Je, inawezakana kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mahusiano(affiliation) yoyote na madhehebu ya kidini?

Je, inawezakana kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mahusiano(affiliation) yoyote na madhehebu ya kidini?

Katika Uislamu hilo unalolisema halipo, na hata akili ya kawaida inapingana na hilo.

Hapo kuna swali la kujiuloza, je Ibada ni nini? Utajuaje kuwa kuwa unayoifanya ni ibada ambayo aliyekuumba anairdhia? na utajuaje kuwa unaifanya katika namna ambayo anairidhia?

Pamoja na kuwa kila muislamu anaamini kuwa Mungu yupo(Allah) -kwa sababu hilo linadhibitika hata kiakili- lakini Allah tunamfahamu zaidi na kufahamu namna sahihi ya kumuabudu kupitia mafundisho yake ambayo ametufundisha kupitia mtume wake Muhammad -swalla llahu allaihi wa sallam-.
 
Sasa Mungu wa kweli anapatikana dhehebu gani, maana nimetumia zaidi ya miaka 20 kwenye dhehebu ambalo nilidhani ndo dini ya kweli lakini baada kufanya utafiti nimevunjika moyo na mambo ya dini....

Kwa kweli kama Mungu atagawa uzima wa milele kwa kutazama mafungamano na hzi dini naona kabisa ntashndwa...
Wewe umetumia vigezo gani kujua hilo dhehebu siyo la kweli?
 
Kwa kuwaza hivyo tu,inamaanisha una wito,ila hujui namna ya kuutekeleza.

M-ngu hajawahi kuwa wa dhehebu au kikundi flani,M-ngu ni wa mtu binafsi,ndio maana utasikia anajiita M-ngu wa Ibrahim au Mungu wa isaka,ukifatilia kipindi cha ibrahim,kulikuwa hakuna ukristo,judism wala uislamu lakini Ibrahim alimwabudu M-ngu,hata kwenye agano jipya Yehoshua(Jesus) anasema,M-ngu haabudiwi hekaluni wala juu ya mlima Bali anaabudiwa katika roho na kweli,simply worship is personal and never a public act.

Ngoja nifupishe maelezo

Fanya mambo haya matatu,utakuja kunishukuru.

1.hilo wazo la kuwa ATHEISM achana nalo kwasababu,kutokana na maelezogu.

2.hilo wazo lako la kuanzisha hizo ibada za hapo nyumban yako,usiliache,hizi dini zote zilianzia nyumbani kwa mtu na m
Mkuu umesema nisipopata mwongozo ntapotea...

Naomba uwe wa kuniongoza katika hili.. Pm haifunguki lakn email ipo

natafutamaisha420@gmail.com
 
Wewe umetumia vigezo gani kujua hilo dhehebu siyo la kweli?
Mkuu mambo ni mengi sana kwa uchache tu,

1. Unabii usiotimia.
2.concealed child sexual abuse cases.
3.unafiki miongoni mwa viongozi wa kidini
4.doctrinal changes, kama jambo n kwel na inspired by GOD linatakiwa liwe vile vile jana, leo na kesho.
5. mpaka nimeona kuwa katika hstoria ya hii dini kuna wakati homosexuality haikuwa considered as adultery
6. Mind control.
 
Hakuna MUNGU wa waIslam na wakristo.Ila kuna nabii Mohamed na MASIHI Issa bin Mariam
Hawa walitumwa na MUNGU kwa kazi maalum.
Aliyetangulia alikuwa Masihi Issa Bin Mariam wayahudi mnaowasifia walivyomsulubu ikapita miaka 570 MUNGU akamtuma Mtume Mohamed.
Issa Bin Mariam alileta Injili na Mohamed alileta Quoran.
Wote hawa wanatokea tawi la Nuhu,Ibrahim na ndo maana hizi dini mbili zinaitwa dini za Ibrahim
Huyo mnayemuita YESU ni jina tu liloletwa na Wazungu Jesus waswahili tukasema YESU.
ila ujue nikuambie jina la nabii yeyote linatakiwa litamkwe kama liivyo.
Ndio maana muislam aliyebobea kwenye dini hawezi kukwambia anamuabudu YESU ila atakuambia anamuabudu Issa Bin Mariam.Na waislam wanakubali alizaliwa bila kuwa na baba wa kibayolojia na ndio maana wanatamka Issa bin Mariam.Ila Mohamed alizaliwa na baba na mama.
Mwisho wa yote MUNGU wa wakristo ni huyo huyo wa waislam

