Je, inawezekana Waziri pale Uingereza kusafiri na timu ya mpira kama Man UTD au Man City au ni hapa kwetu tu?

Je, inawezekana Waziri pale Uingereza kusafiri na timu ya mpira kama Man UTD au Man City au ni hapa kwetu tu?

Badala ya kwenda shamba kuzalisha unaanzisha uzi wa waziri wa Tanzania vs England.
Una akili sawasawa kweli wewe?
Kwa hiyo hapa wewe uko shamba unazalisha? Yule ni waziri wa Tanzania na mm ni mtanzania nina haki ya kuhoji ninapoona mambo anayofanya ni kijinga
 
Wewe una roho mbaya kuliko hata roho mbaya yenyewe, kuna Shida Gani waziri wa michezo kwenda kuipa nguvu timu iliyotinga fainali, unadhan kuingia fainali ni rahisi?
Hakuna kitu kama hicho kuna uhusiano mdogo sana au haupo kabisa kati ya kiongozi fulani mkubwa kuwepo uwanjani na timu kushinda mechi. Ni mara ngapi tumeshuhudia acha waziri pm vp na hata rais mwenyewe kahudhuria uwanjani na bado tukapigwa tena mbele mashabiki karibia elfu 60? Serikali iachane na cheap popularity kinachoweza kuleta mageuzi kwenye michezo sio hizi mbwembwe lazima serikali ije na sera madhubuti zinazozalisha kizazi shindani kinachoweza kushinda katika mazingira yoyote, ukishaweza hilo mashabiki na watia hamasa watajitengeneza wenyewe.
 
Hii kauli ulitakiwa uiseme pia wakati wa Waziri wa Elimu na Michezo kipindi Fulani alipokwenda na timu ya Simba Misri kwa ajili ya mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Africa.

Waliokuwepo watamtaja waziri hiyo kama kumbukumbu zangu zimenihudumia sawasawa.
Huo wote ni utoto unaodumaza maendeleo ya michezo yakiwemo hayo mawazo yako
 
Binafsi hata mm nimeshangaa sana kumuona Hadi Raisi wa TFF naye kasafiri kwenda Algeria kiufupi hii kampeni tu sjui wamefuata nn kule karibia viongozi wengi wamenda
TFF Lazima wawepo kule, wana medali yao na wao kama ulikuwa hujui
 
Inaonekana mijitu mingi hapa JF haifatilii michezo wala siasa...
Juzi Vinicius junior kapigwa Red card ...Rais wa nchi yake kamuita Balozi wa Spain ..kutaka maelezo kuhusu ubaguzi...Hadi kadi ikafutwa...

Nyinyi mnashangaa waziri???
Sida tu, Mjinga, FIFA hsinaga huo ujinga wa Siasa, huyo Raisi wa Brazili anatafutavuungwaji mkono nchini mwake hakuna kitu hapo, Punguza Uchawa
 
Wewe mwenyewe unaweza kuwa ni tatizo vilele

Mara ngapi kazurula zurula na timu.

Mara ngapi timu za tz zimefika hatuna za namna hii.

Wanaenda maraisi wanchi kushangilia Mpira, katako waziri tena mwenye sekta yake unakuja kupigapiga kelele kwani kaenda kuangalia mambo nishatii au ya kimichezo
Ule ni ujinga na kujijenga kisiasa uwepo wake pale ni kuziba nafasi za watia hamasa kweli kweli wangeacha tuu waende washangiliaji waziri abaki kushughulikia sera ili aone na kujibu shida zilizojaa wizarani kwake.

Hatuzalishi wanariadha wazuri hatuzalishi wanasoka wazuri hatuzalishi wanamichezo wazuri licha ya kuwa na mazingira rafiki ya kufanya hivyo hata marefa wetu ni kama hawaaminiki kabisa huko duniani ukiacha malalamiko juu ya namna wanavyoboronga kuchezesha ligi yetu. Haya yalipaswa kumkosesha waziri usingizi.

Kwa sasa inachofanya hapa serikali ni kuzalisha mashabiki ukweli ni kwamba kwenye michezo mashabiki haijawahi kuwa tatizo mkiweza kujenga timu shindani ikashinda back to back walahi mashabiki wanajitengeneza tu
 
Imenishangaza sana kuona waziri mzima wa michezo badala ya kuwa bize kushughulikia sera ili ziinue michezo kuhakikisha taifa letu linag'ara kimichezo badala yake anazurula na ndege hadi Algeria.

