blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,278
- 7,966
- Thread starter
-
- #141
Asili za babu zetu ni wapi?Unaweza kuthibitisha uchawi upo na si hadithi tu?
Babu zetu walipowaona wazungu wana redio, na wanaweza kutabiri kupatwa kwa jua, waliwaita wachawi.
Je, kutumia redio ni uchawi? Kuweza kutabiri kupatwa kwa jua ni uchawi?
Unajuaje kwamba unachofikiri wewe ni uchawi leo si kitu ambacho kinaweza kuelezewa vizuri tu kesho bila uchawi kama leo tunavyoweza kuelezea redio na kupatwa kwa jua, vitu ambavyo babu zetu waliviona uchawi, bila kuhitaji nadharia ya uchawi ?
Ok, mkuu nijuze kadri ya uelewa wako
1.Ni nini asili ya viumbe Duniani,vinaendeshwa na nani na nguvu toka kwa nani?
2.Unaelewa nini juu ya mwili, Roho,Nafsi,Uzima na Kifo?
3. Kabla ya vitu hivyo unavyoviona kulikua na nn na nini hatima yake?
Muale wa mwanga unaoenda katika spidi ya mwanga una experience muda wote kwa pamoja, muda uliopita, uliopo na ujao wote uko pamoja.4. Kila kilicho na mwanzo huwa na mwisho je ni nini mwanzo wa wa hii dunia na mwisho wake ni nini?
Kwa kunjibu hayo maswali naomba sasa uthibitishe kwamba Mungu hayupo.
Thibitisha nawewe kama kweli babu zetu waliwaona wazungu ni wachawi kisa tu wanaweza kutabiri yajayo! Kama si hadithi tu hizo.Unaweza kuthibitisha uchawi upo na si hadithi tu?
Babu zetu walipowaona wazungu wana redio, na wanaweza kutabiri kupatwa kwa jua, waliwaita wachawi.
Je, kutumia redio ni uchawi? Kuweza kutabiri kupatwa kwa jua ni uchawi?
Unajuaje kwamba unachofikiri wewe ni uchawi leo si kitu ambacho kinaweza kuelezewa vizuri tu kesho bila uchawi kama leo tunavyoweza kuelezea redio na kupatwa kwa jua, vitu ambavyo babu zetu waliviona uchawi, bila kuhitaji nadharia ya uchawi ?
Binadamu - Wikipedia, kamusi elezo huruAdamu maana yake ni damu yaani kwa kifupi mwana wa damu watu wote ni wana wadamu sababu damu ndiyo uhai wetu, labda wewe useme hutumia damu, kwahiyo huwezi kukwepa kutokuitwa binadamu.
Kabla sijakuthibitishia, naomba uniambie uthibitisho wa aina gani utakuridhisha?Thibitisha nawewe kama kweli babu zetu waliwaona wazungu ni wachawi kisa tu wanaweza kutabiri yajayo! Kama si hadithi tu hizo.
Sijui, lakini haiwezekani kuwa kwa Mungu mjuzi wa yote, mweye uwezo wote na upendo wote.Asili za babu zetu ni wapi?
Mkuu usijisumbue kutafuta "kumwelewa" MUNGU, huwezi hata siku moja kumwelewa MUNGU wala kuyajua mawazo yake na akili zake. Unachotakiwa wewe kukifanya ni KUTII tu basi. Zitii Amri zake na uyashike mafundisho yake, uwe tajiri au uwe maskini jukumu lako kama mwanadamu ni KUTII tu basi.Je’ ni kweli kila kitu ni mpango wa Mungu? Kwa muujibu wa biblia yapo maandiko mengi ambayo kwakweli yana hitaji tafakari nzito, kuyaelewa. baadhi ya maandiko ya biblia…Ni kama haya.
Nakama hujui tu asili yako na babu zako! Huoni kama unajitaabisha kuhu mambo ya Mungu na pia hujui unalo lisimamia?Sijui, lakini haiwezekani kuwa kwa Mungu mjuzi wa yote, mweye uwezo wote na upendo wote.
Ingekuwa hivyo, asingeachia wauzwe utumwani miaka mingi wapate shida sana.
Tena kwa wazungu ambao walidai wanamjua sana huyo Mungu.
Unaamini habari hizi?
Mungu yupo, kawaachia mababu zetu wauzwe utumwani miaka yote hiyo?
Au utataka nithibitishe mababu zetu waliuzwa utumwani pia?
Hapana.Nakama hujui tu asili yako na babu zako! Huoni kama unajitaabisha kuhu mambo ya Mungu na pia hujui unalo lisimamia?