Hizi ni Propaganda tuu za kila mmoja kutetea upande wake..
Hapa yenyewe unazungumza katika upande wa Mwislam Ila bado ukweli ni kuwa MUNGU wanaomsema wakristo na Waislam Ni Tofauti kabisa.

Angekuwa mmoja Asingekubali utaratibu wa kumubudu utofautiane.
 
Mkuu pm yangu haifunguki nadhani kwa sababu ya simu ninayotumia ni hz tecno zenye opera mini, tuwasiliane kwa email.. ikishndikana ngoja nitafute simu nyngne,
 
Wakuu niaje?

Natumai mko poa...
Twende kwenye mada tajwa hapo juu... Je kuna uwezekano wa kumuabudu Mungu pasipo kuwa na mafungamano na haya madhehebu ya kidini?

Siku za hivi karibuni nimefanya utafiti wa kina kuhusu madhehebu ya kidini hasa nililokuwa na mafungamano nalo.. Aisee ni mambo ya kusikitisha sana.. Binafsi naamini Mungu yupo japo nina wasiwasi na utu wake(personality) namuona kama atakuwa anafurahia kuona wanadamu na viumbe wake wakiteseka..

Vyovyote vile bado naamini yupo..

Sasa naombeni mnisaidie maoni na mapendekezo(tips) za kumuabudu bila kujihusisha na hizi dini ambazo ukizifuatilia kwa undani utapatwa na sonona.

Niliwaza kuwa na vipindi vya ibada hapa kwangu, kama kuimba mwenyewe, kusoma biblia na kusali.. Je ni sawa?

Natanguliza shukrani....
Fungamana na Yesu, si madhehebu! Hata ukienda kuabudu kwenye madhehebu uwe unafuata kujifunza toka kwa wengine, si kufuata na kufungamana na madhehebu yao. Hakuna madhehebu yanamwokoa na/au kumpeleka mtu mbinguni - ni Yesu pekee.
 
Halafu sisi wachungaji sadaka yake tutakulaje..?????
🤣🤣🤣

Sindio ktk dini ya kiislam unaambiwa Mwanaume Anapaswa haswaa kusali msikitini !! !? Akisali msikitini Mema yake Yana double value Kwa Mungu , kumbe ni strategy ya kuwafanya wanao Sali msikitini iweze kuwa rahisi kupatikana Kwa wingi ili waweze kusupport movement za kugharamia shughuli za kidini mfano msikiti unahitaji kulipiwa maji umeme etc mfano wakisema kila mtu Asali home kwake huo msikiti utajiendesha Vipi !!!? So Wanashindwa kuweka wazi Hilo wanatumia Maneno Mazuri kulainisha mioyo ya waumini ili waweze kufanikisha goals zao

🤣🤣🤣🤣🤣

Kuna Hiyo sasa ktk mafundisho Yao ya kiimani wana ambiwa ukienda kuhij Makkah ikitokea ukafa huko huko au ukafa ndani ya ndege wakati upo njiani kwenda huko basi wewe Moja Kwa Moja peponi 🙌🙌🤣

Yaani mtu anashindwa kuelewa kuwa huo ni mpango mkakati wa kufanyia promotion Hiyo culture ili Wanao amini ktk Hiyo Imani wapate kuipa nafasi zaidi ktk Maisha Yao so unakuta people zina amini kabisa

Kwa kweli dini kitu cha hovyo Sana NI scamm
 
Fanya jaribii hili
Chukua sisimizi wa4 waweke sehemu pana sana mf kwenye kiwanja cha mpira katikati. Wape chakula na mahotaji yote ksha wambke zaeni nkaongezeke.
Wataanza kujiuliza kwani tumewekwa hapa kufanya nn, Pili mwisho wa mipaka yao ni upi mana wakitembea hawafiki mwisho, kwann wamewekwa kwenye shida ikiwa mungu yupo (wewe upo ila wanatembea umbali mrefu badala ya kuwapa mabawa)
Ndio mungu anavyotuona na tunavyomwona na hali ilivyo.

