Je, inawezekana matumizi ya aina fulani ya pedi yakabadili 'flow' ya damu ya hedhi?

Je, inawezekana matumizi ya aina fulani ya pedi yakabadili 'flow' ya damu ya hedhi?

Nimekuwa mtumiaji wa pedi hizi aina ya Human Cherish maarufu kama HQ. Nilitokea kuzipenda kutokana na hali yake ya ubaridi kama air condition na harufu yake nzuri ya aerobic tea.

Lakini nimegundua pad hizi si salama na zinaweza kuwa chanzo cha matatizo mengi kwa wanawake hapo baadae.
Kwa uzoefu wangu na baadhi ya watu niliowauliza, unapotumia pedi hizi damu hutoka kidogo sn kuliko kawaida na mzunguko humalizika kabla ya siku za kawaida.
Kwa kulithibitisha hili nilibadili aina ya pedi katikati ya mzunguko na damu zikaongezeka kama kawaida na wakati wa kuchange nikatumia HC na flow ikarudi katika hali ya vitone.

Je wahusika wanatwambia nini kuhusiana na tatizo hili la pedi zao? Je usalama wa afya zetu za uzazi utaachwa salama?
Wanawake wenzangu tujihadhari sana na ikiwezekana tuchukue hatua ya kuzikimbia.
f1b279e1e3be8b81c64dbf78f52a13af.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
ila hii ni pantliner .hizi zina madhara sio za hq tu
 
Mtoa mada uko tayari kuwa sampuli ya majaribio(case study)?

Sikatae maoni yako lakini kibiashara sio sawa, inachukua muda mrefu sana na gharama kubwa mtu/mfanyabiashara/mvumbuzi kukitengeneza kitu chake mpaka kikakubalika sokoni.

Vyakula/dawa na vitu vyote vinavohusiana na afya ya binadamu vinapitia hatua mbalimbali kabla havijapitishwa na mamlaka husika, hivo hivo kwa padi za HC.

Hatukatai kuna madhara ambayo hayakutegemewa au hayakuonekana wakati wa majaribio hivo hayana budi kutolewa taarifa wakati wa matumizi kama hilo la kwako kama ni kweli linaletwa na pedi za HC.

Kuhusu tatizo lako ni vema uwaone madakitari wa kina mama watakufanyia uchunguzi na kuangalia historia ya maisha yako,vitu kama aina ya pedi unazotumia ni baathi ya maswali yatakayomsaidia mtoa afya.

Kutokana na hayo mimi nafikiri sio sawa wala uungwana kuhitimisha moja kwa moja na kushauri wanawake wenzako wasitishe matumizi ya pedi za HC. Ni bora malalamiko yako ukayapeleka kwa wasambazaji anuani yao ipo kwenye hizo pedi,nafikiri ni mgulani, itakusaidia wewe wao na watumiaji wote wa HC
 
Mmmmmm maana tokea nimeanza kutumia HC nikitumia mbadala naumwa tumbo ila nahilo swala la kiwango cha dam kupungua pia nimekiona japo sikuwazA kama ni tatizo
 
kuna always moja ile ambayo pink yake imekolea sana inawasha balaa sijui ni ya nchi gani kuna siku nilivua chupi barabarani
[emoji39] [emoji39]

sent from my samsung galaxy s8+ using jamiiforums mobile app
 
Nimetumia miaka sijawahi kupata shida yoyote!!
Hayo matatizo ni kwa baadhi yenu.
Sioni kama ni vyema kuhitimisha ati zinaharibu mzunguko wa hedhi hadharani.
Pia wengine tukitumia hizo always, freestyle na nyinginezo tunapata fangasi na miwasho mpaka michubuko.
Generally pedi zote usalama wake inategemeana na mwili wa muhusika


Rubiikimimi[emoji85]
Kweli kabisa muhenga. Mi nazipenda balaa
 
Hizo za ndani kwa ndani zikoje jamani??? Damu inaenda wapi sasa???


Damu inajilundika ukienda kuitoa unafanya kama unaenda haja kubwa kwa kuisuma inatoka mfululizo! sio nzuri kabisa sijui kwanini wanawake wanazipenda
 
Kiukweli pad zinategemea na mtu na mtu kuhusu always, freestyle rose sijui HC au HQ kwa wengine ni pad nzuri na haiwezi kukuaibisha kirahisi...
 
Hahahahaha, ndugu yangu twende pm

kudu ukudulie umande, mvua haina ukuduzi
Ungeweka hapa basi tuelimike wote..mie najitahidi sana kubadili pad ila huwa zinanichubua sijui kwa nini.natafuta mbadala wake

love thé love or hâte thé love.....
 
Back
Top Bottom