Je, hii silaha mpya ya Uturuki inakwenda kubadili sheria za mchezo?

Toka lini copter au ndege vita iteke eneo na kulikalia??[emoji15][emoji12][emoji38][emoji38]
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha

Ila mchina muoga sana, nimeona jana BBC wakisema China imemaliza mazoezi yake huko mpakani mwa Taiwan.
 
Dah!.. Uturuki wanakuja juu sana kwenye hii defense industry miaka ijayo atakuwa military power nini ?
 
Marekani inahamu Sana kuzichapa na china. Naona wanatafuta sababu tu ya kuivaa china. Pengine lengo ni kuishusha kiuchumi. Wataalamu hebu tupieni neno kuhusu hilo nini hasa marekani anakitafuta kwa china?
 
Hakuna nchi dunia ya leo wanaeza kumpiga mchina ukiona nchi Hadi biological weapons anaoagopeka ni hatari Sana China anaeza pukutisha L.A yote kwa amplified moja ya korona version...
 
Natamani sana kuona vita ya Taiwan na China
Au Marekani na Iran
Pro NATO mmarekani kawaharibu,, eti unatamani kuona vita,, siku ukipigwa tu na hata bomu la machozi au mimaji ya kuwasha nadhani utarudi kufuta coment yako hii
 
Dah!.. Uturuki wanakuja juu sana kwenye hii defense industry miaka ijayo atakuwa military power nini ?
Wanataka kuwa imara eneo lako halitaki ukae kizembe. Wapo na Iran pembeni huwa hawapendani, wapo na Greece maadui wa kihistoria na wana strait inayopitisha meli kwenda Russia na Pacific na kurudi Ulaya.
 
Hakuna nchi dunia ya leo wanaeza kumpiga mchina ukiona nchi Hadi biological weapons anaoagopeka ni hatari Sana China anaeza pukutisha L.A yote kwa amplified moja ya korona version...
China anaogopeka kwa biological weapon gani mzee. Corona yenyewe ugonjwa wa kitoto huu unakuzwa na media, kwanza umeua Wachina wengi kuliko Wamarekani. Marekani ina stockpile ya bio weapons kwenye labs zao za miongo na miongo iliyopita, Russia ana stockpile ya Cold war enzi za USSR mahabara zimefungwa uko. Virusi kama Botulinum vimegandishwa uko uje uwatishe na ugonjwa unaodhibitiwa kwa tangawizi
 
Leo ndo umeona hivyo baada ya Ukraine kuwapelekesha?
Ametupelekesha akina nani kwani mm ni Mrusi au?
kwani Urusi amesha shindwa vita mpaka useme anapelekeshwa?
Urusi tutajua ameshindwa vita mpaka pale atakapo kimbia kwa aibu kama Marekani alivyo kimbia Vietnam, Afghanistan na Somalia baada ya kipigo cha mbwa koko.

Au tutajua Urusi amepelekeshwa na kushindwa iwapo ataya tema maeneo aliyo yateka kutoka Ukraine kama Israel ilivyo itema rasi ya Sinai mwaka 1972 baada ya kupokea kipigo kutoka Misri au kama alivyo itema ardhi ya Rebanon baada ya kipigo cha aibu kutoka kwa Hizibullah mwaka 2006

Au ukitaka kujua kuwa vita sio lele mama iulize Israel nn kilicho ikuta baada ya kujaribu kuivamia Gaza mwaka 2014 kwa lengo la kuiangamiza Hamas.

Au ukitaka kujua vita sio lele mama iulize Saudia na vibaraka wake kimewakuta nn baada ya kiwaparamia waasi wa kihuthi.

Ukitaka kujua vita sio lele mama iulize Urusi ilitumia miaka mingapi mpaka kuwashinda waasi wa kichechinia na ililipa gharama kiasi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…