Je, Kanisa Katoliki ndiye mnyama wa nne duniani wa Unabii wa Daniel na Ufunuo?

Je, Kanisa Katoliki ndiye mnyama wa nne duniani wa Unabii wa Daniel na Ufunuo?

Upo sawa kabisa na hilo andiko ila ulakini wangu huwa unakuja upi uhakika wa sabato hii ya jumamosi ya kalenda ya Gregory?

Kwasababu kulikuwa na taratibu za kuandama kwa mwezi na ujio wa sabato ndivyo walivyo hesabu hata miezi haikuwa hii ya Jan to Dec hapo bado pananipa wakati mgumu mgumu mgumu zaidi.


Hili somo ni JEPESI SANA nitakuelekeza inbox kwako.
Ila kwa sasa nitakuelekeza Yesu alifufuka siku ya kwanza ya Juma.

SIKU YA KWANZA YA JUMA AMBAYO HUWA MNASHEHEREKEA PASAKA KILA MWAKA NI JUMAPILI.

Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
Mathayo 28:1

Walipokwenda kutizama kaburi hawakumkuta Yesu walikuta amefufuka.

Kuhusu siku SIKU NI ZILE ZILE 30.
MWEZI MMOJA UNA SIKU 30.

HIZI kalenda za gregolian walipunguza siku na kuongeza kwa matakwa Yao binafsi..

Ukiona siku 28 ujue Mungu wao mwanamke anakuwa kwenye siku ZAKE..

Ila nitakuelekeza vizuri I hop utaenjoy na utanielewa
 
Makosa makubwa mno na ndipo upotofu wa wasabato ulipo. Dola ya Rumi sio Kanisa la Roma. Dola ya Roma ilihusika na kuwatesa baadhi ya mitume na kuwauwa, kama vile Petro na Paulo. Lakini sio Kanisa la Rumi. Kanisa la Rumi ndio lile ambalo Paulio analiandikia katika Waraka kwa Warumi na ndilo ambalo Petro alikuwa askofu wake wa kwanza na leo Francis (papa/baba) ni askofu wake wa 266!


Pole sana rafiki Nina kazi nzito ya kukuelekeza ila utanielewa.

Nitakupa masomo utasoma na I hop UTAELEWA TU brother.
 
Hizi ndiyo mind zinazo dig deep hata mimi naamini almost wengi tunaabudu tusichokijua hilo 666 ni mfumo ulioharibu kabisa Imani ya kweli.
Pole sana rafiki Nina kazi nzito ya kukuelekeza ila utanielewa.

Nitakupa masomo utasoma na I hop UTAELEWA TU brother.
Na mkitaka kujua 666 ina maanisha mnyama yupi katika Biblia (Ufunuo 13:18) basi ni Kaisari Nero. Ikiandikwa Kiebrania herufi zake zikipewa namba na kujumlishwa huja 666. Pia soma hapa:

The letters in Greek for “Nero” (Neron) add up to 1005. However, if the Greek letters for Nero Caesar (Neron Kaisar) are transliterated into Hebrew (nrwn qsr), the letter numbers add up to 666 (50 + 200 + 6 + 50 + 100 + 60 + 200 = 666).

Na utabiri huo wa Ufunuo ulishatimia!
 
Mbona unawashambulia wasabato.

Ingependeza kama ungejega hoja zenye ushahidi wa VITABU.

Nasikitika hata AMRI za Mungu huzijui masikini

UKRISTO SI LELEMAMA.
UKRISTO NI KUJIKANA KUCHUKUA MSALABA NA KUMFUATA YESU KILA SIKU. KWA UKAMILIFU WOTE .
Wewe mbona unashambulia wakatoliki!!?? Wasabato sio Wakristo ... Hamfuati mafundisho yake mnakuwaje Wakristo!!?
 
Wewe mbona unashambulia wakatoliki!!?? Wasabato sio Wakristo ... Hamfuati mafundisho yake mnakuwaje Wakristo!!?

MAFUNDISHO ya Yesu yasiyofuatwa na wasabato ni yepi mkuu.

Mi nadhani ingependeza ungekuwa unakuja na hoja kamili kuliko kurukaruka.

Leta hoja JINSI wasabato wanavyoasi Mafundisho ya Bwana Yesu kristo.
 
Mnyama wa kitabu cha Ufunuo

Watu wengi hawafahamu kuwa mnyama ni nani, na wengi wamejihusisha naye bila wao wenyewe kujua kama wanashiriki na mnyama. Lakini Mungu hajatuacha gizani, hivyo, kwa kupitia neno lake (Maadiko Matakatifu) tunaweza kumfahamu mnyama huyu aliyelezwa katika kitabu cha Danieli na Ufunuo.

Tunapaswa kuyaacha maandiko yajitafisiri yenyewe; kwa maana “hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2Petro 1:20-21. Hatupaswi kumuacha mtu flani atafsri unabii kwa jinsi yake mwenyewe, badala yake tunapaswa kuiacha Biblia ijitafsiri yenyewe.

Katika Danieli 7 wametajwa “wanyama wanne” ambao wanawakilisha falme nne. Kumbuka mmyama wa 4 aliyetajwa katika Danieli 7 ndiye mnyama aliyetajwa katika kitabu chote cha Ufunuo. Hivyo hapa tutaangalia sifa za mnyama wa nne wa kitabu cha Danieli, na mnyama wa kitabu cha Ufunuo, kisha tutaangalia ni wapi hapa duniani ambapo sifa za mnyama zinatimizwa kikamilifu.

1. Mnyama atakuwa na uwezo wa kisiasa na kidini (kanisa na serikali).

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona MWANAMKE, AMEKETI JUU YA MNYAMA mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”

Mwanamke au bibi-arusi katika unabii huwakilisha kanisa.

Ufunuo 21:2 “…Yerusalemu mpya…umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”

Ufunuo 21:9 “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.”

