Uturuki na Iran hizi unazoona leo hazipendani. Na ndicho nilichoandika tangu mwanzo. Kutopendana sio kumaanisha kuna uadui, wala usijejidanganya ukadhani Iran inafurahia Turkey kupiga hatua kijeshi, vilevile Turkey haifurahii Iran kupiga hatua.
Nakupa mifano. Kwenye mapigano ya Nagorno-Kabarakh mwaka 2020 Uturuki iliipa misaada Azerbaijan, Iran ikaipa msaada Armenia. Uturuki inauza silaha kwa Ukraine, Iran inauza kwa Urusi. Syria kwenye civil war Uturuki ilikuwa inapigana na jeshi la Syria ndani ya Syria kule Kaskazini mwa nchi ambako kuna Wakirudi, Iran ilikuwa inasaidia jeshi la Syria kupigana na waasi na ISIS. Mwanzoni vita inapamba moto Uturuki ilikuwa inanunua mafuta ya ISIS baadae Urusi wakalipua miundombinu ile ya mafuta.