Nime like comment zako si kwamba ni nzuri ila juhudi yako unayoifanya kumjua Mungu..Jifunze na usifanye Moyo wako kuwa Mugumu Mungu ni mwema naamini ipo siku atajifunua kwako nawe utamjua na kamwe hutomwacha. Endelea kudadisi na kutafuta juu ya uwepo wake.Sijui,na kutokujua kwangu tu kunaonesha hakuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Angekuwepo na kama yeye ndiye asili ya vyote hivi, angeweka wazi kiasi ya kwamba kusingekuwa na mjadala asili ya hivi vyote ni nini.
Pia,dhana nzima ya asili ya hiki ni nini na asili ya kile ni nini inafanya kazi kama tunaongelea vitu vya middle to large scale in the universe. Ukienda huko chini kabisa katika quantum level, cause and effect, the essential idea behind "asili ya hiki ni nini" inavunjika. Concept nzima ya cause and effect inavunjika, the universe becomes probabilistic.
Kati ya hivyo, vinavyothibitishika kwamba vipo ama physically ama as a state ni mwili uzima na kifo, roho, na nafsi ni nini?
Vitu gani? Be specific please. Pia, swali lako bado limejikita katika msingi wa "cause and effect". Narudia, cause and effect is not fundamental,it is only evident at the mid tolarge scale levelof the universe, if you go deep enough, at the quantum levelfor example, cause and effect breaks down. The universe becomes probabilistic.
Muale wa mwanga unaoenda katika spidi ya mwanga una experience muda wote kwa pamoja, muda uliopita, uliopo na ujao wote uko pamoja.
Dhana nzima ya muda ni mazingaombwe unayoyaona kwa sababu wewe huwezi kwenda kwa speed ya muale ya mwanga, ungeweza, kungwkuwa hakuna muda.
Dunia imeanza kamasehemu iliyojimega kutoka jua (read Laplace) na itaishia kuunguzwa na jua litakapopanuka miaka bilioni 5 ijayo, kama si kabla.
Ambacho hakipo, nje ya dhana na mantiki, hakithibitishiki kwamba hakipo, kwa sababu hakipo ili kithibitishike kwamba hakipo, na kingekuwepo kithibitishike kwamba hakipo, kisingewezakuthibitishika kwamba hakipo, bali kingethibitishikakwamba kipo.
Uthibitisho, nje ya dhana na mantiki, ni uwanja wa vilivyopo, si uwanja wa visivyopo.
Nishathibitisha kimantiki kwamba Mungu hayupo (proof by contradiction, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote angekuwepo,dunia aliyoiumba isingekuwa na baya lolote.Dunia ina mabaya mengi, hivyo, Mungu huyo hayupo)
Hujaweza kuupinga uthibitisho huu.
Kama unasema Mungu yupo, ni kazi yako kuthibitisha Mungu yupo.
Hujaweza kuthibitisha hilo.
Huwezi kumwelewa Mungu.Mkuu usijisumbue kutafuta "kumwelewa" MUNGU, huwezi hata siku moja kumwelewa MUNGU wala kuyajua mawazo yake na akili zake. Unachotakiwa wewe kukifanya ni KUTII tu basi. Zitii Amri zake na uyashike mafundisho yake, uwe tajiri au uwe maskini jukumu lako kama mwanadamu ni KUTII tu basi.
Hakuna kiumbe anayemwelewa MUNGU, siyo Malaika, wala siyo Mashetani, wala siyo Wanadamu, wala siyo Wanyama, hakuna anayeweza kumwelewa BWANA MUNGU. Isipokuwa tu viumbe wake wote wanauwezo wa kuamua KUMTII na kufanya vile anavyotaka yeye. Tena yeye hamlazimishi kiumbe yeyote yule KUMTII, amewapa viumbe vyote hiari ya kuamua KUTII au KUASI.
Wale wanaochagua kutii amewatengea zawadi(neema) ya kuishi naye MILELE sababu yeye MUNGU ni wa milele; na wale wanaochagua KUASI amewatengea adhabu na kifo cha milele vile vile. Sasa basi kutokana na hoja yako, ni kweli ndiyo MUNGU anajua kila kitu na anapanga matukio, lakini MUNGU hakupangii utende dhambi au utende mema.
Ukisoma kitabu cha MWANZO utaona kuna mahali BWANA MUNGU anamwambia Kaini hivi;
"kwanini una ghadhabu? Na kwanini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde". MWANZO 4:6-7
Hivyo basi kutokana na maneno hayo hapo juu ya MUNGU kila unalolitenda ni hiari yako mwenyewe, MUNGU hakupangii utende mema au mabaya, uamuzi ni wako. Isipokuwa yeye kama MUNGU anaweza akaamua uwe Mfalme, au akakupa Utajiri, au uwe na watoto wangapi, n.k. lakini ni kwa kusudi maalumu. Yeye huwa na makusudi yake, na makusudi yake ni kwa faida ya wengi, siyo kwa faida ya mtu mmoja. Hata hivyo makusudi yake hayakufanyi wewe utende dhambi au mema na ndiyo maana mwisho wa siku ameweka hukumu.