Mnyama huwakilisha taifa au ufalme

Danieli 7:17 “Wanyama hao…wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani”

Danieli 7:23 “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia…”

Kutokana na Ufunuo 17:3, mnyama huyu ana mwanamke aliyeketi juu yake, na kwa sababu unabii unatafisiri mwanamke kama kanisa, na mnyama kama taifa. Je kuna taifa au serikali ambayo imechanganywa pamoja na kanisa kama kitu kimoja? Ndiyo! Vatican, ni serikali au taifa ambalo limechanganywa pamoja na kanisa la Romani Katoliki kama kitu kimoja, na kuongozwa na mtu mmoja ambaye ni Papa.

2. Mnyama atakuwa na kanisa & serikali vimekaa juu ya milima 7.

Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana…mwenye VICHWA SABA na pembe kumi.”

Vichwa saba katika unabii vinawakilisha milima saba.

Ufunuo 17:9 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.”

Je hapa duniani kuna kanisa na serikali vimekaa juu ya milima saba?

“Ni ndani ya mji wa Roma, uitwao Mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la Serikali ya Vatican limewekewa mpaka kikamilifu.” –The Catholic Encyclopedia, p 529.

“Je vilima saba vya Roma ni nini?

Roma inajulikana kuwa imejengwa juu ya vilima saba. Roma ilisemwa imepatikana wakati Romulus na Remus, wana mapacha wa Mars, walifika katika futi ya kilima Palatine na wakauanzisha mji, Vilima sita vingine ni Capitoline (kiti cha serikali), Quirinal, Viminal, Esquiline, Caelian, na Aventine.” –Geography.about.com

ENCYCLOPÆDIA BRITANNICA
Vilima saba vya Roma

“…kundi la vilima juu au kuhusu ambapo mji wa Roma wa zamani ulijengwa. Mji wa awali wa Romulus ulijegwa juu ya kilima Palatine (#1) (Kilatini: Mons Palatinus). Vilima vingine ni Capitoline, (#2) Quirinal, (#3) Viminal, (#4) Esquiline, (#5) Caelian, (#6) na Aventine (#7) (Vinavyojulikana kimoja kimoja kwa kilatini kama Mons Capitolinus, Mons Quirinalis, Mons Viminalis, Mons Esquilinus, Mons Caelius, na Mons Aventinus).” –http://www.britannica.com/seo/s /seven-hills-of-rome/

Kwa hiyo unabii huu wa Ufunuo 17:3, unaonyesha wazi kuwa mwanamke aliyeketi juu ya mnyama, amekaa juu ya vilima saba vya mji wa Roma. Kwa vyovyote, ni Vaticani na kanisa la Romani Katoliki ambavyo vimekaa juu ya milima saba, na kutimiza unabii huu. Danieli 7:23 inasema mnyama wa mwisho (Roma) anatofautiana na wanyama wengine watatu waliopita. Kwa hakika hakuna taifa wala ufalme mwingine ambao una kanisa na serikali, harafu kwa wakati huo huo umekaa juu ya milima saba. Ila ni kanisa la Romani Katoliki pekee.

3. Mnyama atatoka baharini

Ufunuo 13:1 “Kisha nikaona mnyama AKITOKA KATIKA BAHARI, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”

Bahari katika unabii huwakilisha watu/jamaa, mataifa, lugha.

Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.”

Ukatoliki wa Romani ulitokea ulaya ya magharibi pamoja na makutano ya “watu/jamaa, mataifa, na lugha.” Na kwa wakati huu kanisa la Romani Katoliki lina idadi kubwa ya “watu, mataifa, na lugha,” kuliko kanisa jingine lolote duniani mwote. Na sasa, baada ya kuanzishwa kanisa moja duniani, Juni 26, 2000, Papa alichaguliwa kama kiongozi wa makanisa yote ambayo yameungana na lake. Hii ilifanya kanisa liongezeke mara mbili. Na hivi karibuni, makanisa yote pamoja na yasiyo ya Kikristo yatatangaza kwamba Papa ni kiongozi wao mwema.

Na Juni, 2008 mataifa 174 katika mataifa 192 duniani, yana serikali zao zikiwakilisha Vatican. Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabii huu kwa ukamilifu.

4. Mnyama atatawala miaka 1260. (kabla hajapata jeraha la mauti).

Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataadhimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake KWA WAKATI, NA NYAKATI MBILI, NA NUSU WAKATI.”

Ufunuo 12:6 “Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko mda wa SIKU ELFU NA MIA MBILI NA SITINI.”

Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake MIEZI AROBAINI NA MBILI.”

Danieli 7:25 inaonyesha muda ambao angetawala mnyama, kama wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. Ufunuo 13:5 inauonyesha mda huu wa utawala wa mnyama, kama miezi 42, miezi 42 = miaka 3 na 1/2. Hivyo, ukiangalia kwa makini hapa utaona kuwa, wakati = mwaka 1, na nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka.

Kwa hiyo, wakati nyakati mbili nusu wakati = miaka 3 na nusu ya Danieli 7:25, au miezi 42 ya Ufunuo 13:5, au siku 1260. Mahesabu haya yanathibitishwa katika Ufunuo 12:6 ambapo inasema, “Yule mwanamke (kanisa) akakimbilia nyikani…wamlishe huko mda wa siku 1260.” Kwa hiyo miaka 3 na 1/2 = miezi 42 au siku 1260 ambazo mnyama angetawala kabla hajapata jeraha la mauti.