Nadhani tuna tatizo kubwa sana linalopelekea tuwe na safari ndefu la kuinua michezo kama watungaji na wasimamizi wa sera ndio Hawa!!!
Hauwezi kufananisha tz na uk kwenye michezo. Tz bado tunajitafuta sana na kwasababu hiyo, sioni ubaya kwa timu kusafiri na waziri
 
Bongo mmekalia lawama tu kudadeki zenu.

Sasa kuna ubaya gani hapo, unaifananisha yanga na man u??
 
Imenishangaza sana kuona waziri mzima wa michezo badala ya kuwa bize kushughulikia sera ili ziinue michezo kuhakikisha taifa letu linag'ara kimichezo badala yake anazurula na ndege hadi Algeria.

Nadhani tuna tatizo kubwa sana linalopelekea tuwe na safari ndefu la kuinua michezo kama watungaji na wasimamizi wa sera ndio Hawa!!!
Nadhani tutofautishe mambo. Yanga iko stage ya juu kuitangaza nchi. Ni stage inayoangaliwa na Afrika nzima. Ni final. Siyo michezo ya kutafuta 16 bora wala kuingia robo final. Kimkakati kama nchi tunapaswa kuipa backup Yanga. #Yanga inacheza final ya Afrika. Michezo ni utalii, uchumi, biashara, ajira na uwekezaji. Waziri yuko sahihi kwa asilimia 100 kupiga kambi Algeria. 🙏🙏🙏
 
Nadhani tutofautishe mambo. Yanga iko stage ya juu kuitangaza nchi. Ni stage inayoangaliwa na Afrika nzima. Ni final. Siyo michezo ya kutafuta 16 bora wala kuingia robo final. Kimkakati kama nchi tunapaswa kuipa backup Yanga. #Yanga inacheza final ya Afrika. Michezo ni utalii, uchumi, biashara, ajira na uwekezaji. Waziri yuko sahihi kwa asilimia 100 kupiga kambi Algeria. 🙏🙏🙏
Sikia ndugu yangu waziri ni mlezi wa wizara yote ambayo ndani yake soka ni kipengele tu na hata huku kwenye soka waziri angepaswa kuumiza kichwa kujua ni Kwa nini tuliingiza timu nne lkn imefika moja final!! Hiyo back up haisaidii chochote zaidi ya kumjenga kisiasa huyo waziri tena ujenzi uchwara.

Sijajua ni Kwa nini Marais wetu hawateui mawaziri serious kusimamia hii wizara?
Kwa mawazo yangu kama serikali ikisuka vizuri hii wizara tutakuwa na mafinalist kwenye Kila mchezo
 
Hauwezi kufananisha tz na uk kwenye michezo. Tz bado tunajitafuta sana na kwasababu hiyo, sioni ubaya kwa timu kusafiri na waziri
Mimi nafikiri sisi ambao soka lipo chini ndio tulipaswa kufanya kazi ya ziada katika kushughulikia mambo hii wizara ikisimamiwa na waziri anayejitanbua itazalisha ajira nyingi sana na kutupatia fedha nyingi sana za kigeni kupitia wanamichezo
 
Sio kilakitu kujifananisha na wazungu!!! Sisi na mamboyetu wao kivyao istoshe rais annatafuta kiki ya kimichezo imbebe 2025 ya kitaifa imebuma hiyo siombaya!
Ferguson alivyoibenjua Bayer Munich UCL unakumbuka kilichifata? Football inanguvu sana huwezi kudharau NGUVU ya boli. Mbona anaendaga mavikao yasiyo na tija huko nje? Sinibora aende kuitia moyo timu ya wananchi
 
Mtoa post una kitu cha msingi naomba asipuuzwe..

Ongezea na serikali ya UK lini ilitoa ndege kuipeleka LIVERPOOL,AU MANCHESTER UNITED,AU MAN CITY,AU CHELSEA,AU ARSENAL kwenda kwenye fainali yeyote?
🤣🤣🤣Mama anaupiga mwingi🤔mitano tena kwa mama akeeee
 
Back
Top Bottom