Ok, mkuu nijuze kadri ya uelewa wako
1.Ni nini asili ya viumbe Duniani,vinaendeshwa na nani na nguvu toka kwa nani?
Sijui,na kutokujua kwangu tu kunaonesha hakuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Angekuwepo na kama yeye ndiye asili ya vyote hivi, angeweka wazi kiasi ya kwamba kusingekuwa na mjadala asili ya hivi vyote ni nini.
Pia,dhana nzima ya asili ya hiki ni nini na asili ya kile ni nini inafanya kazi kama tunaongelea vitu vya middle to large scale in the universe. Ukienda huko chini kabisa katika quantum level, cause and effect, the essential idea behind "asili ya hiki ni nini" inavunjika. Concept nzima ya cause and effect inavunjika, the universe becomes probabilistic.
2.Unaelewa nini juu ya mwili, Roho,Nafsi,Uzima na Kifo?
Kati ya hivyo, vinavyothibitishika kwamba vipo ama physically ama as a state ni mwili uzima na kifo, roho, na nafsi ni nini?
3. Kabla ya vitu hivyo unavyoviona kulikua na nn na nini hatima yake?
Vitu gani? Be specific please. Pia, swali lako bado limejikita katika msingi wa "cause and effect". Narudia, cause and effect is not fundamental,it is only evident at the mid tolarge scale levelof the universe, if you go deep enough, at the quantum levelfor example, cause and effect breaks down. The universe becomes probabilistic.
4. Kila kilicho na mwanzo huwa na mwisho je ni nini mwanzo wa wa hii dunia na mwisho wake ni nini?
Muale wa mwanga unaoenda katika spidi ya mwanga una experience muda wote kwa pamoja, muda uliopita, uliopo na ujao wote uko pamoja.
Dhana nzima ya muda ni mazingaombwe unayoyaona kwa sababu wewe huwezi kwenda kwa speed ya muale ya mwanga, ungeweza, kungwkuwa hakuna muda.
Dunia imeanza kamasehemu iliyojimega kutoka jua (read Laplace) na itaishia kuunguzwa na jua litakapopanuka miaka bilioni 5 ijayo, kama si kabla.
Kwa kunjibu hayo maswali naomba sasa uthibitishe kwamba Mungu hayupo.
Ambacho hakipo, nje ya dhana na mantiki, hakithibitishiki kwamba hakipo, kwa sababu hakipo ili kithibitishike kwamba hakipo, na kingekuwepo kithibitishike kwamba hakipo, kisingewezakuthibitishika kwamba hakipo, bali kingethibitishikakwamba kipo.
Uthibitisho, nje ya dhana na mantiki, ni uwanja wa vilivyopo, si uwanja wa visivyopo.
Nishathibitisha kimantiki kwamba Mungu hayupo (proof by contradiction, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote angekuwepo,dunia aliyoiumba isingekuwa na baya lolote.Dunia ina mabaya mengi, hivyo, Mungu huyo hayupo)
Hujaweza kuupinga uthibitisho huu.
Kama unasema Mungu yupo, ni kazi yako kuthibitisha Mungu yupo.
Hujaweza kuthibitisha hilo.