Bado, wengine watakataa na kusema, hapana, miezi 42 haiwezi kuwa sawa na siku 1260, kwa sababu miezi mingine haina siku 30. Lakini katika unabii mwezi 1 = siku 30. Mwanzo 7:11 inasema, mvua za garika zilianza siku ya 17 ya mwezi wa pili, na Mwanzo 8:3, 4. inasema kuwa maji yakapunguka mwishoni mwa siku 150, harafu safina ikatua siku ya 17 ya mwezi wa saba. Hizo ni miezi 5 tangu mvua zilipoanza. Kama ukigawanya siku 150, kwa miezi 5, utapata siku 30 kwa kila mwezi. Hivyo, miezi 42 ikizidishwa kwa 30 jibu litakuwa 1260. Kwa hiyo wakati, nyakati mbili, na nusu wakati, ni sawa na miaka 3 na nusu, au miezi 42, au siku 1260. Kwa hakika, Ufunuo 12:6 inathibitisha mahesabu haya inaposema kuwa watoto wa Mungu watakimbilia nyikani kwa muda wa siku 1260 wakati wa utawala wa mnyama (upapa).

Katika unabii siku 1 ni sawa na mwaka 1,

Ezekieli 4:6 “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.”

Hesabu 14:34 “…siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka…”

Kutokana na Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34, ni hakika kwamba siku 1260 ni sawa na miaka 1260 ambayo Upapa ungetawala na kuwadhofisha watakatifu. Je hii ilitokea? Je unabii huu ulitimia? Au Je kuna ushahidi wowote unaothibitisha kuwa unabii huu ulitimia?

Kwanza kabisa tunatakiwa kujua ni lini kanisa la Romani Katoliki lilipata nguvu zote za kutawala kama “mwanamke juu ya mnyama” (kanisa na serikali), na kutawala kisiasa na kidini kwa wakati mmoja kama Ufunuo 17:3 inavyosema.

“Vigillius…alikalia kiti cha upapa (538 B.K.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius.” –History of the Christian Church, Vol. 3, p. 327

Hiistoria inathibitisha kuwa upapa umeanza utawala wake kama “kanisa na serikali” mwaka 538 B.K. juu ya amri ya mfalme Jastinian, na chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius. Na unabii unasema mnyama (upapa) atatawala miaka 1260 kabla haujapata jeraha la mauti.

Ukiongeza miaka 1260 katika mwaka ambao kanisa la Romani Katoliki lilianza kutawala kisiasa na kidini, mwaka 538 B.K., utapata 1798 B.K. Hivyo, unabii unasema utawala wa kwanza wa mnyama ungeisha 1798 B.K. Je utawala wa mnyama uliisha mwaka huo 1798 B.K?

“Katika mwaka 1798 Generali Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition

Kwa hakika, hizo ni miaka 3 na 1/2 au wakati, nyakati mbili, na nusu wakati, ambazo ni miezi 42 au siku 1260 za unabii ambazo mnyama angetawala kisha angepata pigo la mauti au kuchukuliwa mateka. Je mnyama alipata pigo la mauti mwaka huo 1798 B.K?

5. Mnyama atapokea jeraha la mauti.

Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake lake la mauti likapona…”

Ufunuo 13:10 “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga…”

Kama tulivyoona huko nyuma baada ya mnyama kutawala miaka 1260 angepata jeraha la mauti na kuuawa kwa upanga (upanga = vita). Baada ya mnyama kumaliza utawala wake wa miaka 1260, ambao ulianza 538 B.K. hadi 1798 B.K., Napoleon alimtuma Generali/Jemedari wake Berthier pamoja na jeshi lake, kwenda Roma kuuondoa utawala wa upapa.

“Katika mwaka 1798 Generali Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition

Napoleon alipomtuma Generali wake Berthier kwenda kumuondoa Papa madarakani, hapo ndipo jeraha la mauti lilipompata mnyama, na mwaka uliofuata 1799 B.K. Papa alikufa. Hii ndiyo sababu watoto wa kikatoliki katika parokia hufundishwa kuwa Napoleoni alikuwa mpinga Kristo.

“Nusu ya Ulaya walidhani…kwamba pamoja na papa upapa ulikuwa umekufa.” –Joseph Rickaby “The Modern Papacy” Lectures on the History of Religion, Lecture 24, (London Catholic Truth Society, 1910), p. 1

Lakini unabii ulisema kuwa jeraha hili lililompata mnyama lingepona. Je jeraha hili lilipona? Je utawala wa upapa ulipoondolewa madarakani na Generali Berthier ulipata nguvu zake tena?

6. Mnyama atapona jeraha lake la mauti.

Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, NA PIGO LAKE LA MAUTI LIKAPONA. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.”

Kama tulivyoona, upapa ulipata jeraha la mauti mwaka 1798 B.K. Vaticani ilibaki kama kanisa tu bila nguvu za kisiasa, na unabii ulisema jeraha hili lingepona. Je jeraha la mauti lilipona? Baada ya jeraha la mauti kutokea miaka kadhaa badaye katika mwaka 1929 B.K. Italia ikautambua mji wa Vaticani kama serikali ya kujitegemea, hii ilimfanya papa kuwa na nguvu tena kama mtawala wa kisiasa na kidini. kama unabii ulivyosema kwamba jeraha la mauti lingepona, na upapa ungerudishiwa tena uwezo wake wa kanisa na serikali kwa pamoja. Hebu angalia magaziti yaliyotoa taarifa hiyo jinsi waandishi wake walivyotumia lugha ya unabii bila ya wao wenyewe kujua.


