Je, huyu Rais wetu wa sasa ni Vasco Da Gama mwingine? Ziara za nje zimekuwa nyingi sana kama enzi za Awamu ya Nne

Je, huyu Rais wetu wa sasa ni Vasco Da Gama mwingine? Ziara za nje zimekuwa nyingi sana kama enzi za Awamu ya Nne

Kukopa ni akili ya kimasikini sana.
Unakopaje sasa wakati raslimali tele.
Hii "mindset" ya kukopa kama taifa ni kwa wenye ufinyu wa mawazo na akili za kimasikini pamoja na wale wavivu wa kujishughulisha kijumla.

Wale wa kule tulioungana nao tunajua kabisa kuwa vichwani ndio hivyo tena na kujishughulisha ndio kabisaa sio sehemu ya maisha yao. Wao ni wapenda mteremko tu.

Rasilimali zote hizi bado twakopakopa tuu as if hiyo mikopo imewahi saidia nchi yoyote ya ulimwengu wa tatu kuendelea.
 
Mama anatakiwa atengeneze long term plan na leadership ambayo haitategemea aina ya rais. Yaani aangalie ni namna gani rasilimali tulizonazo zinaweza ku finance maendeleo yetu. Yeye badala yake anaendq kukopa mikopo ya ujenzi wa madarasa???? Yaani unaenda kukopa hela za kuwekea rehani resources zetu??? Nadhani ile timu ya wachumi angeitumiq ila kwa sasa anapuyanga tu Mama. Mungu atusaidie maana huko mbeleni watoto wetu watatushangaa sana maana watakuta kila rasilimali ya nchi tumekikopea
Kutengeneza "longterm plan na leadership ambayo haitategemea aina ya rais" inataka kuwekwa kwenye katiba. Ndio maana tunasema katiba mpya ni muhimu sana sana kama kweli tunataka tutoke kwenye taifa masikini ombaomba la hovyo.
 
Yaani mi mpaka machozi yananitokaga nikifikiria. Sasa hivi nasikia kuna mradi vyuo vikuu eti world bank imeikopesha serikali kujenga miundombinu ya kuongeza idadi ya enrollments vyuoni ili kuongeza idadi ya wanaofika na kumaliza vyuo vikuu Tanzania. Sasa unajiuliza sasa hivi tu graduate waliopo mitaani bila kazi ni wengi, unaenda kukopa tena ili kuongeza idadi ya graduate wasiokuwa na kazi unategemea nini?????? Maana yake hao hao wazungu watakuja tena na mpango wa kukukopesha ili utatue tatizo la migogoro ya vijana wasiokuwa na ajira kuandamana na wakiandamana serikali ikiwapiga itasema ohh demokrasia haki za binaadamu kiasi kwamba nchi inakuwa dependents na nini wanataka wazungu
Maji yanayopotea baada ya mvua kunyesha mikoani,kama yangevunwa na kuhifadhiwa na kutumika kwenye kilimo cha umwagiliaji,hakika kusingekuwa na uhaba wa ajira.

Tengeneza mabwawa,hifadhi maji,tengeneza schemes za umwagiliaji,ingiza nchini zana za kisasa za kilimo,wakopeshe vijana walipe miaka 5 mpaka 10 kwa riba ndogo,wezesha watanzania waongeze samani hayo mazao kwa kuyachakata hapahapa na kuyapack vyema na hatimaye kuyauza huko nnje yakiwa yatari.

Kama ambavyo ndugu Chige aliwahi andika kuhusu "multiplier effects" za kwenye LNG, ndivyo ilivyo pia kwenye kilimo.
 
Ukishakuwa mtumwa huwezi kutoka, utaendelea tu kuwa mtumwa. Waacheni watoto wa watumwa waendelee kuwa watumwa kama wazazi wao.
 
Pumbavu zako, wakati wa kikwete alisafili sana sasa nini kilitokea cha aajabu hapa tanzania?
Sema hata kimoja?
Kama ni kuonana na wafanya biashara alionana nao saana wote wa ulimwenguni lakini nchi bado ni masikini.
Sasa huyu ataonana na yupi ambae kikwete hakuonana nae?
Good question
 
Pumbavu zako, wakati wa kikwete alisafili sana sasa nini kilitokea cha aajabu hapa tanzania?
Sema hata kimoja?
Kama ni kuonana na wafanya biashara alionana nao saana wote wa ulimwenguni lakini nchi bado ni masikini.
Sasa huyu ataonana na yupi ambae kikwete hakuonana nae?
Jiwe alifanya nn zaidi kuigawa nchi vipande vipande na kupandikiza ukabila?

Mbona nchi bado ni maskini pamoja na kwamba alikuwa hasafiri?
 
Yule jiwe a.k a mzimu wa sukuma gang ndiyo amesababisha yote haya. Aliua biashara zote kubwa na ndogo kwa kupora fedha za watu. Vyanzo vyote vya Kodi vikafa. Akawa anakopa hovyo tena kwa siri kubwa mikopo ya kibiashara ambayo riba zake ni kubwa.

Mama hana namna lazima asafiri ili apate mikopo, maana nchi imeachiwa matatizo na madeni makubwa na jiwe.

Asante mama endelea kuinusuru nchi.
Kweli una wazimu
 
Fedha iliyokopwa haijajenga madarasa tu imeenda pia kwenye miradi ya maji, ujenzi wa vyuo hasa veta, kuimarisha miundombinu kwenye hifadhi zetu, kuimarisha utoaji huduma wa afya kwa ujenzi wa ICU, EMD kununua mitambo
.
Na fedha hii ilikua muhimu kwani iliingizwa kwenye uchumi ili kupunguza maumivu yaliyotokana na janga la uviko-19
Pia imeenda matumboni mwa wale wala urefu wa kamba zao
 
Mwacheni asafiri kwani Kuna vujipesa huwa vinapatikana huko.
 
Wafute kwanza hiyo kasi yao ya ugaidi wa michongo ili wawekezaji waje kuwekeza wakiwa na amani ya moyo,na uhakika wa usalama wa uwekezaji wao.
Uamsho walipokuwa na kesi kama hiyo mbona hatukuona kuwa ni kikwazo kwa wawekezaji?
 
Awamu ya nne tulishudia Jakaya kikwete akifanya ziara za nje huku akisahau kabisa masuala ya ndani ya nchi yake mpaka akapachikwa jina Vasco Da Gama.

Awamu hii nayo naona ni mwendo uleule. Juzi alikuwa ulaya. Leo yupo Uarabuni.

Hii ishu ya Uarabuni asingeweza kuwakilishwa hata na balozi?
View attachment 2131649View attachment 2131650
Unataka aishi kama mnyama? Kama alivyokua dikteta uchwara
 
Back
Top Bottom