mahususi tangu inaundwa ingawa walibadiki gear angani.
Classification yake kwa majeshi mengine ingekuwa amphibious ship kama Mistral ya Ufaransa mbili ziliuzwa Misri, hii ni helicopter carrier. Japan na South Korea wanazo carriers ndogo na nzuri sana zile nazo zinaingia classification hii.