Halafu yeye anasema usisumbukie utakula nn mbona ndege nawalisha halafu ww unaogopa kuzaa watoto kibao kwsbb wewe mwenyewe kula ni mandazi na enegy.
Yeye amekaa juu anakuangalia, anamwaga maji unakunywa anatupa mkate unakula na anakuangalia unavyomchunguza kumbe amelaa juu anakuangalia tu na kucheka
 
Katika Uislamu hilo unalolisema halipo, na hata akili ya kawaida inapingana na hilo.

Hapo kuna swali la kujiuloza, je Ibada ni nini? Utajuaje kuwa kuwa unayoifanya ni ibada ambayo aliyekuumba anairdhia? na utajuaje kuwa unaifanya katika namna ambayo anairidhia?

Pamoja na kuwa kila muislamu anaamini kuwa Mungu yupo(Allah) -kwa sababu hilo linadhibitika hata kiakili- lakini Allah tunamfahamu zaidi na kufahamu namna sahihi ya kumuabudu kupitia mafundisho yake ambayo ametufundisha kupitia mtume wake Muhammad -swalla llahu allaihi wa sallam-.
Kwanini mafundisho ya Yesu na uislamu yanakinzana pakubwa sana hasa kuhusu matendo ya kumuabudu Mungu namaanisha sala na kuswali
Lakini makatazo ni Yale Yale Kwa dini zote
Na zote zimesisitiza huruma na kusaidia watu

"Si wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi, bali wema ni wa yule anayemwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na Malaika, na Vitabu, na Manabii; na anawapa mali yake, kwa kuipenda, jamaa, mayatima, masikini, wasafiri, waombao, na kwa kuwakomboa watumwa...”
— (Qur'an 2:177

Dini iliyo safi, isiyo na uchafu mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwajali yatima na wajane katika dhiki zao, na kujilinda na dunia ili isikuambukize.”
— (Yakobo 1:27)
 
Ahsante mkuu..
Dini niliyokuwemo kuna indocrination ya hatari, maana tumekuwa tukiambiwa kuwa ndo dini ya kweli, ukitoka basi ujue umemuacha Mungu na ujiandae kuharibiwa..nilikuwa humo kwa miaka 20, haya yameniathiri mpaka nimeacha kusali kibinafsi nahsi labda kwa kuwa nimeacha mambo ya dini basi hata Mungu atakuwa asikilizi...
Hizo dini ni utapeli mtupu Achana nazo just be a god person with kindness inatosha
 
Fungamana na Yesu, si madhehebu! Hata ukienda kuabudu kwenye madhehebu uwe unafuata kujifunza toka kwa wengine, si kufuata na kufungamana na madhehebu yao. Hakuna madhehebu yanamwokoa na/au kumpeleka mtu mbinguni - ni Yesu pekee.
Afungamane na Yesu kuliko Mungu aliyemuumba?
Kwahiyo nabii Adam kule bustanini alikuwa na Yesu maana kule ndiko creation ya mwanadamu ilikofanyika
 
Afungamane na Yesu kuliko Mungu aliyemuumba?
Kwahiyo nabii Adam kule bustanini alikuwa na Yesu maana kule ndiko creation ya mwanadamu ilikofanyika
Kwenye Ukristo kuna tofauti kati ya Mungu na Yesu kwenye kila nyanja.

Mfano kwnye nyanja ya Sheria...

Mungu alisema lipiza jino kwa jino kwa adui yako, ila Yesu akasema wapendeni adui zenu.

Mungu alisema wachawi na Wanzinzi wauawe, ila Yesu akasema viacheni vyote magugu na Ngano vikue pamoja.

Ukisoma Bible utaweza Kujua Mungu ni nani hasa, pia Yesu naye ni nani.
 
Back
Top Bottom