Kusaini kwa Mussolini na (Kadinali) Gasspari mkataba wa kihistoria wa Romani

“Suala la Romani usiku huu lilikuwa ni jambo lililopita, na Vaticani ilikuwa katika amani na Italia…katika kuweka sahihi kwenye mkataba wa kukumbukwa kuponya jeraha la miaka mingi, uchangamfu wa kupindukia ulionyeshwa na pande zote.” –The San Francisco Chronicle. Feb. 11, 1929

Papa Amekuwa Kiongozi Wa Serikali Tena

“Roma, Juni 7.–Kutoka saa 5 kamili asubuhi hii kulikuwa na mtawala mwingine wa serikali ya kujitegemea duniani. Katika mda huo waziri mkuu Mussolini, kama waziri wa mambo ya nje Italia akimuwakilisha mfalme Victor Emmanuel–waziri mkuu wa kwanza Italia kuvuka kizingiti cha chini cha mlango wa Vaticani–akibadilishana na kadinali Gasspari, wakala wa serikali ya upapa, akimuwakilisha papa Pius XI, makubaliano ya mikataba yalisainiwa katika ikulu ya Lateran Feb. 11. Kwa kitendo hicho rahisi mtawala wa serikali ya kujitegemea ya mji wa Vaticani amekuwepo.” — New York Times July 7, 1929

Hivyo, unabii huu ulitimia kikamilifu na jeraha la mauti lililoupata upapa 1798 B.K. lilipona kabisa tangu 1929 B.K. mpaka leo kanisa la Romani Katoliki lina nguvu za “kisiasa na kidini” au “mwanamke juu ya mnyama.” Kwa kumaliza sehemu hii tunagundua kwamba mnyama huyu ndiye aliyekuwako, naye hayuko, na sasa yupo.


7. Mnyama aliyekuwako, naye hayuko, naye yuko.

Ufunuo 17:8 “Yule mnyama…alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari…”

Mnyama aliyekuwako: ni kanisa la Romani Katoliki tangu lilipoanza kutawala kama “kanisa & serikali” 538 B.K. na likaendelea mpaka. Napoleon alipomtuma Berthier kwenda kuuondoa utawala wa upapa. 1798 B.K.

…naye hayuko tokea 1798 B.K. mpaka kusaini kwa mkataba uliofanyika katika ikulu ya Lateran katika mwaka 1929 B.K. Vaticani ilikuwa kanisa tu bila uwezo wa kiserikali.

…naye yu tayari kutoka 1929 B.K. mpaka leo kanisa la Romani Katoliki lina nguvu za kisiasa na kidini, “kanisa & sesikali” au mwanamke juu ya mnyama.

8. Mnyama atabadili majira na sheria za Mungu.

Danieli 7:25 “…naye ataadhimu kubadili majira na sheria…”

Unabii huu ni ushahidi ulio wazi sana ambao karibu kila mtu hawezi kusumbuka kuelewa kwamba ni kanisa gani hapa duniani lililobadilisha sheria za Mungu. Ni kanisa moja tu la Romani Katoliki ndilo lililobadilisha sheria za Mungu kama Danieli 7:25 inavyodai kuwa. Kanisa la Katoliki limebadilisha sheria ya pili inayozuia kuchonga sanamu ya kitu chochote kile (angalia Kut 20:4). Katika katekism kanisa limeirarua amri ya 2 kisha likaigawa amri ya 10 katika sehemu mbili ili kuonyesha amri 10 zote. Lakini Je ni nani hapa duniani anayedai kuwa anauwezo wa kubadili amri za Mungu?

“Papa anauwezo wa kubadili majira, kubadili sheria, na kuachana na mambo yote, hata maagizo ya Kristo!” “Papa anayo mamlaka na mara nyingi ameyatumia, kuachana na amri ya Kristo.” –Decretal, de Tranlatic Episcop. Cap. (The Pope can modify divine law.) Ferraris’ Ecclesiastical Dictionary.

“Papa ni wa mamlaka kuu na nguvu kiasi kwamba anaweza kurekebisha, kuelezea au kutafsiri hata sheria za Mungu…Papa anaweza kurekebisha sheria ya Mungu, kwa sababu nguvu zake si za mwanadamu, bali ni nguvu za Mungu, na hutenda kama mwakilishi wa Mungu juu ya dunia.” –Lucius Ferraris,Prompta Ribliotheca, “Papa,” art. 2, translated.

Tangu kwamba papa ana mamlaka na maranyingi ameyatumia kubadili majira na sheria za Kristo, Je alibadili sheria ya Sabato? Je kanisa katoliki liliibadili Sabato ya siku ya saba ya wiki kwenda siku ya kwanza ya wiki? Kwa hakika kanisa lenye linakubali!

“Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons

“Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” –Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923.

“Swali: Siku ipi ni siku ya Sabato?
Jibu: Jumamosi ni siku ya Sabato.
Swali: Kwanini tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi?
Jibu: Tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa katoliki, katika balaza la Laodikia (364 BK) liliihamisha kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.” –The Convert’s Catechism of Catholic Doctrine,p. 50, 3rd ed.

“Kanisa la Romani (Katoliki) liliigeuza amri ya nne kwa kuiondolea mbali Sabato ya neno la Mungu, na kuanzisha Jumapili kama siku ya mapumziko.” –Nicholas Summerbell, History of the Christian Church, 3rd edition, 1873, p. 415 [Christian Church (Christian Connection)].

“Na ni wapi tumeambiwa katika maandiko kwamba tutunze siku ya kwanza kabisa? Tumeamriwa kutunza siku ya saba; lakini hakuna sehemu yoyote tuliyo amriwa kutunza siku ya kwanza. Sababu ya kutunza siku ya kwanza ya wiki kitakatifu badala ya siku ya saba ni kwa sababu ile ile kwamba tunatunza mambo mengine mengi, siyo kwa sababu ya Biblia, lakini kwa sababu kanisa, limeyaingiza [limeyaamuru].” –Isaac Williams, Plain Sermons on the Catechism, vol 1, pp. 334, 336 [Anglican].

Hivyo, kanisa la Romani Katoliki liliibadili sheria ya Sabato na kuwaamuru watu watunze jumapili badala yake. Na mwaka 1582. Papa Gregory XIII, alianzisha kalenda mpya. Kwa vyovyote, ni Vaticani ndiyo ilitimiza unabii huu kwa ukamilifu kabisa, hakuna jumuiya, wala shirika, wala sehemu yoyote ya kidini au isiyo ya kidini ambayo imetimiza unabii huu, kama ilivyo Vaticani. Ni kanisa la Romani Katoliki pekee ambalo lilibadili sheria, na majira, na kuamuru siku ihesabiwe kuanzia saa sita usiku kinyume na Maandiko yanayothibitisha kuwa siku huanza kuhesabiwa jioni.