Mkuu blackstarline fahamu kwamba huwezi KUMWELEWA BWANA MUNGU; akili zake wala mawazo yake hayachunguziki. Wewe jitahidi kumtii, kuzishika Amri zake, maagizo yake na imani ya YESU KRISTO na siku moja utamwona uso kwa uso.
Thibitisha Mungu yupo.Nime like comment zako si kwamba ni nzuri ila juhudi yako unayoifanya kumjua Mungu..Jifunze na usifanye Moyo wako kuwa Mugumu Mungu ni mwema naamini ipo siku atajifunua kwako nawe utamjua na kamwe hutomwacha. Endelea kudadisi na kutafuta juu ya uwepo wake.
Mimi nimeshashuhudia matendo makuu yake na amani niliyonayo moyoni kamwe haielezeki...hata sasa nina ujasiri wa kusema Mungu yupo tena ni mwema sana na fadhili zake hazichunguziki walio wake tunamjua naye tulio wake anatujua pia!
Kidogo sasa unaelekeaKwanini ajitekenye mwenyewe na kucheka mwenyewe?
Mungu wako hana kazi ya muhimu zaidi ya kufanya michezo ya kuigiza?
Hiyo ni hiari yako kuamini kama yupo au kutoamini, hakuna anayekulazimisha wala yeye MUNGU hakulazimishi uamini. Lakini amini usiamini, ipo siku inakuja, aliyoiandaa yeye mwenyewe MUUMBA wa mbingu, dunia na vyote vilivyomo; siku hiyo utajua kuwa hakika yeye ni BWANA MUNGU na hakuna mwingine na mbele yake utapiga magoti!Huwezi kumwelewa Mungu.
Kwa sababu hayupo.
Sitaki kuamini. Nataka kujua.Hiyo ni hiari yako kuamini kama yupo au kutoamini, hakuna anayekulazimisha wala yeye MUNGU hakulazimishi uamini. Lakini amini usiamini, ipo siku inakuja, aliyoiandaa yeye mwenyewe MUUMBA wa mbingu, dunia na vyote vilivyomo; siku hiyo utajua kuwa hakika yeye ni BWANA MUNGU na hakuna mwingine na mbele yake utapiga magoti!
Mark my words mkuu Kiranga , time will tell.
Hapo kuna vitu viwili,kwanza ni mtazamo wako kuwa jua linawaka na pili ni huo ukweli kuwa jua linawaka.Uthibitisho hauwezi kuwa mtazamo uliosahihi?
Nikilitazama jua, linawaka, nikasema kwa mtazamo wangu jua linawaka hapa,na kweli jua linawaka, huomtazamo wangu hauendani na ukweli na hivyokuwa mtazamo sahihi ambao pia upo katikauthibitisho kwamba jua linawaka hapo nilipo?
Sawa mkuu nimekwelewa vizuri sana, swali kabla sijatenda dhambi Mungu anajua nitatenda dhambi?Wale wanaochagua kutii amewatengea zawadi(neema) ya kuishi naye MILELE sababu yeye MUNGU ni wa milele; na wale wanaochagua KUASI amewatengea adhabu na kifo cha milele vile vile. Sasa basi kutokana na hoja yako, ni kweli ndiyo MUNGU anajua kila kitu na anapanga matukio, lakini MUNGU hakupangii utende dhambi au utende mema.
Mtazamo hauwezi kuwa katika kweli ukaendana na uthibitisho?Hapo kuna vitu viwili,kwanza ni mtazamo wako kuwa jua linawaka na pili ni huo ukweli kuwa jua linawaka.
Sasa wewe umeona kabisa kuwa jua linawaka(uthibitisho) halafu tena unasema kwa mtazamo wako jua linawaka!!!
Bado tunarudi pale pale tu mtazamo na uthibitisho.
Wewe unaongea pumba tupu,nakwambia hivi ukizungumzia suala la Mungu ujue unazungumzia jambo la imani.Imani haijadiliwi, ukishaingia katika mjadala, huku unafikiri unajadili imani, wewe ndiye uliyepotea njia.
Kuna watu kibao hawajadili imani zao hapa, kwa sababu wanajua suala zima la kujadili imani ni mufilisi wa mawazo.
Mimi najadili facts, sijadili imani.
Imani unaruhusiwa kuamini chochote unachotaka.
Lakini, katika facts, Mungu hayupo.
Ndiyo maana huwezi kuthibitisha kwamba yupo factually