Mwanzo 1:5 “Mungu akaiita nuru Mchana, na giza Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.”


9. Mnyama atanena maneno ya makufuru juu ya Mungu.

Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu…”

Ufunuo 17:3 “…nikaona mwanamke ameti juu ya mnyama…mwenye kujaa majina ya makufuru…”

Ufunuo 13:1 “…nikaona mnyama…mwenye…vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.”

Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena makuu, ya makufuru…”

Kukufuru katika Biblia inaelezewa kama hali ya mtu kujifanya yeye mwenyewe kama Mungu.

Yohana 10:33 “Wayahudi wakamjibu, kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwamadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.”

Je nani hujiita na kujifananisha na Mungu hapa duniani?

“Papa siyo mwakilishi tu wa Yesu Kristo, yeye ni Yesu Kristo mwenyewe, amejificha chini ya uficho wa mwili.” –Catholic National July 1895.

“Kwa kuwa wewe u mchungaji, wewe u tabibu, wewe u mwongozaji, wewe u mkulima, hatimaye wewe u Mungu mwingine duniani.” –Labbe and Cossart’s “History of the Councils.” Vol. XIV, col. 109

“Tunapachukulia juu ya dunia hii sehemu ya Mwenyezi Mungu…” –Pope Leo XIII Encyclical Letter of June 20, 1894,

Katika “The Bull Unam Sanctam” iliyotolewa na Papa Boniface VIII inasomeka kama ifuatavyo…
“Papa wa Roma huukumu watu wote, lakini yeye haukumiwi na mtu. Tunatangaza, kutetea, kuelezea, na kutamka; kutawaliwa na Papa wa Roma ni kwa kila kiumbe cha mwanadamu muhimu kwa ajili ya wokovu ambao ulisemwa na Kristo ‘Ameviweka vitu vyote chini ya miguu yake’ inaonekana vizuri imethibitishwa kwangu…Nina mamlaka ya Mfalme wa Wafalme. Mimi ni yote katika yote na juu ya yote, hivyo basi, Mungu Mwenyewe na mimi, kasisi wa Mungu tuna usawa mmoja, na ninaweza kufanya yote ambayo Mungu anaweza kufanya.”

“Mwokozi mwenyewe ni mlango wa zizi la kondoo; ‘Mimi ni mlango wa kondoo’. kwenye zizi hili la Yesu Kristo, hakuna mtu anayeweza kuingia mpaka awe ameingizwa na Papa mtawalawa na ni pale tu kama wameunganika naye ndipo wanadamu wanaweza kuokolewa, kwa sababu Papa wa Roma ni kasisi wa Kristo na ni mwakilishi wake kwa nafisi duniani.” –(Pope John XXIII in his homily to the Bishops and faithful assisting at his coronation on November 4, 1958).

Kudai kuwa Mungu duniani Biblia inathibitisha kuwa ni kukufuru ju ya Mungu aliye hai. Kufuru nyingine ni kudai kuwa na uwezo wa kusamehe dhambi.

Marko 2:7 “Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi ispokuwa mmoja, ndiye Mungu?”

Je makuhani wa kanisa la Romani Katoliki hudai wana uwezo wa kusamehe dhambi?

“Kuhani kiukweli kabisa husamehe dhambi kwa uwezo aliopewa na Kristo.” -Joseph Devarbe’s Catechism, p. 279

“Dhambi zinaweza kusamehewa kupitia sakramenti pekee…wote makuhani na sakramenti ni vifaa ambavyo Kristo anavitumia kukamilisha msamaha ndani yetu na neema ya utakaso.” -Catechism of Trent, p. 115.

“Haya mamlaka ya jaji (Judicial authority) yatajumuisha hata uwezo wa kusamehe dhambi.” –[The Catholic Encyclopaedia Vol 12, -article “Pope” pg 265]

“Na Mungu mwenyewe analazimika kufungwa na hukumu ya kuhani wake na ama kutokuomba msamaha au kuomba msamaha, kutokana na kama wanakataa kutoa ukamilifu, unaotoa toba inayoridhisha.” –Liguori, «Duties and Dignities of the Priest», p.27

10. Mnyama ana jina lenye namba 666.

Ufunuo 13:17 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, ispokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Ufunuo 13:18 “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinaadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.”

Biblia inatuambia kuwa hesabu au namba ya jina la mnyama ni 666

Kanisa la Romani Katoliki hudai kuwa Papa ni kichwa cha kanisa au mwakilishi wa Yesu.

“Maneno yaliyoandikwa katika kofia (miter) ya Papa ni haya, ‘VICURIUS FILII DEI’. ambayo ni ya kilatini kwa ajili ya ‘KASISI WA MWANA WA MUNGU’. Wakatoliki huchukulia kwamba kanisa, ambalo ni jumuiya ya kuonekana, lazima liwe na kichwa cha kuonekana. Kristo, kabla ya kupaa kwake kwenda mbinguni, alimteua M.t. Petro kuwa kama mwakilishi wake…hata hivyo Askofu wa Roma, kama kichwa cha kanisa, alipewa jina ‘KASISI WA YESU.'” –Our Sunday Visitor, (Catholic Weekly) “Bureau of information,” Huntington, Ind., April 18, 1915.

Kwa hiyo “VICARIUS FILII DEI” ndilo jina linalotumiwa na mamlaka ya Upapa na kumthibitisha Papa kama kichwa cha kanisa.

Helufi za kilatini zinaweza kutumika pia kama namba, na siku hizi hujulikana kama “Namba za Kirumi,” na helufi U inaweza pia kutumika kama V.


“VICARIVS FILII DEI”

(Kasisi wa Mwana wa Mungu)

V........5
I........1
C..... 100
A...... 0
R.......0
I........1
V.......5
S.......0
F........0
I.........1
L .......50
I.........1
I.........1
D........500
E.........0
I............1
Jumla= 666

Vicarius inamaanisha, katika nafasi ya
Filii Mwana
Dei Mungu
Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabi huu wa hesabu ya mnyama 666 kwa ukamilifu kabisa.

11. Onyo la Mungu kwa wote walio katika kanisa katoliki.

Mungu anaoya vikali sana juu ya wale wote ambao wanashirikiana na mnyama huyu, kama wewe ni mmojawapo unapaswa kuchukua uamuzi sahihi sasa bila kupoteza muda; kwa maana hukumu itakuja juu ya mnyama na yule kahaba (kanisa Katoliki) aliyekaa juu mnyama. Hili ni onyo la mwisho la upendo na la rehema kutoka kwa Mungu.

Ufunuo 14:9-10. “Na mwingine, malaika watatu, akafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.”

Ufunuo 19:20 “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;”

Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amemkumbuka maovu yake…Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemuhukumu ni mwenye nguvu.
Mnavyozidi kutusema, sisi wala hatujali..!! Nyie semeni, sisi ikifika Dominika tunaenda zetu kanisani, baada ya hapo tunaenda kwenye kitimoto na bia, then tunarudi home kupumzika. Ukitaka kujiunga na sisi, we tafuta kanisa lilipo kajieleze utaingia, hutaki tunakuacha na tunaendelea na maisha yetu..!! Wewe toa povu la foma gold sisi tunaendelea na maisha yetu ya ukatoliki..!!
 
MAFUNDISHO ya Yesu yasiyofuatwa na wasabato ni yepi mkuu.

Mi nadhani ingependeza ungekuwa unakuja na hoja kamili kuliko kurukaruka.

Leta hoja JINSI wasabato wanavyoasi Mafundisho ya Bwana Yesu kristo.
Tuanzie tu na EKARIST vipi mnakomunika kama makanisa mengine yote ya Kikristo !!
 
Unafikiri lengo la Yesu ni kutufanya tukopi kila maisha na matendo aliyotenda? Yesu alitolewa hekaluni akiwa mtoto na njiwa wakitokewa dhabihu. Lakini sio lengo la Yesu kwamba wafuasi wake waige utamaduni huo.

Yapo mambo ya msingi ambayo Yesu anataka wafuasi wake (wakristo) tuyafuate mfano kuu kuliko yote ni upendo.

1) Yesu ndio ameanzisha dini ya ukristo
2) Yesu dini yake ilikuwa ukristo
3) Yesu aliifanya ibada Kwa kupiga magoti kanisani ibada ikiongozwa na padri au mchungaji


1. Unafikiri ni nani alianzisha imani kwa Kristo? Yesu aliwachagua mitume na kuwafundisha kwa muda wa miaka 3 na kuwaamuru kuyashika yote na kuyaeneza duniani kote. Ndio hao tangu enzi za Yesu wanaitwa wafuasi wa Yesu aitwaye Kristo au kwa kifupi wakristo.

2. Yesu alizaliwa kati ya watu waliokuwa wa dini ya kiyahudi lakini hakuwa mfuasi typical wa uyahudi alikuwa mwanamapinduzi au critic wa dini hiyo. Uyahudi wa leo ni ule ule wa zama za Yesu. Yesu hakuwa mkristo ila Kristo mwenyewe. Wafuasi wake wanaitwa wakristo.

3. Yesu alisali mlimani akisimama, kukaa, kulala kifudifudi na kupiga magoti na hakuna shida katika hayo wala hakuyakataza kwa wafuasi wake. Mitume na mashemasi waliwaongoza watu kuomba na ndio hao hao wanaongoza ibada za sala na maombi leo waitwe wachungaji, mababa wa Kanisa (mapadri), mashemasi, etc sio hoja.
Ulichokiandika hapa ni mahubiri kama yale ya kanisani yanayoitwa DOGMA kuaminishana vitu vya uongo

Ila nashukuru umekubali kuwa Yesu dini yake sio ukristo

Kwahiyo hata wanafunzi wake hakuwafundisha dini ya ukristo Kwa sababu yeye mwenyewe haijui

Swali lipo pale pale wewe dini ya ukristo umeipata wapi?

Ni nani aliyekuambia uwe mkristo na ibada yako uifanyie kanisani ukiwa umepiga magoti na Padre akiwa mbele yenu anaongoza ibada?


Haya ni maneno ya mwisho Yesu aliwambia wanafunzi wake

Yesu akisikitika kuwa wanafunzi wake watatengwa na masinagogi na hao watakao watenga watafanya hayo Kwa kuwa hawamjui Yesu Wala Mungu

Yohana 16:1
Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
Yohana 16:2
Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
Yohana 16:3
Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.
Yohana 16:4
Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.
Yohana 16:5
Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi?


Hao waliowatenga wanafunzi wa Yesu na Masinagogi na kuwauwa ndio walioianzisha dini ya ukristo na ndio huyo mnyama 666
 
Ulichokiandika hapa ni mahubiri kama yale ya kanisani yanayoitwa DOGMA kuaminishana vitu vya uongo

Ila nashukuru umekubali kuwa Yesu dini yake sio ukristo

Kwahiyo hata wanafunzi wake hakuwafundisha dini ya ukristo Kwa sababu yeye mwenyewe haijui

Swali lipo pale pale wewe dini ya ukristo umeipata wapi?

Ni nani aliyekuambia uwe mkristo na ibada yako uifanyie kanisani ukiwa umepiga magoti na Padre akiwa mbele yenu anaongoza ibada?


Haya ni maneno ya mwisho Yesu aliwambia wanafunzi wake

Yesu akisikitika kuwa wanafunzi wake watatengwa na masinagogi na hao watakao watenga watafanya hayo Kwa kuwa hawamjui Yesu Wala Mungu

Yohana 16:1
Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
Yohana 16:2
Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
Yohana 16:3
Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.
Yohana 16:4
Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.
Yohana 16:5
Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi?


Hao waliowatenga wanafunzi wa Yesu na Masinagogi na kuwauwa ndio walioianzisha dini ya ukristo na ndio huyo mnyama 666
Kwani Yesu alianzisha Usabato? Unafikiri Yesu na wafuasi wake (wakristo) walikuwa wanafanya kusanyiko kila Jumamosi?
 
Kwani Yesu alianzisha Usabato? Unafikiri Yesu na wafuasi wake (wakristo) walikuwa wanafanya kusanyiko kila Jumamosi?
Sabato sio dini sabato ni siku ya ibada
Na Yesu alikuwa anafanya ibada siku hiyo ya Jumamosi

Luka 4:16
Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
Luka 4:17
Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
Luka 4:18
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,


Jibu maswali Kwa maandiko

1)Wewe ukristo umeupata wapi wakati Yesu na wanafunzi wake dini Yao haikuwa ukristo?

2)Nani aliyekuambia ufanye ibada kanisani ukiwa umepiga magoti na ibada iongozwe na Padre ?

3)Nani aliyekuambia Jumapili ni siku ya kufanya ibada

Ili tujue kuwa wewe sio zao la mnyama 666
 
Tuanzie tu na EKARIST vipi mnakomunika kama makanisa mengine yote ya Kikristo !!


Unareference ya Bible???

Naomba uwe unakuja na refence za bible.

MATHAYO 15:8.

Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

USILETE MAFUNDISHO YA WANADAMU LLETE BIBLIA.
 
Tuanzie tu na EKARIST vipi mnakomunika kama makanisa mengine yote ya Kikristo !!
Ekaristi Ni mapokeo ya Upagani


Alichoacha Yesu alisema tumege mkate na kutawazana Kama Yeye na wanafunzi wake


Waadventista wanafanya hivo
 
Ngoja kwanza wafausi wa paulo waparuane nipo hapa na 🍿
 
Hayo mambo ya kula hiki na kuacha kile wala Yesu hakusisitiza. Alisema sio kimwingiacho mtu kimtiacho unajisi bali kimtokacho. Inashangaza kwamba wasabato bado wameng’ ng’ana na Agano la Kale la mambo ya kimwili.

Waislamu wanaishika sheria ya kutokula nguruwe vizuri kuliko ninyi na haiwasaidii chochote kama ilivyo kwenu pia.
UNAPOTOSHWA NA WEWE UNAPOTOSHA

KUTOKUJUA MAANDIKO KUMEWAFANYA MNAUZIWA MAFUTA ,MAJI NA UDONGO



[https://www]

Log in

Habari na Hoja mchanganyiko

Wakristo wasio Wasabato wanaruhusiwa kula paka, panya, kobe, kinyonga, kenge, kunguru, nyani, n.k?

Thread starterNetMaster

Start dateNov 11, 2022

Tagskula mbwa nyani panya punda wakristo wasabato

1 of 7Next Last

NetMaster

JF-Expert Member

Nov 11, 2022

#1

Kwa kuwa sisi ni wakristo ni kwamba sisi tunafata nyayo za Yesu Kristo. Ni vipi kitu ambacho hakusema Yesu Kristo kinawekewa mabano ya kuweka uchambuzi wa maono ya waliotafsiri biblia? mbaya zaidi kuna biblia hata hayo mabano hayamo, uchambuzi umeunganishwa kuonekana ni maandiko matakatifu yaliyokuwemo kwenye biblia.

Kimuingiacho mtu hakimtii unajisi ni jibu alilotoa Yesu baada ya kuulizwa kwanini wanafunzi wake waliokuwa na njaa walikula mahindi wakiwa njiani bila kuosha mikono, kwa sheria walizojiwekea viongozi wa mda huo waliona kwamba kula bila kuosha mikono kunamtia mtu unajisi, Yesu ndipo akawasahisha kwamba sheria zao hazipo sawa na kwamba kula bila kuosha mikono hakumtii mtu unajisi. Sasa je, hapa kulikuwa na haja ipi ya watafsiri kuongeza maneno yao kwamba maana yake ilikuwa ni karuhusu kula vyakula ambavyo havikutakaswa kama mijusi, kenge na nguruwe wakati kilichokuwa kinazungumziwa ni kula bila kuosha mikono?

Wasabato walipuuzia hayo mabano maana hayakuwa maneno ya Yesu na kazi ya watafsiri sio uchambuzi, Wakristo wengine wakadhani ni Yesu kawapa kibali wakaona ni ruksa ya kula chochote.

Sasa najiuliza kwamba mbwa, konokono, vinyonga, kunguru, paka, chunusi, kobe, n.k wanaweza kuliwa?

Mfano kuna samaki na wanyama wana sumu ama huleta madhara wakiliwa na wakawekwa kwenye kundi la vyakula visivyofaa, Mungu alikosea kusema hawatakiwi kuliwa?

Halafu pia nashangaa Biblia za sikuhizi za kiswahili zimeunganisha hayo maneno bila kuweka mabano, ni wazi kabisa wakristo wengi wanaamini haya maneno yalikuwemo bila kujua kuna uhuni umefanyika kuyaunganisha, maskini mweee! Mtu anabisha mpaka mishipa inamtoka shingoni kwasababu ya mistari iliyopachikwa ambayo haikuwahi kuwepo, ni ujanja ujanja tu ukafanyika kupachika.



Reactions:makwega7, Interlacustrine E, mkwepu jr and 1 other person

NetMaster

JF-Expert Member

Nov 11, 2022

#2

Kwa kuwa sisi ni wakristo ni kwamba sisi tunafata nyayo za Yesu Kristo, Ni vipi kitu ambacho hakusema Yesu Kristo kinawekewa mabano ya kuweka uchambuzi wa maono ya waliotafsiri biblia ? mbaya zaidi kuna biblia hata hayo mabano hayamo, uchambuzi umeunganishwa kuonekana ni maneno ya Yesu Kristo.

Kimuingiacho mtu hakimdhuru ni jibu alilotoa Yesu baada ya kuulizwa kwanini wanafunzi wake waliokuwa na njaa walikula mahindi wakiwa njiani bila kuosha mikono, Je hapa kulikuwa na haja ipi ya watafsiri kuweka kwenye mabano kwamba maana yake ilikuwa ni kwamba Yesu karuhusu kula nguruwe wakati kilichokuwa kinazungumziwa ni kula mahindi bila kuosha mikono ??



Reactions:mkwepu jr

hamis77

JF-Expert Member

Nov 11, 2022

#3

Hakuna mabano katika Hilo andiko,yanayoruhusu kula kila kitu ila Wachungaji fake na manabii wauongo matapeli Kama kina mwamposa wasiojua maandiko ndio wanapotosha tafsiri , hata mwakasege anayesifiwa bado biblia inampiga chenga ,maana alifundishwa hivo

Hilo andiko Wala halina mabano ya kuruhusu Kula Mende,kenge,n.k hata wewe umeingia kwenye mtego was kina mwamposa , gwajima,n.k

BIBLIA HUMAANISHA NINI INAPOSEMA KIMUINGIACHO MTU AKIMTII UNAJISI BALI KIMTOKACHO?

Ni jambo gani ambalo Biblia inasema katika Marko 7:15-23?
Biblia Inasema

"Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. [Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.]


Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule mfano.
Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.
Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi."(Marko 7:15-23).
Sasa shida inayokuja hapa watu wameshikilia kula vyakula najisi kuwa ni halali kama vile kitimoto na kambare na wanasema inahusisha mwili tu, wanasahau Kuwa kukaidi agizo la Mungu ni matokeo ya uasi ambao uanzia kwenye maamuzi, Lakini pia wanasahau kuwa Yesu ametaja na mambo mengine yanayoweza kumtia mtu unajisi, kama vile ufisadi, uuaji, uzinzi, wivi, je hivi vinausisha roho tu? Je havina matokeo yoyote kwenye mwili kiasi cha mwili kuhusishwa? Inabidi wafikilie upya.

Katika Marko 7:15-23, Yesu hatamki kwamba mtu anaweza kula kitu chochote. Baadhi ya vyakula na vinywaji havistahili na pia vinafisha, na vingine ni hatari kabisa kwa afya. Angalia katika (Walawi 11:2-23) kwa ajili ya orodha ya wanyama, ndege, samaki, na wadudu wasiofaa kuliwa.

Anachoelekeza Yesu hapa ni imani kuwa endapo Myahudi mtaua (mcha Mungu kwelikweli) akifuata tu sheria za usafi wa taratibu za kidini atakuwa safi kimaadili/kiroho. Kwa upande mwingine, hakuna chakula ambacho kwa chenyewe kinaweza kuinajisi tabia ya mtu. Kinachonajisi ni mawazo maovu (ambayo hujitokeza kwa ndani na kujidhihirisha katika matendo ya nje). Ndiyo maana Biblia inatuambia, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” (Mithali 4:23)

Hapa Yesu hasemi kuwa vyakula vyote vinaruhusiwa au vinafaa kuliwa. Yesu anatumia vitendo vya nje vya kuosha mikono na kula kama kielelezo cha matendo ya nje ili kuweza kutofautisha na hali ya moyoni. Yesu hugeuza mtazamo wa walimu wa sheria, waliingiza mapokeo ambayo hayakuwa agizo la Mungu, miongoni mwa mapokeo hayo ni kunawa hadi kwenye kiwiko Kabla ya kula Biblia Inasema "Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao;" (Marko 7:3). Kwa hiyo hata kama ungekula chakula ambacho sio najisi kwao walikiita najisi kwa sababu tu haujanawa hadi kwenye kiwiko, na Habari hizi zilizua mjadala baina ya Yesu na mafarisayo na kuamua kuwaambia ukweli, Biblia Inasema "Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa,Watu hawa huniheshimu kwa midomoIla mioyo yao iko mbali nami;
Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundishoYaliyo maagizo ya wanadamu," (Marko 7:6-7).

Basi ingekuwa vyema kwa kila msomaji wa maandiko kutambua kuwa mgogoro ulianzia nyuma kwenye kutokunawa hadi kwenye kiwiko mpaka Yesu anafikia hatua ya kusema "kimuingiacho mtu akimtii unajisi, bali kimtokacho" mawazo ya mafarisayo yalishatiwa unajisi,
walikuwa wamejikita katika mambo ya nje, wakati Yesu alisisitiza matendo ya ndani ya roho, hali ya kimaadili/kiroho. Ni rahisi kudumisha hali ya nje ya kuwa Mkristo kwa kile tunachofanya au tusichofanya. Hata hivyo, wakati ambapo wanadamu huangalia nje, Mungu huangalia hadi ndani ya moyo hupima nia ya makusudi yanayosukuma matendo yetu. (Angalia pia Mwanzo 1:29-30; Matendo 10; 1 Wakorintho 10:31).

Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa hili.
 
Zimewekwa hoja ,zipinge kwa hoja ,wewe unasema hawana akili

Huoni wewe ndio huna akili
hizo siku za mwisho[nje kidogo ya mada]
'' hutaweza kuuza wa kununua bila chapa ya huyo myama 666'' Huu wakati hatujaufikia au ulipita? je unaamini papa atakujafanya hivyo? je nabii wa uongo atakua nani au ni nani? nieleweshe hapa
 
Back
Top Bottom